UTANGULIZI
Uchungu wa kumpoteza mtu unayempenda, kazi unayoipenda au kitu unachokipenda kinaweza kuleta athari kubwa zisizoelezeka. Changamoto hazikwepeki maishani na wahenga walisema shida tumeumbiwa binadamu. Lakini ni jinsi gani tunaweza kuzikabili hizi changamoto wakati zinapotukuta? Kila mmoja ana uwezo wake wa kubeba mizigo mizito kwa jinsi alivyoumbwa au alivyolelewa. Tatizo linakuja pale ambapo mtu anakabiliwa na tatizo na anaona hawezi kulihimili. Hii inapelekea mtu kukosa matumaini na hatimaye kupelekea msongo wa mawazo au ugonjwa wa sonona.
Picha Kutoka Mtandaoni
Habari za watu kuuana zimeanza kushamiri hapa Nchini: watoto kuua wazazi wao, wazazi kuua watoto, mke kuua mume, mume kuua mke au vijana wadogo kuuana kwasababu ya mapenzi. Tunasoma habari za wafanyakazi kuua mabosi wao au mabosi kuua wafanayakazi wao. Tunasikia habari za marafiki kuuana na watu kujinyonga kwasababu mbalimbali. Na haya matukio yameanza kuonekana kama jambo la kawaida sana katika Jamii.
Waathirika wengi wa ugonjwa wa afya ya akili ni vijana chini ya miaka 50 kutokana na taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO). Hii inaonyesha hatari kubwa iliyopo maana vijana ndio nguvu kazi ya Taifa. Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu aliitisha Kongamano la kwanza la afya ya akili mwezi wa kumi tarehe 10 mwaka jana 2022. Aliwaelezea wadau wa sekta ya afya kuwa Nchini Tanzania kuna wagonjwa Milioni 7 wenye ugonjwa wa akili wakiwemo watu zaidi ya Milion 1.5 wanaoishi na ugonjwa sonona.
Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu
Picha Kutoka Mtandaoni
Chanzo cha tatizo
Ugonjwa wa afya ya akili hauibuki tu ghafla. Mtu anaweza kuwa na ugonjwa huu kwa kuzaliwa nao, ama kwa matumizi ya madawa ya kulevya ambayo huathiri ubongo na namna ya kufikiri ama kwa sababu nyingine za Kisaikolojia ambazo mtu huzipata kupitia matukio mbali mbali yanayomsibu katika maisha. Ningependa kujikita zaidi kwenye sababu za Kisaikolojia ambazo zenyewe hupelekea msongo wa mawazo ambao athari zake ni kubwa zaidi kwa mtu binafsi lakini zaidi kwa watu wengine wanaomzunguka.
Picha Kutoka Mtandaoni
Mtu mwenye msongo wa mawazo mara nyingi huwa ni mpweke,mwenye wasiwasi, anajiona hafai kuishi wala haoni umuhimu wake tena katika Dunia. Inapofikia hali hii mtu huwa anakosa matumaini na anaona kila mtu ni adui. Hili linamfanya kushindwa kuamini mtu na kukosa nguvu ya kushirikisha watu matatizo anayopitia. Msongo wa mawazo ukizidi hupelekea mtu kuwa na ugonjwa wa afya ya akili. Mtu huyu kwasababu mbele yake anaona kiza ataanza kutafuta faraja za muda mfupi. Atajiingiza kwenye ulevi uliopindukia, matumizi ya madawa za kulevya au kufanya uhalifu kama wizi, ubakaji na hata mauaji.
NINI KIFANYIKE?
Ushauri kwa Serikali
Takwimu Kutoka Mtandaoni
Picha Kutoka Mtandaoni
Familia ndio nguzo ya kwanza ya umoja na mshikamano. Familia bora huweka misingi bora ambayo itainua jamii na Taifa kwa ujumla. Wazazi tusikwepe majukumu yetu. Malezi ya watoto yanatuhusu kwa sehemu kubwa sana. Tusiachie majukumu hayo kwa walimu au wasaidizi wa nyumbani. Hata kama mihangaiko ya kazi ni mingi tujitahidi kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wetu. Dunia imebadilika sana na imechafuka sana. Kuna vitendo vya ushoga na usagaji vimeshamiri, kuna habari za watoto kulawitiwa mashuleni, makanisani na Madrasa na watu waliotakiwa kuwalinda. Tusipokua na ukaribu na watoto wetu tukaongea nao na kujenga urafiki nao wataogopa kutukimbilia wakipata shida na hivyo kudumbukia kwenye matatizo ya msongo wa mawazo na ugonjwa wa afya ya akili.
Ushauri binafsi
Ahsanteni wasomaji wote.

