Taifa au CCM- Kadi au Katiba?

Taifa au CCM- Kadi au Katiba?

eti nasikia Mzee Sitta ilimlazimu kuomba msamaha vinginevyo waliitisha kadi yake ya CCM kwa lengo la kumvua Ubunge na Uspika. Sasa najiuliza kwanini Sitta hakukataa kuomba msamaha? kwanini Sitta hakukubali kunyang'anywa kadi ya CCM na awe amestaafu siasa kwa heshima? lol! nafasi moja ya ukombozi imepotea hapa.

Hata hivyo nafasi bado ipo, nakushauri Mzee Sitta jiondoe sasa CCM, sababu unayo, utakuwa umesaidia sana ktk vita vya ukombozi wa Taifa kutoka mikononi mwa mafisadi.
 
Nadhani suala hili lime-expose CCM kwa umma. Inaumiza kichwa kuona watu mbalimbali na wengine ni wanabodi wenzetu , wakitaka kugombea ubunge kupitia CCM . Inaonyesha ni jinsi gani watu tusivyo na values when it comes to power .Let the truth be told, CCM is not there to defend neither the public's interest nor the united republic constitution. These are bunch of crooks that are using politics as a decoy in exploiting others especially the less fortunate ones. Despite of many evil things that CCM has done to Tanzanians, its reputation has not been affected at all! It has won two parliamentary elections; furthermore, many people are flocking to it. These series of events clearly indicate that there is something profoundly wrong with Watanzania.
 
Yaani CCM haifai hata kidogo, na style walioanza nayo ya kuwanunua wapinzani, jamani tunakoelekea ni kubaya
Itafika wakati tutaingia vitani hatuwezi kundelea kunyonywa...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Habari ambazo zimekuwa zikitiririka kwa muda wa masaa kadhaa yaliyopita zinatuthibitishia kuwa waoga wanaongoza CCM sasa hivi. Habari za kuwa Spika wa Bunge la Muungano alipewa kibano katika mojawapo ya vikao vya juu vya CCM ni habari za kuudhi, kukera, na kuchekesha; yote kwa kwa wakati mmoja. Vile vile tukio la kujadili mambo ya Bungeni na taratibu za Bungeni kuonesha kutoridhishwa kwa mwenendo wa Bunge kwenye vikao vya chama ni tukio la kulaaniwa na kukataliwa na kila mpenda demokrasia.

Kwa vile CCM wamelewa ugimbi wa madaraka inaonekana hawajui kuwa Bunge siyo tawi la CCM wala Jumuiya ya chama. Spika wa Jamhuri ya Muungano siyo Spika wa Bunge la CCM. Bunge la namna hiyo halipo.

Bunge linaendeshwa kwa taratibu zake na wakati wowote mbunge yoyote hafurahishwi au kuridhishwa na mwenendo wa Bunge taratibu zipo za kutoa malalamiko yake na kama ni kundi kubwa la wabunge basi wana nafasi ya kujadili na hata kumuondoa Spika kwa taratibu za Kibunge (Impeachment).

Lakini CCM imejinyanyua juu na kujiweka kwenye kiti cha enzi ambapo kitu kinachoitwa Katiba hakiangaliwi tena isipokuwa kadi na sheria zilizotungwa na Bunge lenyewe haziangaliwi tena bali taratibu za chama. Imefika mahali watu wanapewa uchaguzi wa "Chama" au "Taifa".

Mjadala wa viongozi hao wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao na "vigogo" wengine wa chama hao kuhusu mwenendo wa Bunge au maamuzi ya "Spika" ni mjadala potofu, usio na msingi na kwa hakika ni wa kiwoga!

Kama kuna kundi la wabunge wa CCM ambao wanaamini kuwa Spika hawatendei haki na wao ndio wako wengi Bungeni kwanini wasilete malalamishi yao ndani ya Bunge na badala yake kutumia mbinu za kiviziaji nje ya Bunge? Kama kuna watu ambao wanaona Spika anawapendelea watu wengine kwanini watu hao wasifuate taratibu za Bunge kutoa malalamiko yao?

Hawawezi. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa kuwa Bunge ni mhimili mwingine wa dola na Spika ni Mkuu wa Mhimili huo. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa hawaungwi mkono ndani ya Bunge; Hawawezi kwa sababu wanajua wakizungumza Bungeni Taifa zima litajua nani kazungumza nini na ana hoja gani! Wanaogopa; wanawaogopa Watanzania! Wanaogopa kujulikana!

Ni waoga.

Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.

Wao wametumia vikao vya chama, Sitta anawasubiri tena Bungeni. Bunge haliongozwi na Katiba ya CCM au maoni ya wana CCM peke yake. Hivyo, badala ya kuwapa njia rahisi ya kutokea (kumvua uanachama - kitu ambacho nina uhakika hawawezi pamoja na mikwara yao yote!) Sitta ameamua kuwapa ushindi wa pambano moja.

Ndugu zangu mafisadi wanaweza kushinda kwa sababu nyingi lakini kubwa ni kwa sababu Watanzania tumewaachia hivyo. Kuna watu ambao wanatumia hoja ya kuwa "Sitta naye si safi" hoja hii haina msingi! Uchafu wa mtu haumfanyi ashindwe kuona usafi au kuutetea usafi! Mtu mchafu ambaye hataki kusafishika au kufuata usafi wala kuupigia usafi debe ni mchafu per exellence!

Tanzania haiitaji watu wakamilifu (kwani hawapo duniani); Tanzania haiitaji watu watakatifu (wako mbinguni); Tanzania haiitaji watu wasiokosea (hawapatikani); Tanzania inahitaji watu ambao wanajua mapungufu yao, wamesahihisha makosa yao na wanakubali kusahihishwa. Watu ambao wanatukuza uadilifu na wanautafuta sana. Tanzania inahitaji viongozi ambao wanatambua wito wao kuwa ni mkubwa zaidi kuliko makosa au udhaifu wao, watu ambao wako tayari kusahihissha walikokaribu siyo wanaoendelea kunyosha vidole kuwa "fulani naye si safi"!

Ninaamini kwa moyo wangu wote, hakuna kiongozi wa Tanzania sasa hivi ambaye amesimamia wito huu wakuliinua taifa zaidi kama Spika Sitta. Leo hii anasimama kama ngao peke kati ya mafisadi kuliteka Bunge letu na wananchi kulimiliki. Spika Sitta aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya amelipa Bunge letu kile ambacho kwa miaka mingi tumekuwa tukikilalamikia; meno.

Kuna viongozi watatu wa dola yetu; Rais (Utendaji), Jaji Mkuu (mahakama) na Spika (Utungaji wa Sheria na Usimamizi wa serikali). Mhimili hii mitatu katika nchi ya demokrasia haiwezi kuwa pamoja wakati wote. Urais, Mahakama, na Bunge vikikubaliana kwa kila kitu na wakati wote basi tujue kuwa tunaishi kwenye nchi ya Udikteta! Havipaswi kukubaliana kila kitu na wakati wote; ni lazima vigongane.

Hivyo sasa tunashuhudia kugongana kati ya Urais na Bunge na huko tunakokwenda tutashuhudia kugongana kati ya Urais na Mahakama au Mahakama na Bunge. Hii ni sehemu ya demokrasia.

Ni kwa sababu hiyo tunapoona kikundi cha wahuni wachache (namaanisha neno "wahuni" katika kila maana yake mbaya) kujaribu kuliteka Bunge letu na kulijadili pembeni na kutaka lifanye mambo kwa manufaa ya kikundi cha watu hao wachache kwa jina la "chama" ni lazima tuwapinge.

Tunawapinga kwa sababu siyo kazi yao (ni wabunge Bungeni); tunawapinga kwa sababu Bunge si la kwao (ni Bunge la Watanzania); tunawapinga kwa sababu wamefanya kwa woga (wangetaka kuwa majasiri wangesimama Bungeni mbele ya huyo Spika).

Nawataadharisha CCM, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vyao; Msiliteke Bunge wala kusababisha Bunge lisimame peke yake au Spika afanye mambo yamewahi kutokea sehemu nyingine ambako kumekuwepo na mvutano kati ya Bunge na Urais. Ninawahakikishia kuwa mkiendelea kulishambulia Bunge letu namna hii (kama walivyofanya wengine mwaka jana) tutawapinga kwa nguvu zaidi kwani sasa hivi ni Bunge tu linasimama kati yetu na mafisadi waliiokubuhu wanaoshirikiana na mafisadi wa kizungu (wanaitwa wawekezaji) kutugeuza vijakazi wa milele.

