Taifa halina vipaumbele, linaendeshwa kama biashara ya daladala

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,687
Reaction score
1,111
Ukweli utabaki hivyo,tuna tatizo kubwa kwenye vipaumbele vya taifa,hatujui nini tunataka na wakati gani tunahitaji hicho tunachokitaka.

Madhara yake ni nchi kuendesha kama biashara ya daladala, kondakta ana nguvu kuliko dereva kwa kuwa tu ndiye mshika fedha.

Kipau mbele cha serikali hakikidhi bajeti angalau kwa 10%. Bajeti yenyewe ya serikali mpaka ina maliza mwaka haifiki 60%,lakini watu wanakaa mjengoni wanabariki ukanjanja huu na business as usual.

Commitment ya kuitumikia nchi hii ni fumbo la imani ndo maana kufika Canaan itatugaharimu muda sana kwa kuwa suala hili ni mindset. Database yake imejaa ubinafsi na upigaji wa kiwango cha juu sana.
 
Kipindi cha JPM ndo ilikua lakini kwasasa hapana mama apewe pongezi kubwa.
 
Ukiniambia mama anakopa sana nitakuelewa ila kinacho endelea ni pombe ile ile kwenye muonekano wa chupa tofauti
 
Ndani ya siku chache zijazo Chato itatambuliwa kama mkoa, ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi iliyokuwa imemsimamishwa huko.

Hii sio ramli.
 
Kipindi cha JPM ndo ilikua lakini kwasasa hapana mama apewe pongezi kubwa.

Vipaombele havikuwepo before jpm hata halipokuja. Kila kiongozi alika anakuja na lake, na litajirudia mpaka mfumo utakapo badilika
 
Ukweli utabaki hivyo,tuna tatizo kubwa kwenye vipaumbele vya taifa,hatujui nini tunataka na wakati gani tunahitaji hicho tunachokitaka.

Madhara yake ni nchi kuendesha kama biashara ya daladala, kondakta ana nguvu kuliko dereva kwa kuwa tu ndiye mshika fedha.

Kipau mbele cha serikali hakikidhi bajeti angalau kwa 10%. Bajeti yenyewe ya serikali mpaka ina maliza mwaka haifiki 60%,lakini watu wanakaa mjengoni wanabariki ukanjanja huu na business as usual.

Commitment ya kuitumikia nchi hii ni fumbo la imani ndo maana kufika Canaan itatugaharimu muda sana kwa kuwa suala hili ni mindset. Database yake imejaa ubinafsi na upigaji wa kiwango cha juu sana.
Sijui kwenye mada kama hii mtu utaanzia wapi kuchangia, maana iko kila mahala, ni kama haina lengo maalum linalotakiwa kuchambuliwa!

Serikali nayo ikiendeshwa kwa mtindo huu huu, ndiyo hivyo tena, matokeo yake hayatofautiani na mada inayowasilishwa.

Samahani, mkuu 'sammosses' imenibidi nichangie hivi, pamoja na kukisia kwangu kuhusu lengo la mada yako, ambalo kwa kweli naungana nawe juu yake.
 
Ukweli utabaki hivyo,tuna tatizo kubwa kwenye vipaumbele vya taifa,hatujui nini tunataka na wakati gani tunahitaji hicho tunachokitaka.

Madhara yake ni nchi kuendesha kama biashara ya daladala, kondakta ana nguvu kuliko dereva kwa kuwa tu ndiye mshika fedha.

Kipau mbele cha serikali hakikidhi bajeti angalau kwa 10%. Bajeti yenyewe ya serikali mpaka ina maliza mwaka haifiki 60%,lakini watu wanakaa mjengoni wanabariki ukanjanja huu na business as usual.

Commitment ya kuitumikia nchi hii ni fumbo la imani ndo maana kufika Canaan itatugaharimu muda sana kwa kuwa suala hili ni mindset. Database yake imejaa ubinafsi na upigaji wa kiwango cha juu sana.
Naunga mkono hoja ✔️. Ukifuatilia kwa haraka kila Rais anakuja na lake kichwan kiasi kwamba ilan kwake sio lazima!! Hatuwez fika popote kwa mtindo huu, Kama Taifa ni lazima tuwe na mpango mkakati wa maendeleo wa miaka 30 kila atakae kalia kiti cha urais afuate hilo.
 
