Tahasusi ipi kati ya PCM na PCB ina uwanda mpana wa kusoma kozi nzuri zinazoendana na hali ya Dunia ya sasa?

Tahasusi ipi kati ya PCM na PCB ina uwanda mpana wa kusoma kozi nzuri zinazoendana na hali ya Dunia ya sasa?

Combination ya PCB (Physics, Chemistry, Biology) na PCM (Physics, Chemistry, Mathematics) ni nzuri sana kwa maeneo mengi ya kusoma baada ya kidato cha sita. Hapa kuna baadhi ya kozi ambazo unaweza kuzifikiria kulingana na combination yako:

  1. Fani za Sayansi za Afya: Kama vile Udaktari, Daktari wa Meno, Pharmacy, Nursing, Medical Laboratory Science. Hizi zinahitaji PCB au PCM.
  2. Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia: Kama vile Computer Science, Software Engineering, Information Technology. Kwa hizi, PCM ni muhimu sana.
  3. Uhandisi: Aina mbalimbali za uhandisi kama vile Mechanical Engineering, Electrical Engineering, Civil Engineering. Kwa ujumla, PCM ni muhimu hapa.
  4. Sayansi ya Mazingira na Sayansi ya Ardhi: Kama vile Environmental Science, Geology, Geography. PCB inaweza kuwa na umuhimu kulingana na kozi unayoitaka.
  5. Sayansi ya Maabara: Kama vile Physics, Chemistry, au Biology lab technician. Hizi zinahitaji PCB.
  6. Biotechnology na Sayansi ya Chakula: PCB ni muhimu kwa kozi hizi.
Kwa hiyo, kuchagua kati ya PCB na PCM inategemea sana maslahi yako binafsi na malengo ya kazi ya baadaye. Ikiwa unapendelea masomo ya sayansi ya afya au biolojia, PCB inaweza kuwa chaguo bora. Kwa upande mwingine, ikiwa unaona una vipaji katika hesabu na unavutiwa na uhandisi au teknolojia ya habari, basi PCM inaweza kukufaa zaidi.

Kumbuka pia kwamba wakati wa kuchagua combination yako, ni muhimu kuzingatia vigezo vingine kama vile maoni ya wazazi, maelekezo ya shule au ushauri wa wataalamu wa elimu. Pia, fikiria sifa za vyuo vikuu au taasisi za elimu ya juu unazopenda kujiunga nazo ili kuhakikisha unakidhi mahitaji yao ya mchanganuo wa masomo.
 
Ndugu wadau, nilitaja kujua combination ipi kati ya PCB na PCM ukifauli inaweza kukupa uwanda mkubwa wakusoma course nzuri huko mbele za safari baada ya form six.

Asante sana.
Upana na urefu ama unataka upana tu
 
AI atachukua kazi zote kasoro za mikono.
Nenda veta
 
Ndugu wadau, nilitaja kujua combination ipi kati ya PCB na PCM ukifauli inaweza kukupa uwanda mkubwa wakusoma course nzuri huko mbele za safari baada ya form six.

Asante sana.
M;MATHEMATICS
HUKUU HAMNAAA SHOBO UKIPASUA UNAPASUA
 
Ndugu wadau, nilitaja kujua combination ipi kati ya PCB na PCM ukifauli inaweza kukupa uwanda mkubwa wakusoma course nzuri huko mbele za safari baada ya form six.

Asante sana.
pcm nenda usa utanishukuru kijana mpaka kizazi chako
 
B ;BIOLOGY
HAIUMIZI SANA KICHWA KAMA HAPO JUU JUHUDI ZAKOTU
 
Najiulaumu kusoma PCB japo niligonga one form six. Kumbe kazi za afya ndo zipo hivi za kupelekeshwa na viongozi wa CCM. Diwani wa darasa la saba ananipelesha mwenye Master's ya afya huu ujinga. Dogo komaa na PCM.
PCM inamanufaa Gani?kwanini unashauei PCM?
 
usa river iko Arusha!!
So ulimaanisha kijana aende USa river sec kusoma PCM au ? Sikukuelewa hapo mwazi uliposema kija a aends Usa atakuja kukushukuru.Asante kwa ufafanuzi
 
Ndugu wadau, nilitaja kujua combination ipi kati ya PCB na PCM ukifauli inaweza kukupa uwanda mkubwa wakusoma course nzuri huko mbele za safari baada ya form six.

Asante sana.
Dunia ya Leo, imebadirika sana, unaweza ukawa umesoma HGL, HGK,na ukaweza kuchukua kozi fupi za programming, artificial intelligence, software engineering nk, cha mwingi ujue lugha vzr,
Kuna mzee mmoja kitaa,yeye ni mwalimu, amefundisha kwa miaka mingi, lakini anaendesha kampuni ya ujenzi, kila kitu kinawezekana, Nilikuwa kwenye sherehe ya Uhuru ubalozi wa Qatar, nikakuta jamaa wanaseti sound system, lighting system, daaa hizo setting wanazofanya, richa ya Mimi kuwa mbobezi na mnyama kwenye umeme, waliniacha hoi kabisa
 
Najiulaumu kusoma PCB japo niligonga one form six. Kumbe kazi za afya ndo zipo hivi za kupelekeshwa na viongozi wa CCM. Diwani wa darasa la saba ananipelesha mwenye Master's ya afya huu ujinga. Dogo komaa na PCM.
Tatizo la PCM ni kwenye Ajira, huko ndo kunatakaa connection balaa.

Bora PCB, serikali inatoa ajira za Afya, ni juhudi za muhusika na cheti chake kukidhi vigezo na sifa hitajika.

Bora Aende PCB
 
Back
Top Bottom