Kama mnafikiri mambo hayaendi vizuri, na mnafikiri mna hoja, Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.

CCM mmeruhusu utajiri wetu utweke nyara na mafisadi na sasa mnataka kuteka na Bunge letu? Nyinyi mmechagua CCM ishikeni na ikumbatieni; nyinyi mmechagua kadi za chama chenu zibebeni na mlale nazo; tuachieni Taifa letu; iacheni Katiba yetu!

Mshindwe!

niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Makala hii inaweza kutumika na gazeti lolote lile bila ya kubadilisha mtunzi.

M.M.

Kweli Kabisa unayoyasema,lakini kundi hilo hilo la mashujaa,likiongozwa na Sitta,Linaimba kila siku kuwa kuna pesa zimetumwa na mafisadi majimboni mwao ili kuwaondoa.

Swali, je Yeye Sita,akiwa kama mwana sheria na kiongozi wa bunge,ni kwanini asilifanyie kazi hilo jambo?.Badala ya kuendelea kuwapigia wananchi kelele kila mara?

Sitta na wenzeke wamekuwa wakilitumia sana neno ufisadi kama tiketi ya kuwarudisha kwenye ubunge 2010,bila kusema au kumfikisha mtu PCCB.

Wananchi tunakosa imani kabisa na sitta na kundi lake.Kama anaushahidi na kundi lake,basi angeiambia NEC kuhusu hayo mambo kuliko kugawa watu kwa kutumia neno ufisadi.
 
wengine tulilaani sana kitendo cha ccm kutoheshimu katiba yake (rejea zengwe la jk kuwa mgombea pekee) tukainisha kwamba iwapo ccm inashindwa kuheshimu katiba yake jee itaweza heshimu katiba ya nchi? wapo waliodai hayo ni mambo ccm na tuiache ccm ijiamulie mambo yake yenyewe.

sitashangaa na hili tukiambiwa hayo ni masuala ya ccm na tusiingilie na kama tunauwezo tukaliseme bungeni huku wakijua huko bungeni ccm ni wengi na wataizima hoja.

hivi kunauwezekano wa wananchi kutangaza mgogoro wa kikatiba na kulipeleka suala hili mahakamani (japokuwa huko nako mmh)?
 
eti nasikia Mzee Sitta ilimlazimu kuomba msamaha vinginevyo waliitisha kadi yake ya CCM kwa lengo la kumvua Ubunge na Uspika. Sasa najiuliza kwanini Sitta hakukataa kuomba msamaha? kwanini Sitta hakukubali kunyang'anywa kadi ya CCM na awe amestaafu siasa kwa heshima? lol! nafasi moja ya ukombozi imepotea hapa.

Hata hivyo nafasi bado ipo, nakushauri Mzee Sitta jiondoe sasa CCM, sababu unayo, utakuwa umesaidia sana ktk vita vya ukombozi wa Taifa kutoka mikononi mwa mafisadi.
.

Hana uwezo wa kujiondoa kutokana na kuwa sitta baado anatamaa na madaraka.

Ukumbuki wale wenzie wote walikaa kimya mwenzio alipokuwa akikaangwa
 
Hivi bado Watanzania wataipigia tena CCM KURAAAAAAAAAAAAAAA? Jamni tuamke tuachane na huu u CCM utatufikisha pabaya.
 
Tanzania haiitaji watu wakamilifu (kwani hawapo duniani); Tanzania haiitaji watu watakatifu (wako mbinguni); Tanzania haiitaji watu wasiokosea (hawapatikani); Tanzania inahitaji watu ambao wanajua mapungufu yao, wamesahihisha makosa yao na wanakubali kusahihishwa. Watu ambao wanatukuza uadilifu na wanautafuta sana. Tanzania inahitaji viongozi ambao wanatambua wito wao kuwa ni mkubwa zaidi kuliko makosa au udhaifu wao, watu ambao wako tayari kusahihissha walikokaribu siyo wanaoendelea kunyosha vidole kuwa "fulani naye si safi"!
mm
hapa umesema sana
thanks
 