Kipindi cha JPM ndo ilikua lakini kwasasa hapana mama apewe pongezi kubwa.
Sio kwel ❌. Kipind kile nayey aliingia na yake kichwan hata yaliyomo kwel ilan baadhi aliyatupa akaja na mipango yake!! Hoja hapa hatutaki kila Rais akija aje na yake bali iwekwe ilan ya miaka 30 kila atakaeingia aishi humo!!!
 
Naunga mkono hoja ✔️. Ukifuatilia kwa haraka kila Rais anakuja na lake kichwan kiasi kwamba ilan kwake sio lazima!! Hatuwez fika popote kwa mtindo huu, Kama Taifa ni lazima tuwe na mpango mkakati wa maendeleo wa miaka 30 kila atakae kalia kiti cha urais afuate hilo.
Ukweli ni kwamba hata anayerithi tu kiti cha urais, aliyekuwa msaidizi wa aliyemrithi, na yeye anapokalia kiti hicho anajiona anayo 'mandate' ya kuchepuka kufanya yake mbali ya yale waliyokuwa wameyalenga kwa pamoja na huyo aliekuwa akimsaidia kutimiza malengo.
Huu ni ukichaa! Nchi haiwezi kuendeshwa hivi halafu ikapata mafanikio.
 
Well said mkuu
 
Naona umejiandika tu ili mradi umeweka maandishi yako Hapa pasipo kufikiri Wala kuwa na hoja zenye msingi,na kwa minajili hiyo unapaswa kuelimishana na kufumbuliwa kifikra
 
Yeah huu ndo uwanja wenyewe wewe wenye fikra sahihi kuweka zako hapa,ufinyu wa fikra na uwezo wa kufikiri unachagizwa na makasiriko bila kuangalia mantiki ya hoja iliyoko. Nikufunze kitu,hata kama umekasirika jifunze kupinga kwa hoja
 
KImsingi kila Rais anataka kuacha legacy yake...
 
Kipindi cha JPM ndo ilikua lakini kwasasa hapana mama apewe pongezi kubwa.
Hapana, jpm alikuwa na vitu maalum na ndiomaana baadhi ya wizara zilipewa %200 ya bajeti, jpm akiamua kufanya kitu kinafanyika, kama umesema nitamaliza kwa miezi 18 basi hakikisha ndani ya hiyo miezi 18 unakabidhi mradi, tofauti na sasa hakieleweki kipini kipi, mfano tuliambiwa tozo zinaenda kumaliza tatizo la wanafunzi vyuo vikuu kukosa mikopo je tatizo limeisha?
 
Changamoto kila kukicha,sanjari na mabadiliko ya kauli mbiu zisizo na tija.
 
Ukweli utabaki hivyo,tuna tatizo kubwa kwenye vipaumbele vya taifa,hatujui nini tunataka na wakati gani tunahitaji hicho tunachokitaka.

Madhara yake ni nchi kuendesha kama biashara ya daladala, kondakta ana nguvu kuliko dereva kwa kuwa tu ndiye mshika fedha.

Kipau mbele cha serikali hakikidhi bajeti angalau kwa 10%. Bajeti yenyewe ya serikali mpaka ina maliza mwaka haifiki 60%,lakini watu wanakaa mjengoni wanabariki ukanjanja huu na business as usual.

Commitment ya kuitumikia nchi hii ni fumbo la imani ndo maana kufika Canaan itatugaharimu muda sana kwa kuwa suala hili ni mindset. Database yake imejaa ubinafsi na upigaji wa kiwango cha juu sana.
Wasomi wa viwango vya phd, wanashindwa kupanga mipango ikapangika, maana kila mpango ukiletwa kwenye dinner table kuna 10% zao mule. Aibu tupu.
 
Back
Top Bottom