TAHLSO Jisahihisheni kazi yenu ni kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo

TAHLSO Jisahihisheni kazi yenu ni kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo

Katabaro_EJ

Member
Joined
Jul 6, 2013
Posts
16
Reaction score
11
Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati hapa Tanzania (TAHLSO) ilianzishwa ili iweze kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo.

Bahati mbaya kwa sasa TAHLSO siyo chombo tena cha kushughulika na masuala ya wanafunzi bali ni chombo cha kueneza propaganda za watawala.

Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la wanafunzi hasa wa kada ya afya ngazi ya cheti na diploma ambao wamekuwa waki-disco si kwa sababu ya kutokusoma ama kufundhishwa vizuri bali ni kutokana na mifumo mibovu iliyowekwa na Nactvet TZ ambayo TAHLSO haijaona kama ni tatizo!

Iko hivi kwa sasa wanafunzi wa diploma na certificate wa kada yya afya wako chini ya NACTVET ambapo mkufunzi anafundisha akiwa chini ya taasisi iliyomuajiri lakini mtihani wa mwisho wa mwaka inatungwa, kusimamiwa na kusahihishwa na hao NACTVET na kutoa matokeo. Sasa mtu hajafundisha amekaa zake huko anatunga mtihani kwa ajili ya kuwakomoa wanafunzi na kuwafanya wa-disco! Huu utaratibu siyo mzuri hata kidogo kwani unawachonganisha wanafunzi na wakufunzi wao, wakufunzi na waajiri wao, taasisi zinazotoa elimu na jamii!
Kwa masikitiko makubwa TAHLSO haijaliona hili iko busy kueneza propaganda!

Wakati mwingine nitakuja kuwaelezea NACTVET na mambo yao yaaiyofaa na njia bora ya kuratibu mafuzo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati!

Katabaro EJ
Morogoro
August 2025
 
Sasa km hiyo Taasisi husika inachagua kiongozi aliye disco chuo, unategemea nn?

Taasisi inaendeshwa na kilaza m1 anayeji mwambafy na venye hamna kitu. Kiliba nae kuwa prezoo? Kuishiwa kwa viongozi huku. Lol.
😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom