Hapa silaumu mafisadi.
Yaani wameshindwa kwenda kukata fito na miti kadhaa na kuja kujenga hizo kuta?
Sehemu za madirisha zingeachwa wazi ila vijana wawe ndani. Yaani hata udongo na fito nayo ni kazi? Hicho kijiji ni cha kuchapa viboko. Hiki ni kilema cha kutegemea serikali ije itufanyie kila kitu. Kijiji kizima kingelifanya hiyo kazi siku moja tu.
Inabidi kupata jina la Mbunge wa eneo hilo, mkuu wa wilya, mkoa, katibu kata, katibu tarafa, mwenyekiti wa kijiji....... Huu ni ukiwete mbaya kabisa duniani --KILEMA CHA MAWAZO.
Ningelaani kama kusingelikuwa na madawati na mabati juu. Hii shule ni BOMBA sana sana ukilinganisha na wengine tulizosomea. Masanilo, kama umetembea Sikonge nafikiri ulijionea mwenyewe shule za huku kwetu kama Iyombakuzova, Mibono, Pangale, Ipole, Tumbili, Utawambogo nk.
Hebu tuache kulaani kila kitu MAFISADI. Wananchi inabidi tubebe lawama ya asilimia 40 ya hali hii kwa ujumla. Yaani hakuna MWALIMU Juma wa kutibu magonjwa ya namna hii? Ningelimpeleka huko akatibu UTINDIA UBONGO wa Kijiji kizima. Mengine nakubali lawama ila hili mwenzenu SINUNUI.