Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Nakwepa sana kitu kinaitwa chuki, nakwepa mno visasi... Chuki huzaa kisasi na kuviziana.... Kuombeana mabaya na kushindwa
Kama Taifa tulipitia vipindi tofauti vya chuki... Achana na chuki ile ya majirani kama ilivyo sasa... Hii inayojaribu kutengenezwa kati yetu na Wakenya.... Tuliwahi kupitishwa kwenye chuki za kiimani Waislam VS Wakristo... Chuki mbaya mno hii.... Lakini Mungu ni mwema hili likapita bila madhara makubwa
Hatujawahi kuingia kwenye chuki kubwa za kikabila... Hizi nazo zina sumu mbaya sana... Zinaweza kushabihiana kwa karibu na chuki za kidini...
Tafakuri, maono na hekima zetu zimeshindwa kutuepusha na chuki za kisiasa.... Kwasasa Waislam na Wakristo ni kitu kimoja.. Ila Watanzania kwa sasa wanachonganishwa na siasa kupitia wanasiasa...!
Uongozi ni kipawa... Tunaaswa kwenye misahafu kulinda vitu viwili kuliko vingine vyote.... MOYO na MDOMO... kwakuwa hivi ndio karakana ya mambo yote... Mema na mabaya... Moyo wenye msingi asili wa wazo na mdomo kama kiwakilishi na kipaza sauti cha kusambaza....
MDOMO ndio hatari zaidi ndio wa kulindwa zaidi kwakuwa chochote kitakachotoka humo hakina rivasi... Ni kama risasi ikitoka imetoka.... Kifuatacho ni madhara
Tuliombee taifa hali ni ngumu, chuki ni za wazi kabisa.. Tuwaombee viongozi wetu... Tuwashauri kwa hekima.... Kwa tafakuri kuu...
Maneno ni sumu, maneno yanajenga chuki, maneno yanafarakanisha.. Maneno yanaleta vita na kuangamiza roho nyingi zisizo na hatia......!!!
Tulitegemea leo iwe furaha kuu kwa timu yetu ya Taifa kufika ilipofikia baada ya miaka 40... Tulitegemea msisimko, shangwe, nderemo vifijo na kila aina ya bashasha... Lakini kilichopo kwa sasa ni kipi?
Hakuna shamrashamra, hakuna bashasha, hakuna msisimko wowote bali kuna MAOMBI hasi ya kutaka Taifa stars ishindwe.... Hii ndio itakuwa furaha ya wengi.... Kushindwa kwa stars kutaleta furaha kuliko kushinda....!!
Hapa ndipo tulipolifikisha Taifa.... Tutachomokaje kwenye mtego huu? Muda utasema... Siombei timu yangu ya Taifa ishinde wala ishindwe... Sitaki awepo mshindi kwenye hizi chuki...
Yeyote atakayeshinda ndio mwanzo wa kumea kwa mbegu ya chuki iliyokwisha pandikizwa...
Mungu ibariki Tanzania na watu wake...!!!!