Asante Mwanakijiji kwa kuleta tena hoja ambayo ni muhimu sana. Nawashangaa chama tawala kwa kujaribu kulizima bunge. Ukweli ni kuwa mambo yamebadilika na hili ni suala ambalo hawana namna ya kulizuia. Kama wanataka kumdhibiti Spika wakifikiri mambo yatakuwa yameisha, wanajidanganya. Imefika sehemu sasa inabidi wabadilike, vinginevyo ufalme utany'ang'anywa na kupewa watu watu wengine.
Mwanakijiji, mwendo mdundo. Kazi nzuri na ya kweli haipotei bure. Historia itatuhukumu kama tukisahau hilo
 
sita_kinana.JPG

Sitta na Kinana
Spika wa Bunge la Jmahuri la Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samwel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha mapinduzi(CCM)Abdulahman Kinana kwenye mkutano mkuu wa Halmashauri hiyo Mjini Dodoma.Picha na Mdau Jube Tranquilino
kwa hisani ya Hakingowi blog.

Huyo Kinana anamwambia nini Spika !

tuachieni Taifa letu; iacheni Katiba yetu!

Hapana Mwanakijiji, taifa ni letu sawa lakini katiba ni yao - sana sana sisi ni mateka wao kupitia katiba hiyo na Bunge, mhimili muhimu wa dola limeridhia hali hiyo. Hebu fikiria:-

  • Katiba inayotoa ruhusa kwa kikundi cha wahuni kufanya kikao cha siri na kuonyesha dharau ya wazi kwa bunge kwa jina la CCM.
  • Katiba inayolipa jeuri genge la mafisadi kutapanya rasilimali za taifa bila woga wowote wa kuwawajibishwa kwa jina la CCM.
  • Katiba inayokipa madaraka chama kimoja cha siasa kuwa mchezaji na mwamuzi katika uchaguzi unaohusisha vyama vingi.
  • Katiba inayomnyima ruhsa mpiga kura kumwajibisha mbunge mlafi anayeamua kutetea maslahi binafsi ya CCM kuliko ya taifa.
  • Katiba inayompa kiongozi wa nchi na serikali madaraka makubwa na hapo hapo kumpa kinga hata pale anapoyatumia vibaya.
  • Katiba inayoruhusu utawala usiojali haki na usawa na kuwatukuza wavunjaji wa sheria bila kuwachukulia hatua madhubuti.
  • Katiba inayomnyima fursa mwananchi kuchaguliwa ama kupigiwa kura eti kwa sababu si mwanachama wa chama kilichosajiliwa.
Mwanakijiji kwa bahati mbaya Mh. Sitta kama Spika wa Bunge, ameruhusu kwa kiasi fulani hali kama hiyo kustawi ndani na nje ya Bunge. Bunge kwa nyakati tofauti limetumiwa kama taulo ya kuisetiri serikali inapovuliwa nguo na kubaki uchi.

Bunge pamoja na kutunga sheria, ndicho chombo kinachoisimamia serikali katika utendaji na utekelezaji - hivyo hapa tulipo tumefika kwa sababu Bunge halikutimiza wajibu wake na hasa katika kulinda bila kurekebisha mapungufu ya katiba.

Ombi kwa Spika, wengine tutakuwa tayari kukusamehe kama utakuwa tayari kujifunza kutokana na maamuzi ya hili genge la wahuni na kusimamia unachokiamini. Kama kuna wakati taifa limehitaji watu wa kulipigania na kulitetea, wakati huo ni sasa.
Kwa pamoja tujipange tuliokoe taifa
Mikononi mwa hili genge la wahuni
Wakati ni sasa.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Habari ambazo zimekuwa zikitiririka kwa muda wa masaa kadhaa yaliyopita zinatuthibitishia kuwa waoga wanaongoza CCM sasa hivi. Habari za kuwa Spika wa Bunge la Muungano alipewa kibano katika mojawapo ya vikao vya juu vya CCM ni habari za kuudhi, kukera, na kuchekesha; yote kwa kwa wakati mmoja. Vile vile tukio la kujadili mambo ya Bungeni na taratibu za Bungeni kuonesha kutoridhishwa kwa mwenendo wa Bunge kwenye vikao vya chama ni tukio la kulaaniwa na kukataliwa na kila mpenda demokrasia.

Kwa vile CCM wamelewa ugimbi wa madaraka inaonekana hawajui kuwa Bunge siyo tawi la CCM wala Jumuiya ya chama. Spika wa Jamhuri ya Muungano siyo Spika wa Bunge la CCM. Bunge la namna hiyo halipo.

