Mpaka hapa tulipo kama nchi, tumetoka mbali sana!
Tumepitishwa jangwani sisi, kwenye miiba na mbigili tumepitishwa,
Tumepita kwenye machungu makali na kisha viongozi wetu badala ya kutengeneza vijana na watumishi waadirifu, wamejikuta wakitengeneza vijana wezi, watumishi wa umma mafisadi na Taifa la watu waliokata tamaa kabisa na kesho yao
Sababu moja wapo ni viongozi kuwa majizi na mafisadi huku wao wakiwahimiza waliochini yao wawe waadirifu mpaka kufa ili hali wakiwaona viongozi wao wanavyojichotea mabilioni ya mapesa na kutengeneza ufalume wao wa ki anasa hapa duniani
Hiyo imekuwa ni ambukizo baya sana kiasi ambacho hata wale viongozi tuliodhani wako sahihi katika kuliongoza Taifa letu bado wananchi na hasa watumishi wa umma, wamekuwa wakitupia lawama kwa viongozi hao na ukiangalia kwa undani, ni kuwa tu pengine imetokea kubanwa mianya ya ufujaji wa pesa za Wananchi
Tumeshuhudia aina mbalimbali ya viongozi na jinsi ambavyo viongozi hao wamekuwa wakiweka mikakati mbali mbali katika kulinasua Taifa letu ili kuondokana na umasikini uliopo
Lakini kila tulipopata kiongozi, sauti kubwa imekuwa ikisikka kuwa, HATOSHI NA HAFAI kwa kuwa huyu ni dhaifu, huyu ni mshamba na huyu ni hivi na vile!
Kama mtanzania, matamanio yako ni kupata kiongozi yupi na afanye nini ili pengine moyo wako utasema, This is the leader we will travel with to bring us the promised land
Kinachosikitisha zaidi, jamii pia ilishawakatia tamaa hata wapinzani, wakiwaona ni wale wale na hawatabadirisha chochote zaidi ya kujibadisha wao na maisha yao
Taifa la watu waliokata tamaa! Dawa yake nini?
Viongozi nao walishakata tamaa, hawana mawazo mapya, hawana uwezo wowote wa kuwatoa wananchi kwenye mtanzuko huu wa maisha duni na kukata tamaa, badala yake wamebaki kujisifia wasivyovianzisha wakati huohuo wakiviita ni miradi ya kukurupuka!