Kuna watumishi(Wataalamu) wengi wazuri wako serikalini miaka mingi hadi kufikia level za Senior or Principle hawajatumika ipasavyo, yeye ni nani kuwa wa tofauti na special kushinda wazoefu waliyotumikia serikali miaka nenda rudi na wana ma degree kadhaa kichwani!?Nimemfuatilia sana Upendo Peneza. Ni kiongozi anayetumia akili sana, na amekuwa tofauti na Chadema wengi wanaokurupuka.
Ni msomi wa haja, madigirii yamejaa kichwani, ana hekima kubwa sana.
Natamani mama ampe majukumu makubwa sana serikalini. Pamoja na hayo, kama anapenda siasa, apewe nafasi afanye siasa.
Ila ninamuona kama anapenda kazi za kitaalamu, sio mpenda makelele.
Taifa limechelewa kupata utumishi wake, ila wakati wa Mungu ni wakati sahihi.
Ni muhimu kuwa na succession plan, sio kutoa vyeo kwa mihemko! hii ina demoralize watumishi wengi sana wanao tumikia serikali kwenye hard times na mazingira magumu ya utendaji.