Taharuki Uingereza: Msako wa Usiku Manchester Wawatia Hofu Watu wa LGBTQ+

Taharuki Uingereza: Msako wa Usiku Manchester Wawatia Hofu Watu wa LGBTQ+

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Ripoti zinaeleza kuwa makundi ya vijana yamekuwa yakifanya msako wa usiku katika baadhi ya mitaa ya Manchester, nchini Uingereza, yakilenga kuwatafuta na kuwashambulia watu wa LGBTQ+, wakiwemo transgender na mashoga.

Tukio linalodaiwa kutokea hivi karibuni liliripotiwa katikati ya jiji la Manchester, karibu na eneo la Manchester Specialist Markets, ambako hali ya taharuki na vurugu ilizuka usiku.

Soma pia: Nchi 10 Zenye Idadi Kubwa ya Watu wa LGBTQ+ (2023/2024)

Video zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha makundi ya vijana wakiwa wamevalia jaketi na hoods wakikimbizana na kugombana mitaani. Katika baadhi ya picha, watu waliovalia mavazi ya kike wanaonekana wakihusika katika vurugu hizo.

Tukio hilo limeibua hofu kuhusu usalama wa watu wanaolengwa, huku video zikiendelea kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, kwa wakati huu, taarifa kamili kutoka mamlaka husika kuhusu chanzo cha vurugu hizo, wahusika na kama kuna watu waliokamatwa bado hazijawekwa wazi.


 
Mbaga Jr , hivi jana ulikuwa temeke au Manchester ! Angalia vizuri flight logs zako halafu ujiandae kutoa maelezo mahakamani kwanini unawatisha watu wenye ulemavu wa matako
 
Excellent, sisi kwa sasa ni Katiba, mengine tutayafix mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom