Taifa Linagua

Taifa Linagua

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Taifa letu linaugua
Nchi tofauti tofauti zina matatizo mbalimbali ikiwemo njaa, vita nk. Sisi kama watanzania tuna ugonjwa wa chuki.

Sisi hjipambanua kama taifa lenye amani, huku viongozi wetu wakijisifia kila Kona kuwa wameweza kusimamia na “kulinda” amani kwa miaka mingi na kuwazodoa majirani zetu kama Kenya kwa yale yaliyowakumba.

Pamoja na sifa hizo, tunajua wazi kuwa si kweli. Sielewi kabisa kwa nini viongozi wanaukimbia ukweli kuwa nchi Ina fukuto la chuki kuu. Kinachonijia akilini ni kile alichosema Jaji mstaafu Warioba kuwa jeshi la polisi limeingizwa kwenye siasa.

Wanasiasa walio madarakani wanapuuza chuki iliyopo kwa kuwa wana uhakika polisi watawalinda. Hawa polisi ni watanzania, Hawa polisi wana nyama na moyo. Huenda hawajafikwa na yale yanayowafika watanzania wengine. Au huenda wamefikwa ila kwa namna walivyopewa maelekezo, wanajikuta wakiwa watumwa.

Ugonjwa wa chuki si wa kupuuza. Hakika nawaambia. Kwa sababu ni ugonjwa unaosababishwa na “MALIMBIKIZO“ ya maumivu yaliyokosa msamaha. Kwa miaka kadhaa sasa Watanzania wamepita na wanapita kikaangoni kwa sababu ya wanasiasa wanaodhani hii nchi ni ya kwao peke yao.

Kwa nguvu na madaraka yao wameweza kupandikiza mbegu ya mgawanyiko, uonevu, unyanyasaji, vitisho na hofu ya utekaji na mauaji. Hebu fikiria mtu anabeba haya yote, bado kodi unamlabua kotekote, na huduma za kijamii umembania. Unategemea nini?

Ukweli ni kuwa chuki kuu humfanya mtu ajisikie kama amekabwa, anakosa hewa na hutafuta namna ya kujisaidia ili imtoke... hapo ndipo “KISASI” hutokea. Ubaya ni kuwa, wakati polisi wakiwa bize na yasiyowahusu, lile jukumu la ulinzi na usalama linakuwa limeachwa na ombwe isiyozibika ndio maana watekaji wamekuwa na nguvu kuliko jeshi la polisi.

Sitaki kuwahusisha polisi na utekaji ikizingatiwa kuwa watekaji hujitambulisha kama polisi na wanakuwa na vitendeakazi vya polisi, watajihusisha wenyewe wakipenda kwa kuwa hawajawahi kukamata watekaji wenye kujitambulisha kama polisi wakatuambia kuhusu kosa la kutumia Jina la jeshi la polisi na vifaa vyao.

Kwamba, kama Kuna visa 50 (kwa mfano) vya utekaji na kuuawa au kuumizwa, halafu polisi inakamata watu kwa visa vitano (5) halafu hivyo 45 vinakuwa kwenye kundi la “TUNAENDELEA NA UCHUNGUZI” kwa miaka na miaka, hakika hapo watekaji wamekuwa wajanja kuliko polisi.

Sasa Hawa watanzania wanaoona kuwa hata vile visa vinavyopata ufumbuzi vinahusu upande wa serikali au chama fulani na upande wa wananchi ni bila bila, hapo ndipo chuki huanza kumea...

Ugonjwa huu wa chuki una makundi haya
1. Chuki kati ya wananchi na jeshi la polisi (yule aliyetakiwa kuhakikisha usalama wako akafanya mambo mengine akakuacha hatarini na wala asijali)
2. Chuki dhidi ya serikali (kwa kunyamazia hao walioacha kazi zao na kufanya yasiyowahusu)
3. Chuki dhidi ya kundi linalopendelewa. Hii iwe wazi kuwa wanaopendelewa ni CCM. Wao wakipata changamoto mambo yao yanatatuliwa chaaaap lakini wengine wanasubiri. Ieleweke kwamba kuna watu ni CCM kimaslahi lakini moyoni wanaamini mambo tofauti. Sasa unaweza ukadhani una watu (CCM) wenzako wanaokusapoti kwa kuwa wamevaa nguo za kijani, kumbe wapo na chuki zao
4. Chuki dhidi ya mfumo kandamizi
5. Chuki dhidi ya wao wenyewe (kwa kushindwa kufanya kitu). Iko hivi, unapokuwa na changamoto ambayo unatakiwa wewe ndio uitatue, lakini unajikuta huna uwezo huo, unaanza kujichukia, kujiona huna thamani.

