Taifa la Barbados limeamua kumuondoa Malkia Elizabeth II wa UK kama kiongozi wa juu wa taifa hilo

Taifa la Barbados limeamua kumuondoa Malkia Elizabeth II wa UK kama kiongozi wa juu wa taifa hilo

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Baada ya miaka 54 tangu iwe huru,leo taifa la Barbados limeamua kumuondoa Malkia Elizabeth II wa UK kama kiongozi wa juu wa taifa hilo. Mataifa mengine kama Canada na Jamaica yanaendelea kumtambua Malkia Elizabeth kama kiongozi wa juu wa mataifa yao. Barbados sasa itakuwa jamhuri.

Gavana mkuu wa Barbados bibi Sandra Mason amesema muda umefika wa wao kuacha historia ya ukoloni nyuma. Barbados ilitawaliwa na Uingereza na ikapata uhuru miaka 54 iliyopita, licha ya kupata uhuru iliendelea kumtambua Malkia wa Uingereza kama kiongozi wa juu wa taifa lao.

Asante

IMG_20200917_095835.jpg
IMG_20200917_095856.jpg
IMG_20200917_095901.jpg
 
November mwakani wameweka nia ya kujitoa
Tuone nani atafuata maana nafikiri hata ufalme UK uko mashakani
Miaka si mbali watabadilika tu
 
Sijaelewa; ni kutomtambua Malkia Elizabeth II au ni kutomtambua Malkia? Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kwamba akija malkia au mfalme mwingine watamtambua?

Nadhani wameshaona shida mbele kwamba nyakati za Her Majesty the Queen zinapita kwa kasi hususan umri so soon someone else gonna reign.

Now, the problem is not who is gonna reign, but his/her personal attributes! Kuna siku mtajikuta chini ya mtu asiye na maadili kwa hiari yenu wenyewe; bora kujitoa.
 
Huo ulikuwa ujinga wa kiwango cha standard gauge.. Hatimaye wamejitambua.... maendeleo hayana chama
 
Malkia Elizabeth

Visiwa wa Barbados vimetangaza nia yake ya kumuondoa Malkia Elizabeth kama kiongozi wa nchi hiyo na kuwa Jamuhuri.
''Muda umewadia wa kuachana na historia yetu ya kikoloni,'' Serikali ya taifa hilo la kisiwa hicho cha Caribbean imesema.

Ina lengo la kumaliza mchakato huo wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wake kutoka Uingereza, itakayofanyika mwezi Novemba mwaka 2021.
Hotuba iliyoandikwa na Waziri Mkuu Mia Mottley imesema raia wa visiwa hivyo wanamtaka kiongozi mzawa.

Kasri la Buckingham lilisema kuwa ni suala la serikali na watu wa visiwa vya Barbados.

Chanzo cha habari katika kasri la Buckingham kimesema kuwa wazo hilo ''halikuja tu ghafla'' na '' limekuwa likizungumzwa hadharani mara nyingi'', Mwanahabari wa BBC Jonny Dymond alisema.
Kuhusu Barbados:
  • Moja kati ya visiwa maarufu katika Caribbean
  • Ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1966
  • Malkia Elizabeth ameendelea kuwa mtawala wa kikatiba
  • Inajitegemea sana katika uchumi utokanao na shughuli za usafirishaji wa sukari, pia kwenye utalii.
  • Waziri Mkuu wake ni Mia Mottley, alichaguliwa mwaka 2018 na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
Kauli hiyo ilikuwa sehemu ya taarifa ya serikali ya kifalme, ambayo imetanabaisha sera za serikali na programu katika kuelekea vikao vipya vya bunge.
Wakati ikisomwa na gavana mkuu, ina maana kuwa imeandikwa na Waziri Mkuu wa nchi.

Hotuba hiyo pia ilinukuu onyo kutoka kwa Errol Barrow, Waziri Mkuu wa kwanza wa Barbados baada ya kupata uhuru, ambaye alisema kwamba nchi hiyo haipaswi "kurandaranda kwenye maeneo ya majengo ya wakoloni".

Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley

Sio sauti yake tu huko Barbados ambayo imekuwa ikipendekeza kuhama kutoka kwenye utawala wa kifalme. Tume ya ukaguzi wa katiba ilipendekeza hadhi ya jamhuri kwa Barbados mnamo 1998.

Mtangulizi wa Bi Mottley katika nafasi hiyo, Freundel Stuart, pia alitetea "kuhama kutoka kwa mfumo wa utawala wa kifalme kwenda kwa serikali ya jamhuri katika siku za usoni".

Barbados haitakuwa koloni la kwanza la Uingereza katika Carribean kuwa jamhuri. Guyana ilichukua hatua hiyo mnamo 1970, chini ya miaka minne baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Trinidad na Tobago walifuata nyayo mnamo 1976 na Dominica mnamo 1978.