- Elimu kuhusu afya ya akili itolewe kuanzia mashuleni. Ugonjwa wa afya ya akili huanzia mtoto akiwa miaka 14 kutokana na taarifa ya Shirika la afya Duniani. Hapa Nchini huu ni umri ambao watoto wengu huwa wanaingia kidato cha kwanza. Watoto wajifunze dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kuzikabili. Ni elimu pekee itakayoweza kookoa taifa hili na kizazi cha sasa na baadae.
- Serikali iwekeze kwenye fani ya utabibu na uuguzi wa afya ya akili. Tanzania ina uhaba wa Madaktari na washauri wa afya ya akili. Serikali kupitia Wizara ya afya itenge bajeti ya kuwadhamini asilimia 100 wanafunzi wenye nia ya kusomea afya ya akili katika vyuo vya ndani na nje ya Nchi. Takwimu za Wizara ya Afya inaonyesha ongezeko la wagonjwa wa afya ya akili kwa asilimia 40 ndani ya miaka miwili tu kati ya mwaka 2018 mpaka 2020. Wakati wagonjwa wanaongezeka Hospitali na wauguzi bado ni wachache hii inahatarisha maisha ya wagonjwa hata ya wauguzi wenyewe ambao wanapaswa kuhudumia wagonjwa wengi zaidi ya uwezo wao.
Takwimu Kutoka Mtandaoni
- Serikali itambue kwamba kinga ni bora kuliko tiba. Hivyo iwekeze zaidi katika njia za kudhibiti visababishi vya ugonjwa wa akili kuliko kusubiria watu wawehuke na kukimbilia kuwahudumia wakiwa Milembe, Muhimbili, Bugando,au Hospitali ya Lutindi Tanga.
- Serikali kupitia wizara ianzishe mpango utakaowezesha watu kuweza kuongea kwa uhuru shida zao bila kuhisi kunyanyapaliwa au kuhukumiwa. Mpango huu unaweza kuratibiwa na wataalamu wa afya ya akili waliobobea katika ushauri nasaha. Njia zinazoweza kufikiwa kwa urahisi ni kupitia simu kwa namba ya bure ya kupiga au kutuma meseji ambayo itatolewa. Mtu akiwa na tatizo ataweza kutumia namba hiyo na kuunganishwa na wataalamu moja kwa moja ambao watampa msaada kwa wakati.
- Sote tunaishi katika jamii yenye watu wenye tabia tofauti. Uwajibikaji unaanza na sisi wenyewe. Tukiona mtu ana shida tusisite kumsaidia. Tusiseme ni shida zake mwenyewe. Viashiria vya tatizo huwa vinaonekana mapema. Kama tunaona hatuwezi kutoa msaada basi tunaweza kumsaidia mtu kwa kumuelekeza sehemu anazoweza kupata msaada. Tusingoje mpaka ifike siku tujilaumu kwamba tumechelewa. Tusiwanyayapae wenzetu wenye shida. Tusiwatenge na kuwabagua bali tuwajali na kuwapenda.
Picha Kutoka Mtandaoni
- Matumizi ya mitandao ya kijamii. Mitandao ya Kijamii inaweza kumsaidia mtu au kumdidimiza na kumuongezea tatizo. Ni vyema tuitumie vizuri ili kuwasaidia na kuwainua wengine. Tuwe sehemu ya kuponya wengine. Wakati tunachangia mijadala tujitahidi kutumia lugha yenye upendo na kutokejeli shida za wengine. Mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe.
Familia ndio nguzo ya kwanza ya umoja na mshikamano. Familia bora huweka misingi bora ambayo itainua jamii na Taifa kwa ujumla. Wazazi tusikwepe majukumu yetu. Malezi ya watoto yanatuhusu kwa sehemu kubwa sana. Tusiachie majukumu hayo kwa walimu au wasaidizi wa nyumbani. Hata kama mihangaiko ya kazi ni mingi tujitahidi kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wetu. Dunia imebadilika sana na imechafuka sana. Kuna vitendo vya ushoga na usagaji vimeshamiri, kuna habari za watoto kulawitiwa mashuleni, makanisani na Madrasa na watu waliotakiwa kuwalinda. Tusipokua na ukaribu na watoto wetu tukaongea nao na kujenga urafiki nao wataogopa kutukimbilia wakipata shida na hivyo kudumbukia kwenye matatizo ya msongo wa mawazo na ugonjwa wa afya ya akili.
Ushauri binafsi
- Ukiwa na tatizo ambalo linakuumiza na unaona huwezi kulimudu peke yako tafadhali tafuta watu unaowaamini na kuwashirikisha. Usiweke vitu moyoni na kujiona hufai. Ongea. Ongea. Ongea. Usidhani uko peke yako na kuona aibu na uoga. Kukubali una tatizo na kuliongelea ndio njia ya kwanza kuelekea kwenye uponyaji.
Ahsanteni wasomaji wote.
Upvote
6