Sasa ikitokea umebeba na chuki nyingine hapo juu, kinachobaki ni “KUJILIPUA”

Ukitazama comments za watz kuhusu ajali na kifo cha kundi wanalolichukia, tena wanasema kwa uwazi, hakika utajua Hawa wameamua KUJILIPUA. Hapo kabla, wakati wakiwa na hofu ya kutafutwa na TCRA, walikuwa wakisema “MWANASHERIA WANGU AMESAFIRI” lakini kwa sasa hakuna cha hofu... Hawa wamempiga huyu, wale wamefanya hivi au vile....

Fukuto ni kali... ni kama bomb lililorushwa, linagaagaa kabla ya kufumuka. Kwa nini kati ya comments 100 moja tu itakie wabunge waliopata ajali afya njema, na 99 zitamani wafe... hivi wabunge hawaogopi? Hawana macho au hawajui kusoma? Ingekuwa mimi na pensheni ningeacha nijitoe huko siasani niwe salama. Usikute wameona hizo comments wakadhani ni za “ChatGPT” (AI)

Je, dawa ni nini?
Haki! Misingi ya haki isimamiwe na mihimili yote ya serikali Kuondoa yale maagizo ”NATAKA MKEKA WA KIJANI kwenye uchaguzi”
Kushughulikia visa VYOTE vya utekaji, mauaji kwa kuanza na cha Lisu ambacho kinakaribia kuwa na jubilee ya miaka 10 bila ufumbuzi.
Kufuta upendeleo. Kwamba kila mwananchi ana haki sawa bila kujali kama ni CCM
kuwaondoa polisi kwenye siasa (kama aliyoshauri Jaji Warioba)
Kusimamia upatikanaji wa katiba ya wananchi

Dawa ni chungu. Ila usipoinywa madhara ni makubwa zaidi. Siku isiyo na jina tutasikia wananchi (Sio Yanga) wamefanya mambo wao 1 serikali 0
 

Attachments

  • 1733031958857.jpg
    1733031958857.jpg
    208.8 KB · Views: 7
  • 1733558173764.jpg
    1733558173764.jpg
    113 KB · Views: 5
  • 1733558171008.jpg
    1733558171008.jpg
    101.9 KB · Views: 5
  • 1733558492569.jpg
    1733558492569.jpg
    195.4 KB · Views: 7
  • 1733558485824.jpg
    1733558485824.jpg
    247 KB · Views: 6
Hakika tumefikia hatua mbaya, we fikiria mkuu wa wilaya anaagiza, shule ifukuze wanafunzi ambao wazazi wao ni chadema.

Leo eti Ili mkurugenzi, ama DC kubaki kwenye cheo chake au ku-secure uteuzi mwingine basi lazima ahakikishe CCM inashinda by hooks and crooks.

Kigezo Sasa si uwezo na namna bora ya kuwahudumia wananchi, bali kuhakikisha mkeka wa kijani kwenye uchaguzi.

Leo, Sifa za mtu kuteuliwa kuwa kiongozi wa umma si weledi, uwezo na uzalendo, bali ni ama awe CCM au chawa bin kunguni wa utawala uliopo. Watu wanao teuliwa kwa Sifa hizo hawana uwezo wa kutatua changamoto za maendeleo Kwa TAIFA; kimsingi si wabunifu na Wala hawana tija. Ni wale wa ilimradi kumekucha wameingia ofisin, wanaopokea mishahara na posho basi.

Zaidi wanabaki kuwa attention seekers Kwa kufanya vioja mbali mbali au petty issues ili waonekane kuwa wanafaa Kwa mamlaka zao za uteuzi.

Zaidi ni watu wanaosubiri maelekezo na siyo problem solvers kwenye jurisdiction zao. Kwa mwenendo huu, tusahau kuhusu maendeleo ya kweli, tutabaki kupiga maktaimu tu.
 
Back
Top Bottom