Bunge linaendeshwa kwa taratibu zake na wakati wowote mbunge yoyote hafurahishwi au kuridhishwa na mwenendo wa Bunge taratibu zipo za kutoa malalamiko yake na kama ni kundi kubwa la wabunge basi wana nafasi ya kujadili na hata kumuondoa Spika kwa taratibu za Kibunge (Impeachment).

Lakini CCM imejinyanyua juu na kujiweka kwenye kiti cha enzi ambapo kitu kinachoitwa Katiba hakiangaliwi tena isipokuwa kadi na sheria zilizotungwa na Bunge lenyewe haziangaliwi tena bali taratibu za chama. Imefika mahali watu wanapewa uchaguzi wa "Chama" au "Taifa".

Mjadala wa viongozi hao wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao na "vigogo" wengine wa chama hao kuhusu mwenendo wa Bunge au maamuzi ya "Spika" ni mjadala potofu, usio na msingi na kwa hakika ni wa kiwoga!

Kama kuna kundi la wabunge wa CCM ambao wanaamini kuwa Spika hawatendei haki na wao ndio wako wengi Bungeni kwanini wasilete malalamishi yao ndani ya Bunge na badala yake kutumia mbinu za kiviziaji nje ya Bunge? Kama kuna watu ambao wanaona Spika anawapendelea watu wengine kwanini watu hao wasifuate taratibu za Bunge kutoa malalamiko yao?

Hawawezi. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa kuwa Bunge ni mhimili mwingine wa dola na Spika ni Mkuu wa Mhimili huo. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa hawaungwi mkono ndani ya Bunge; Hawawezi kwa sababu wanajua wakizungumza Bungeni Taifa zima litajua nani kazungumza nini na ana hoja gani! Wanaogopa; wanawaogopa Watanzania! Wanaogopa kujulikana!

Ni waoga.

Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.

Wao wametumia vikao vya chama, Sitta anawasubiri tena Bungeni. Bunge haliongozwi na Katiba ya CCM au maoni ya wana CCM peke yake. Hivyo, badala ya kuwapa njia rahisi ya kutokea (kumvua uanachama - kitu ambacho nina uhakika hawawezi pamoja na mikwara yao yote!) Sitta ameamua kuwapa ushindi wa pambano moja.

Ndugu zangu mafisadi wanaweza kushinda kwa sababu nyingi lakini kubwa ni kwa sababu Watanzania tumewaachia hivyo. Kuna watu ambao wanatumia hoja ya kuwa "Sitta naye si safi" hoja hii haina msingi! Uchafu wa mtu haumfanyi ashindwe kuona usafi au kuutetea usafi! Mtu mchafu ambaye hataki kusafishika au kufuata usafi wala kuupigia usafi debe ni mchafu per exellence!

Tanzania haiitaji watu wakamilifu (kwani hawapo duniani); Tanzania haiitaji watu watakatifu (wako mbinguni); Tanzania haiitaji watu wasiokosea (hawapatikani); Tanzania inahitaji watu ambao wanajua mapungufu yao, wamesahihisha makosa yao na wanakubali kusahihishwa. Watu ambao wanatukuza uadilifu na wanautafuta sana. Tanzania inahitaji viongozi ambao wanatambua wito wao kuwa ni mkubwa zaidi kuliko makosa au udhaifu wao, watu ambao wako tayari kusahihissha walikokaribu siyo wanaoendelea kunyosha vidole kuwa "fulani naye si safi"!

Ninaamini kwa moyo wangu wote, hakuna kiongozi wa Tanzania sasa hivi ambaye amesimamia wito huu wakuliinua taifa zaidi kama Spika Sitta. Leo hii anasimama kama ngao peke kati ya mafisadi kuliteka Bunge letu na wananchi kulimiliki. Spika Sitta aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya amelipa Bunge letu kile ambacho kwa miaka mingi tumekuwa tukikilalamikia; meno.

Kuna viongozi watatu wa dola yetu; Rais (Utendaji), Jaji Mkuu (mahakama) na Spika (Utungaji wa Sheria na Usimamizi wa serikali). Mhimili hii mitatu katika nchi ya demokrasia haiwezi kuwa pamoja wakati wote. Urais, Mahakama, na Bunge vikikubaliana kwa kila kitu na wakati wote basi tujue kuwa tunaishi kwenye nchi ya Udikteta! Havipaswi kukubaliana kila kitu na wakati wote; ni lazima vigongane.

