Taifa letu limekosa maafisa Usalama wa Taifa wenye uzalendo kama alivyokuwa Lyatonga Mrema na wenzake. Ufisadi kama huu sio wa kuvumiliwa

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Nimedokezwa kuwa aliyepata tenda ya kuiuzia serikali vishikwambi vya sensa na walimu amepiga kama bil 10 faida ya pesa chafu.

Ripogi ya CAG imetupatia jibu sahihi kuwa kumbe pesa za umma zinapotea sababu tu rais hayupo serious kuzilinda.

Zinakwapuliwa na wahuni kama njugu.

Lakini taifa hili lingekuwa na maafisa usalama walio na uchunngu wa taifa lao kama Lyatonga Mrema (Rip) ukweli wa matapeli na mafisadi wanotuibia ungejulikana.

Lyatonga Mrema (Rip ) aliweza kupambana kwa taifa hili kwa kila namna hadi kulala vichakani ili kupinga wizi na utapeli. Leo hii tunaibiwa kama.

Taifa halina wazalendo.

 
Mmesema mnamuomba mungu kwa kulia kupiga magot na kusali na 2025 apite tena awaongoze
 
Zamani watu waliapa kulinda nchi yao. Leo hii tunaapa kulinda maslahi ya chama. Kiongozi anayetokana na chama yakiwekwa wazi mabaya yake; chama kitadhalilishwa.

Usalama nao wamegeuka kuwa 'chawa'
 
Siunaona hata bosi wao alitenguliwa.
Mambo nimengi muda hautoshi na majibu ni tete
 
Wazanlendo na wenye uchungu na hii nchi tupo sana tu. Lakina shida huko juu kuna ndugu, jamaa na watoto wa viongozi, ukikaza unaondoka mwenyewe.
 
UVCCM imejaza vijana wenye upeo mdogo sana wanaoshindwa kujitegemea, wamejazana huko kuganga njaa. Huko ni nadra sana kumpata mtu msafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…