Wote watatu wamekuwa ndani ya Jumuiya ya Madola, umoja wa nchi huru za makoloni ya zamani ya Uingereza pamoja na nchi nyingine ambazo hazina mafungamano ya kihistoria na Uingereza.
2px presentational grey line

Ni jambo lisilo la kawaida kwa nchi kumuondoa Malkia kama kiongozi wao. Nchi ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Mauritius mwaka 1992. nchi nyingine za Caribbean kama vile Dominica, Guyana, Trinidad na Tobago zilikuwa jamuhuri katika miaka ya 1970.

Nchi 15 ambazo ni sehemu ya dola ya Malkia zinaonekana kuthamini mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo na Uingereza.

Ni kweli, baadhi wamekuwa wakiongelea suala ya kuwa na wakuu wao wa nchi na kuachana na utawala wa kifalme. Lakini mara nyingi malengo ya kisiasa yamekuwa kikwazo.
Si mara moja kwa wanasiasa wa Barbados kueleza nia yao ya kuwa Jamuhuri.

Malkia Elizabeth, alipoitembelea nchi ya Barbados mwaka 1977, kama kiongozi mkuu wa nchi

Swali ni kuwa kama uamuzi huu utalingana na wengine. Jamaica awali alisema kuwa hiyo ni njia ambayo ingeifuata.
Umuhimu wa jambo hili unaelezwa kuwepo katika suala la kuondokana na 'historia ya kikoloni'.

Katika dhana ya kampeni ya Black Lives Matter, itakuwa jambo linalosubiriwa kuona kama hatua hii italeta msukumo wa kisiasa kwa serikali za Caribbean kuchukua mkono huo huo.

Na ikiwa hili litatokea, na kuondolewa kwa Malkia kama mkuu wa nchi kutlingana na, tuseme, kuondolewa kwa sanamu ya mfanyabiashara wa watumwa, basi hiyo inaweza kusababisha maswali magumu kwa familia ya kifalme ya Uingereza na Jumuiya ya Madola.

BBC Swahili
 
Na wafanye haraka kwa maana uongozi ujao wa U.K utakuwa wa kifalme na si Kimalkia tena!
 
Wakae waangalie nini watapata na nini watakosa.... Ila Visa za Free kwenda London ndio bye bye... Watalipia... na issue za Usalama itakuwa juu yao... kuna faida na hasara zake na watakao umia ni raia
 
Sijaelewa; ni kutomtambua Malkia Elizabeth II au ni kutomtambua Malkia? Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kwamba akija malkia au mfalme mwingine watamtambua?

Nadhani wameshaona shida mbele kwamba nyakati za Her Majesty the Queen zinapita kwa kasi hususan umri so soon someone else gonna reign.

Now, the problem is not who is gonna reign, but his/her personal attributes! Kuna siku mtajikuta chini ya mtu asiye na maadili kwa hiari yenu wenyewe; bora kujitoa.
Mbona unajichanganya kifikra.
Malkia anayejulikana as far as Barbados is concerned ni Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Hakuna Malkia mwingine.
Kutomtambua KAMA sovereign(mtawala wa Barbados) ni jambo la kikatiba.
N ndio maana wanataka kuwa a republic state.
Watachagua kiongozi wao ambaye atawala kulingana na katiba ya nchi.
 
Mbona wamechelewa sana
Halafu hawa waenglish hawa we acha tu yaani mambo wakifanya wenzao midomo na fujo kama zote ila wakifanya wao ni sawa tu siwapendi
 
Sijaelewa; ni kutomtambua Malkia Elizabeth II au ni kutomtambua Malkia? Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kwamba akija malkia au mfalme mwingine watamtambua?

Nadhani wameshaona shida mbele kwamba nyakati za Her Majesty the Queen zinapita kwa kasi hususan umri so soon someone else gonna reign.

Now, the problem is not who is gonna reign, but his/her personal attributes! Kuna siku mtajikuta chini ya mtu asiye na maadili kwa hiari yenu wenyewe; bora kujitoa.

Hapana
Wao wanataka kuwa Republican na kujitoa kwenye commonwealth ili wasiwe chini ya UK tena
Wanataka uhuru wao wenyewe
 
Hapana
Wao wanataka kuwa Republican na kujitoa kwenye commonwealth ili wasiwe chini ya UK tena
Wanataka uhuru wao wenyewe
.... kwani walipokuwa chini ya UK ni uhuru gani waliukosa? Malkia si alikuwa cheo tu cha heshima kisicho na mamlaka ya ku-enforce chochote kiutendaji?
 
Wakae waangalie nini watapata na nini watakosa.... Ila Visa za Free kwenda London ndio bye bye... Watalipia... na issue za Usalama itakuwa juu yao... kuna faida na hasara zake na watakao umia ni raia
Ukisikia colonial mentality ndio kama hii
 
Back
Top Bottom