Hivyo sasa tunashuhudia kugongana kati ya Urais na Bunge na huko tunakokwenda tutashuhudia kugongana kati ya Urais na Mahakama au Mahakama na Bunge. Hii ni sehemu ya demokrasia.

Ni kwa sababu hiyo tunapoona kikundi cha wahuni wachache (namaanisha neno "wahuni" katika kila maana yake mbaya) kujaribu kuliteka Bunge letu na kulijadili pembeni na kutaka lifanye mambo kwa manufaa ya kikundi cha watu hao wachache kwa jina la "chama" ni lazima tuwapinge.

Tunawapinga kwa sababu siyo kazi yao (ni wabunge Bungeni); tunawapinga kwa sababu Bunge si la kwao (ni Bunge la Watanzania); tunawapinga kwa sababu wamefanya kwa woga (wangetaka kuwa majasiri wangesimama Bungeni mbele ya huyo Spika).

Nawataadharisha CCM, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vyao; Msiliteke Bunge wala kusababisha Bunge lisimame peke yake au Spika afanye mambo yamewahi kutokea sehemu nyingine ambako kumekuwepo na mvutano kati ya Bunge na Urais. Ninawahakikishia kuwa mkiendelea kulishambulia Bunge letu namna hii (kama walivyofanya wengine mwaka jana) tutawapinga kwa nguvu zaidi kwani sasa hivi ni Bunge tu linasimama kati yetu na mafisadi waliiokubuhu wanaoshirikiana na mafisadi wa kizungu (wanaitwa wawekezaji) kutugeuza vijakazi wa milele.

Kama mnafikiri mambo hayaendi vizuri, na mnafikiri mna hoja, Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.

CCM mmeruhusu utajiri wetu utweke nyara na mafisadi na sasa mnataka kuteka na Bunge letu? Nyinyi mmechagua CCM ishikeni na ikumbatieni; nyinyi mmechagua kadi za chama chenu zibebeni na mlale nazo; tuachieni Taifa letu; iacheni Katiba yetu!

Mshindwe!

niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Makala hii inaweza kutumika na gazeti lolote lile bila ya kubadilisha mtunzi.
uiweke kwenye cheche hii makala mkuu!kuna watu nimewazoesha vibaya kila ijumaa,wakiiona na hii WATAELEWA KINACHO!...............

bravo bro!.....good job
 
Msubiri makofi, vifijo na vigelegele, kwa mzee Sitta atakapo ingia bungeni..
Nina imani kabisa kwamba hili lilikuwa kokoro la JK na kawazoa wengi sana...Sitta amekamilisha kazi yake hawezi kujiuzuru kwani ni ushindi kwa Mafisadi na itachukua miaka mitano mingine kurekebisha. Hata makachero wanapocheza double Agent hujifanya wanyonge na wakuaminika ili wapate kile walichokihitaji na ndivyo mchezo ulivyochezwa..
Wakati ndio huu subirini mtakuja sema Mkandara kaona mbali!
 
Mkandara vitu unavyoongea ni vikubwa sana kwa JK kufikiria. Mimi sidhani kama JK alikuwa ameset up mtego wowote ule, jamaa is so weak na ndio maana siku zote anashindwa kutoa misimamo yakinifu kwenye ishu nyingi zinazohusu taifa.
 
M.M,

Heshima mbele, well said and said it all. Swali, je wanamasikio yanayosikia na kama yanasikia, je wana political will ya kuyafanyia kazi haya?

wayatoe wapi, wameziba pamba, lugha inayopendwa ni ile inayoendana na ufisadi tu, zaidi ya hapo hawasikii kingine.
 
Chama hiki kinaomba wananchi kushirikiana nacho kumaliza mafisadi, lakini pale unapowapa huo ushirikiano basi wewe ndiyo unakuwa mbaya. Mimi kwa mawazo yangu nilifikiri SISIEMU ilitakiwa kumpa pongezi Sitta kwa utendaji wake wa kazi, lakini walitaka kumnyang'anya kadi kwa kutoridhika na kazi yake. May be he needs to do more that what he's been doing.

