TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kuhusu Mikopo

TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kuhusu Mikopo

Tangu bodi ya mikopo imeanza kutangaza awamu za wanaufaika wa mikopo Kwa elimu ya juu imekua ikitoa takwimu na kusema awamu ya kwanza wanaufaika wa mwaka wa 1 walkuwa 56,120 na awamu ya pili walikuwa 14,428 na kufanya jumula ya wanufaida wa mwaka wa kwanza kua 70,560 lakini katika uhalisia wanafunzi wa mwaka wa 1 bado weng hawajapita mikopo na bodi imekuwa ikijificha kwenye kichaka ya kuwa wanafunzi watembelee account zao za SIPA.

Kwanini bodi istoe majina kabsa yakiwa n namba ya form 4 na form 6 Kwa direct entry na AVN Kwa diploma Ili tuwe na uhakika na takwimu lasivo n uongo mana bado weng hawajapita mikopo hiyo na pia huenda Hela zinaibiwa sana hapa na ndo mana watu hawakupata mkopo akiingia kazini anakuta anakatwa tu mkopo na akifatilia anazungushwa wanafanya hvo kulipia fedha walizoiba.

TUNAOMBA WATOE IDADI KWA MAJINA NA SIO KUJIFICHA KWENYE KICHAKA CHA SIPA.
 
Naitwa Abdul-Aziz Carter Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM):
View attachment 2788445Octoba 20,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo (HESLB) Abdul-Razaq Badru aliishukuru serikali kwa kutenga Bilioni 731 kwa ajili mikopo ya wanafunzi 220,376 wa Elimu ya juu, lakini pia alitangaza awamu ya kwanza ya wanufaika wa mkopo (first batch) ambapo alisema Bilioni 159.7 zimetumika kuwanufaisha wanafunzi 56,132.

Taarifa hii inatia mashaka kwa sababu ukiangalia akaunti za wanafunzi (students individual permanent account) maarufu kama SIPA wanafunzi wengi wa mwaka wa 1 wamepata chini ya 20% .

Kiwango cha pesa kilichotengwa (Bilioni 159.7) hakiendani na 20% ambayo wanafunzi wengi wamepewa.

TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kwani ndio lengo la kuundwa kwake, Bodi ya mikopo inapaswa kutoa ufafanuzi kwa kuwa Kuna wanafunzi walikua na sifa na vigezo vilivyoainishwa na bodi ya mikopo,licha ya kuweka viambatanisho katika maombi yao bado wamepata chini ya 20% na mwisho serikali kupitia wizara ya Elimu wanapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini na kuitafutia suluhu changamoto hii.


=============

UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO: MKOPO UNATEGEMEA NA UHITAJI WA MUOMBAJI KWA ALIVYOOMBA

Mkuu wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), Omega Ngole anafafanua:

“Upangaji wa viwango vya mikopo kwa Wanafunzi wanufaika unatokana na uhitaji wa muombaji kulingana na nyaraka alizowasilisha HESLB wakati wa maombi yake, mfano muombaji akisema ana ulemavu, yatima, historia yake kimasomo n.k inaweza kuchangia kiwango anachotakiwa kukipata.

“Hali hiyo inafanya viwango vitofautiane, kuna makundi yanayopewa kipaumbele mfano yatima, wenye ulemavu au waliofanya vizuri zaidi katika mitihani n.k

"Hao wanaolalamika wanatakiwa kujua kiwango cha mkopo kinatokana na nyaraka zao wenyewe.

"Kiwango cha mkopo hakiwezi kulingana kwa kila Mwanafunzi na ndio maana kila mmoja anaingiziwa fedha kwenye akaunti yake binafsi, hilo ni suala la mtu mmoja mmoja kulingana na mahitaji na ndio maana wapo ambao wamepata mkopo kwa kiwango cha 100%."
Mkuu Yani Huku vyuoni Ni shida kabisa Imagine mpaka leo tarehe 1 watu hatujapata boom , hivi iyo Ela ya kumsaidia mwanafunz unampa wiki tatu baada ya kufungua chuo , bodi ya mikopo kila mwaka changamoto Ni ile ile kuweni na huruma na watto wa Masikini , wengine wameanza kujiuza kiss boom halijaingia wengine wanaingia mtaani kufanya kazi ili wapate Hata Ela ya kula kwa siku badala ya kuingia Class Yani ila Mungu yupo asee mtalipwa kwa mnayoyatenda .Inasikitisha Sana.
 
Mkuu Yani Huku vyuoni Ni shida kabisa Imagine mpaka leo tarehe 1 watu hatujapata boom , hivi iyo Ela ya kumsaidia mwanafunz unampa wiki tatu baada ya kufungua chuo , bodi ya mikopo kila mwaka changamoto Ni ile ile kuweni na huruma na watto wa Masikini , wengine wameanza kujiuza kiss boom halijaingia wengine wanaingia mtaani kufanya kazi ili wapate Hata Ela ya kula kwa siku badala ya kuingia Class Yani ila Mungu yupo asee mtalipwa kwa mnayoyatenda .Inasikitisha Sana.
Kuna tatizo kubwa la msingi namna serikali inavyoendesha elimu ya vyuo vikuu, wanajua shida ipo ila wanajifanya hamnazo. Ila ukisikia takwimu za ufisadi zinazotajwa na kina Mpina unabaki kuduwaa tu.
 
Back
Top Bottom