Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Taifa letu pendwa mzimwini
Taarifa zimetufikia zenyeujonzi
Radio zimetutenga mafukara
Rafiki wetu taarifa katuaga
Viongozi wamegawanyika
Vikumbo wapigana
Samia kauza Bandari
Samia hajauza Bandari
Lakini ndugu zangu
Lambisa mkataba mangunga
Mkataba mmeuona?
Macho yenu mmethibitisha?
Mgenzi nimeusoma
Mlengo umeketi kisheria
Yamkini Bandari si yetu
Yaamini yangu ya kikwetu
Sheria pendwa zimevunjwa
Shari si kwa hao mabunjwa
Dhiki ni kwetu sie kabwera
Dhahama kuipambana
Wasomi wamegawanywa
Wasomi Vilaza wasomi khalifa
Wazalendo na mzungu mweusi
Wamalenga na wasusi
Taifa limegawanyika
Taarifa zimepotoshwa
Katika ukweli ulio mezani
Kariba ya uongo imetutia huzuni
Mwatudanganya mkataba mezani
Mwanza kwetu uwezo DP wedi
Wamalenga twataka vipengele
Wazigua wapewa kengele
Kelele DP wedi si rofa
Kejeli wanazuoni wamehongwa.
Fukara DP world kuhonga wanazuoni?
Fursa kutaka ya tumboni?
Nahitima kwa huzuni
Naona hatima ya kwinini
Kwa kwikwi na machozi
Kwanini muuze Bandari?
Pascal Ndege
S. L. P...........
JAMII FORUM
TANZANIA
Taarifa zimetufikia zenyeujonzi
Radio zimetutenga mafukara
Rafiki wetu taarifa katuaga
Viongozi wamegawanyika
Vikumbo wapigana
Samia kauza Bandari
Samia hajauza Bandari
Lakini ndugu zangu
Lambisa mkataba mangunga
Mkataba mmeuona?
Macho yenu mmethibitisha?
Mgenzi nimeusoma
Mlengo umeketi kisheria
Yamkini Bandari si yetu
Yaamini yangu ya kikwetu
Sheria pendwa zimevunjwa
Shari si kwa hao mabunjwa
Dhiki ni kwetu sie kabwera
Dhahama kuipambana
Wasomi wamegawanywa
Wasomi Vilaza wasomi khalifa
Wazalendo na mzungu mweusi
Wamalenga na wasusi
Taifa limegawanyika
Taarifa zimepotoshwa
Katika ukweli ulio mezani
Kariba ya uongo imetutia huzuni
Mwatudanganya mkataba mezani
Mwanza kwetu uwezo DP wedi
Wamalenga twataka vipengele
Wazigua wapewa kengele
Kelele DP wedi si rofa
Kejeli wanazuoni wamehongwa.
Fukara DP world kuhonga wanazuoni?
Fursa kutaka ya tumboni?
Nahitima kwa huzuni
Naona hatima ya kwinini
Kwa kwikwi na machozi
Kwanini muuze Bandari?
Pascal Ndege
S. L. P...........
JAMII FORUM
TANZANIA