Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
TAIFA AMBALO WATU WAKE WANAJIVUNIA MAMBO YA KIJINGA KWA KISINGIZIO CHA KUPATA KIPATO NI TAIFA LA WAPUMBAVU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Nyerere Kwa maoni yake alisema taifa lina maadui watatu ambao ni Ujinga, umaskini na maradhi lakini adui ambaye alitaka Watu wapambane naye zaidi ni adui ujinga.
Kupambana na ujinga elimu ilihesabika kama silaha kuu.
Lakini mambo yamebadilika.
Ujinga sio adui tena.
Kuna mtu anaweza akawa mjinga lakini asiwe mshabiki wa Ujinga. Akawa anatamani siku moja ajue. Mtu huyu huwa anaupeo mkubwa wa akili(IQ) lakini hana elimu.
Kuna mtu ni mjinga alafu akawa shabiki lialia wa ujinga. Yaani anajivunia ujinga wake. Huyu upeo mdogo. Na huwa ni mpumbavu.
Kuna mtu anaweza kuwa na elimu lakini akawa mshabiki wa ujinga. Huyu upeo mdogo na ni mpumbavu.
Alafu kuna yule anaelimu na sio mshabiki wa ujinga. Huyu anaakili na hekima
Taifa letu adui anaweza asiwe ujinga tena isipokuwa akawa upumbavu.
Kwa sasa wapo Watu waliosoma na kupata kile kinachoitwa elimu lakini ukifuatilia ni wapumbavu.
Ili uwe mpumbavu lazima uwe na upeo mdogo wa kufikiri.
Mpumbavu ni mtu mwenye uwezo mdogo wa akili.
Yaani mtu anaweza akawa na elimu kubwa lakini upeo Mdogo.
Ni mpumbavu pekee ambaye anaweza kufanya mambo ya kijinga kwa visingizio anavyoona kwake ni hoja. Kama nafanya hivi ili nipate kipato kwamba huna akili ya kufanya mambo ya heshima na akili ili upate kipato mpaka kujidhalilisha na kudhalilisha Watu wengine?,
Upumbavu unadhalilisha haswa.
Ujinga unaweza ukaaibika lakini Watu watagundua kuwa wewe ulikuwa hujui.
Ujinga ni kama ushamba. Mfano ulikuwa hujui kuwa alama fulani ukiona kwenye nguo inakutambulisha Kama shoga. Utaaibika lakini akitokea mtu akakueleza ukaacha haiwi tena aibu bali ilikuwa sehemu ya kujifunza, Elimu.
Lakini kama utajua alafu kwa makusudi ukaendelea hiyo ndio inaitwa upumbavu ambao utakudhalilisha.
Ni upumbavu kwa mwanaume kujidhalilisha mbele za Watu na kujiita au kuitwa chawa.
Mwanaume mwenye akili anayejua thamani yake ndani ya jamii hawezi kufanya jambo hilo. Hata kwa kisingizio chochote.
Ni upumbavu na kujidhalilisha kwa kijana kujisifia umario, kulelewa ni dalili ya kuwa kijana huyo hajitambui. Ni tangazo kuwa wewe ni mvivu. Uvivu unadhalilisha.
Ni upumbavu kwa mwanaume kujisifia kufanya zinaa na wanawake hovyohovyo. Ni dalili kuwa wewe ni mchafu usiye na kinyaa. Lakini pia ni tangazo kuwa wewe ni mharibifu wa miili na hisia za wengine.
Ni upumbavu na kujidhalilisha kwa mwanamke kutaka kuhudumiwa badala naye atafute kazi.
Kwenye zama za giza za ujinga ilikuwa ni mila potofu kuwa mwanamke ni chombo cha starehe hatakiwi kufanya kazi. Ulikuwa ujinga.
Lakini zama hizi elimu imetupa nuru kuwa wanawake nanyi sharti mfanye kazi.
Ni wapumbavu na wanaopenda kujidhalilisha wanaotaka kuendelea kutaka kuhudumiwa na hawataki kufanya kazi za kuzalisha.
Ni upumbavu na kujidhalilisha kwa kuona kuna jamii iliyopendelewa labda kiakili au kimaumbile. Huo ulikuwa ukosefu wa ujinga. Binadamu ni sawa ila hatulingani.
Hakuna jamii bora kuliko jamii nyingine.
Wale unaowaona mchana ndio haohao wanaolala usiku. Na kinyume chake.
Wewe kuzaliwa kabila fulani labda ni dogo au sio maarufu hiyo usichukulie kuwa jamii yenu ni duni. Yaliyopo kwenye zile jamii ambazo mtazamo wako uliona ni bora ndio haohao waliopo kwenye jamii yenu.
Ishu kubwa hapo ni uchaguzi wa mfumo.
Wapo walioamua kuchagua upumbavu.
Na wapo walioamua kuchagua Akili na hekima.
Taikon acha nipumzike sasa.
Nawatakia Sabato Njema.
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam