Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!

Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali tuu kuhusu watu watu, kwa kulisaidia jeshi letu la polisi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuitumia mitandao ya kijamii positively as source of a security tip ya vital information kuhusu uchunguzi mbalimbali. Usisubiri hadi mtu akaripoti polisi kuhusu uhalifu, wenzetu wakiona chochote kwenye social forum, kama security implications, wanakichukulia very seriously.

Tangu kushambuliwa kwa Tundu Lissu, na watu wasiojulikana, jana kuna bandiko humu, limewataja kwa majina, waliopanga mpango huo, huku wakipanga mipango mingine miovu.

Nawaomba waichukulie taarifa hii hapa if very serious
Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana
Taarifa yenyewe ni hii

Anaandika Ansbert @Ngurumo

Very important Tip:

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, HAKUWA KIKAONI

Kinondoni


Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

Siha haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa walifanya makosa.

Isamilo, Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.
2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.
3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.
4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya Kwa Malisa, katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land Cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

Ansbert Ngurumo
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14:02:2018

Japo mimi binafsi ni kama Tomaso, huwa siziaamini baadhi ya taarifa za wanasiasa kirahisi rahisi, ikiwemo taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, kwa vile licha ya kuwa ni mwanasiasa, pia ni mwana habari, hivyo taarifa hii kihabari ni taarifa muhimu sana kuhusiana na shambulio la Lissu!.

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa walifanya makosa.", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.

Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.

Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".

Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.

Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.

Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.

Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.

Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimewahi kuyazungumza hapa TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

Ila pia niliwahi kutoa tahadhari, sio kila unachosikia lazima ukiseme Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Na mwisho namuuliza Ngurumo, akitafutwa ili ayathibitishe haya, anaweza kuthibisha?.

Paskali

PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Pascal Mayalla Paskali, tunazuguka mbuyu, haya mauaji yote, utekaji, upotezwaji and all evils against upinzani, anayeamrisha yote haya anajulikana. Kila mmoja anamjua, na wewe unamjua (tafadhali nyamaza, usijiweke kwenye matatizo kumtaja), na shetani anamjua, na Mungu anamjua, na Pope anamjua wooooooooooooooooooooooooooooooooooooote wanamjua. Ni muda ndio utasema!
 
Polisi walishasema hawafanyii kazi habari za kwenye mitandao..ila kwa hili wanaweza kuzifanyia kazi maana zimeenda kugusa pabaya...ila kwa dalili zooote hizi na Mimi naweza kusema polisi wanausika na udunguaji ule..basi Tu kwa vile hatuna namna ya kushinikiza wachunguzi huru WA kimataifa waketwe..na waliohusika nao Kati ya vitu hawataki kusikia Ni kuwaamvia Scotland yard wanakuja
 
Mkuu pasco tumsifu yesu Kristu

Naomba jibu

Ni wakati gani Ngurumo anakuwa mwanahabari na wakati gani anakuwa mwanasiasa tena kamanda wa chadema kikwelikwelii?

Utamtofautishaje Ngurumo wa siasa na mwanahabari?

Nijibu nirudi kwa mapana
 
Pale Ikulu kuna mtu aliamuru spika awashughulikie huko bungeni na yeye wakitoka huko bungeni basi huku nje atawashughulikia.

Kuna mtu tena katoa mamilioni cash kwa ajili ya matibabu ya mbongo movie mmoja ila sio kuhimiza Lissu apewe stahiki zake za kitiba,aakiongea anajifanya mcha Mungu ila ni mbaguzi na mvunjanji wa umoja na upendo aliyejaa chuki dhidi ya wenye mawazo tofauti.

Amejivisha uungu mtu na kuwafanya wasaidizi zake Kama Bashite,MMunyeti etc wafanye watakalo huku wakijitamba ni wateule wa Mungu.

Uhuni na uhalifu huu una baraka za boss wao,achilia mbali masheikh wanaopotea kama sindano nyakati za giza huko Zanzibar na siku hizi watu hawaokotwi tena kwenye viroba fukweni mwa bahari.

Awamu ya V-WONDERS!!!
 
Pascal Mayalla Paskali, tunazuguka mbuyu, haya mauaji yote, utekaji, upotezwaji and all evils against upinzani, anayeamrisha yote haya anajulikana. Kila mmoja anamjua, na wewe unamjua (tafadhali nyamaza, usijiweke kwenye matatizo kumtaja), na shetani anamjua, na Mungu anamjua, na Pope anamjua wooooooooooooooooooooooooooooooooooooote wanamjua. Ni muda ndio utasema!
Na hata huyo unayemsema naye anamjua.
 
Pascal Mayalla Paskali, tunazuguka mbuyu, haya mauaji yote, utekaji, upotezwaji and all evils against upinzani, anayeamrisha yote haya anajulikana. Kila mmoja anamjua, na wewe unamjua (tafadhali nyamaza, usijiweke kwenye matatizo kumtaja), na shetani anamjua, na Mungu anamjua, na Pope anamjua wooooooooooooooooooooooooooooooooooooote wanamjua. Ni muda ndio utasema!
Timu iliyokwenda Dodoma kumpiga Lisu Risasi ni Le mutuz, Lipumba Jerry muro na Maliyamungu Bashite sio siri tena
 
Pale Ikulu kuna mtu aliamuru spika awashughulikie huko bungeni na yeye wakitoka huko bungeni basi huku nje atawashughulikia.

Kuna mtu tena katoa mamilioni cash kwa ajili ya matibabu ya mbongo movie mmoja ila sio kuhimiza Lissu apewe stahiki zake za kitiba,aakiongea anajifanya mcha Mungu ila ni mbaguzi na mvunjanji wa umoja na upendo aliyejaa chuki dhidi ya wenye mawazo tofauti.

Amejivisha uungu mtu na kuwafanya wasaidizi zake Kama Bashite,MMunyeti etc wafanye watakalo huku wakijitamba ni wateule wa Mungu.

Uhuni na uhalifu huu una baraka za boss wao,achilia mbali masheikh wanaopotea kama sindano nyakati za giza huko Zanzibar na siku hizi watu hawaokotwi tena kwenye viroba fukweni mwa bahari.

Awamu ya V-WONDERS!!!
wanafanya kazi kama enzi za idd Amin na Maliyamungu, wameiga stye hiyo, Mtukufu akitaka jambo baya lifanyike haraka anatimwa Maliyamungu Bashite na kikosi chake kumteketeza mtu haraka.
 
Polisi walishasema hawafanyii kazi habari za kwenye mitandao..ila kwa hili wanaweza kuzifanyia kazi maana zimeenda kugusa pabaya...ila kwa dalili zooote hizi na Mimi naweza kusema polisi wanausika na udunguaji ule..basi Tu kwa vile hatuna namna ya kushinikiza wachunguzi huru WA kimataifa waketwe..na waliohusika nao Kati ya vitu hawataki kusikia Ni kuwaamvia Scotland yard wanakuja

Inawezekana kuwa kweli ni Polisi au la,yawezekana pia siyo Polisi ni wale wacheza shoo stajini wakati wa kampeni.Nakumbuka kabla ya Uchaguzi wa 2015 hawa wacheza stajini waliwekwa kwenye misitu fulani hukooooooooooooooooooooooooo TBR wakawa wanapewa mafunzo makubwa sana hasa ya kufanya mauaji,hivyo tunaweza bila kujua tukawasema Polisi lakini ndani kabisa Polisi nao ni watumiwa tu.Ila wanaingia kwenye mtego sababu wameshindwa kufanya wajibu wao kama Polisi
 
Back
Top Bottom