nafiri kama wewe sio mzinzi, uwe wa kwanza kurusha jiwe. however ujue kuwa Mungu anapenda watu wote, wazinzi na wasio wazinzi. sote tunaishi kwa neema tu. kama Mungu angekuwa kama wewe hivi, basi siku ileee, unayoikumbuka uliyozini angelikuulia palepale kwenye kitanda, lakini ana huruma alikuacha tu, ukamaliza, ukaondoka, siku ukajifikiria ukarudi kwake ukatubu akakusamehe na sasaivi unarusha mawe kwa wenzio. hapa hatushabikii uzinzi wa mtu, tuna msiba wa mtu aliyekuwa balozi wa tz katika sanaa kwa nchi mbalimbali za afrika mashariki na ameingiza ajira kwa watu wengi waliokuwa wakisambaza kazi zake za sanaa. ni muhimu kuelewa kuwa, wasanii wanatakiwa kutathiminiwa sana. kumbuka kagame alituma hadi ndege kuwachukua wale waimba kwaya chrust ambassadors....tuwajali watu wetu. don't judge his uzinzi, Mungu angehesabu maovu hakuna ambaye angesimama.
mimi nimependa sana hii, nimeona kumbe watz tuna umoja sana, hii kitu imetuunganisha watz sana sana. mimi hapa niko kahama shinyanga, huwezi amini kuna wasukuma walilia mitaani ajabu huku usukumani. kauli kama yako hiyo ikiitoa huku usukumani, unaliwa nyama nakwambia...and some of them don't even know whether incident ilitokana na uzinzi, wao wanamwangalia kanumba as kanumba hawaangalii uzinzi wake. Mungu anisaidie mimi binafsi kwasababu bado tu ni mwenye dhambi. wala siihitaji kuwanyoshea wengine vidole, labda kama ni kuwaombea tu Mungu awarehemu wageuke.