Taifa la waliokata tamaa maisha, ila hakuna namna mpaka mitano ikatike

Taifa la waliokata tamaa maisha, ila hakuna namna mpaka mitano ikatike

Biashara za Wananchi zimekufa, Wafanyabiashara wengi wamekata tamaa. Mzunguko wa pesa umedumaa, masoko yamesimama.

Watumishi wa Umma hawana uhakika juu ya nyongeza ya mishahara, miaka mitano wamepigwa kimya.

Wakulima wanalima, wakivuna soko la ndani halina bei, wanaambulia kupata chakula cha kushibisha matumbo yao.

Wanasiasa hawana usemi,atakalo sema mkuu ndio hilo litekelezwe hata kama halina tija. Wakitoa ushauri mzuri wanatumbuliwa.
Tuko kwenye "Shamba la Wanyama" - "The animal farm".
 
Tumeikabidhi nchi kwa Mfalme....Hasikii,haoni wala kujali vilio vya wanae,yupo busy anakoroga zege na kutandaza lami.Hatusemi kuwa hatuhitaji vyote hivyo Bali hatujaweka vipaumbele vya kununua saruji badala ya unga tukiwa na njaa.Maisha hayasimami na tunayaishi kila Siku.

CCM, turejesheeni Tanzania yetu mliyojimilikisha kupitia Katiba ambayo hamtaki tuiboreshe/tuibadilishe ili tujitawale tunavyoona inafaa baada ya makubaliano.
Maccm hayasikii mpaka damu itoke masikioni.
 
kazi ipo kweli kweli maana si kitoto kuna mtumishi wa Mungu aliwahi kusema walioshinda hawana furaha walioshindwa hawana furaha watu wote hawana furaha ila kikundi cha wahuni wachache tu ambao wameshika akili za watu. Nyerere alisema ukiona watu wanakusifiasifia sijui we Mungu sijui we Malaika waogope kama ukoma maana hapo sio wao ni matumbo kwasababu kuna faida wanapata kutokana na uwepo wako
 
Nawashangaa mnaosema watu hawapandishwi mishahara wakati madaraja wanapanda na juzi tu hapa jirani yangu kapanda!
 
Msoto mwanzo mwisho atatoka dikteta anaingia dikteta.Dikteta ni kiumbe kinachotazama maisha yake tu hata kama Jamii itaozea kwenye ufukara sio jukumu lake, kumbuka dikteta apendi watu smart bali dhaifu
 
Maisha tunayoishi sasahivi ndiyo maisha HALISI ya Tanzania.....hapo kabla tulikuwa tunaishi fake fake..kama mdada aliyeboost maziwa, akivua sidilia ndio sasa hivi tunavyoishi.
Enzi zile uongozi wa mtaa unakaa kikao kujadili mbinu za kuwazuia vijana kucheza pool table tangu asubuhi hadi jioni, mbona sasa hivi wameacha wenyewe, njaa mbaya Sana! Eti vijana wanakaa njia panda kuwashambulia wanawake wanaovaa nguo zisizo na stala...hahaha wako wapi sasa? Njaa imewakimbiza, wengine wameamua kugombania wanaume na dada zao...na bado wa mjini msio na kazi mtarudi huku kijijini tulime pamoja.
Viva JPM "ama kweli TUMEJIPANGA"
 
Uzaliwe Ndebile uwe na akili?
 
Endelea kulialia humu wenzako mwendo mdundo, na Kama ni wa kiume unakaribia kuolewa.
Ukilala ukiamka unalialia tu, pole sana

Ww lazima utambe maana ni mchepuko wa jiwe.
 
Back
Top Bottom