Sasa chama kinapodai kuwa kinapambana kusafisha fisadiz ndani yake halafu wakamkalia shingoni Sitta kwa kuruhusu kuibua ufisadi bungeni..... napata kiarabuarabu.
 
Vast majority of Tanzanians know JK is FISADI, kwenye hiki kikao JK alitakiwa alambe dume kwa kum-support Sitta na ku-go after fisadiz. Lakini sasa ndo kaonyesha rangi zake zote kwenye paji lake la uso. Masikini wa Mungu..........Mithali 10:1-kuendelea (Nukuu: Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye bali mwana m......... ni mzigo wa mamaye. Hazina ya uovu haisaidii kitu bali haki huondoa mauti......."), endelea kusoma kwenye biblia.

Wengi wa viongozi wa SISIEMU wanajali chama chao kama mama yao kuliko kutetea haki ya TAIFA zima. Hii inamaanisha kuwa attitude yao hiyo ni mzigo kwa chama chao,......wait and see.
 
Indume Yene,
Mkuu JK hakuwa na haja ya kuchukua upande.. yeye ni mwenyekiti wa chama ktk kikao hicho hivyo mamlaka yake yanakwenda kama mwenyekiti na sii rais. Kama mwenyekiti anasikiliza hoja zai za watu na kuna baraza la wazee kina hao kina Mwinyi na Kinana ambao hawapo ktk madaraka Ikulu.

Na itakuwa ujinga mkubwa kwa JK kuwashambulia Mafisadi moja kwa moja ndani ya kikao hicho wakati ni wao Mafisadi walioleta hoja.. Hakuwaunga mkono wala kuwapinga, alikaa kati kusikia filimbi zao namwisho wa yote kaondoka na picha kamili..

Yatakayo fuata tusubiri, kama nilivyokwisha sema JK anasubiri wakati muafaka kuangusha scandal la Ufisadi. Kama angekwisha wakamata Mafisadi toka mwaka jana leo hii Wadanganyika tungekwisha sahau na bila shaka ingekuwa kazi ngumu na mpya kuunda mkakati mpya kuviangusha vyama vya Upinzani..

Just imagine this, Kabla ya uchaguzi Oct au Nov 2010 tunaambiwa Uchunguzi wa Mafisadi umekamilika na watajwa wamekamatwa na kufikishwa ktk vyombo vya sheria! Hizo pongezi sii tu zitafika mikoani na Afrika nzima bila shaka hata Washngton wataipata na pengine JK atachukua miaka mingine ya uongozi Tanzania na nchi za Kiafrika..Ya Lowassa na mawaziri wake tu yalimpa Ukuu na sifa za taji na kuwa mwenyekiti wa AU...kwa kitu gani ambacho wewe unaweza kusema kweli JK alistahili nafasi ile. Yote hii ni mikakati ya Utawala...mchezo wa mzee Bush!
Ndugu yangu huko nje, JK ana jina kubwa tofauti na jinsi mnavyomtazama au kumjua toka ndani kwani huko nje hawajui kinachoendelea nchini..
 
Katiba wanatunga wenyewe afu wanashindwa kuifuata.

Tatizo ninaloliona mimi juu ya hawa viongozi wa CCm, hasa hawa wenye viti wa mikoa na wajumbe wengine wa NEC ni kwamba hawajaelimika!! Wengi wao wanategemea fadhira ya CCM for their livelihood; kwahiyo si rahisi kwao kuwa critical juu ya uoza wa chama chao. Mfano mdogo tu ina order to substantiate my point, take the example of the Shinyanga CCM chairman, huyu bwana ni con man ameiba hela za kuanzisha bank ya wananchi kule Kahama na ili afunike madhambi yake na alindwe anatumiwa kwenda kuwasemea mafisadi kwenye vikao vya chama for a "FEE",huo kama sio umamluki ni kitu gani? Mwenyekiti huyu wa CCM Shinyanga has no other means of livelihood except kukaa na kupika majungu kwenye ofisi za CCM; what kind of leadership can one expect from such people who use CCM as their bread winner? The same thing applies to many CCM Chairmen, in actual fact some are known hard core criminals who use the party as their cover.Do you expect such people to understand the constitution and uphold it?
 
Yaani katika mambo yote ambayo wengine tunapigia kelele wao wanalilia hawapati nafasi ya kuzungumza Bungeni na kuwa Spika anawapendelea watu fulani fulani!?
 
Back
Top Bottom