Taifa linaloona Urais ni kupokezana vijiti baina ya wakristo na waislam ni taifa la wajinga

Umenena vyema,huu ni upumbafu wa hali ya juu,ccm waleta upuuzi mwingi sana hata ule wa viongozi wa dini kuhudhuria vikao vya serikali na vyama vya siasa ni upuuzi mwingine.
Tactical Bribes ??!
 
Hahaa...ila kweli
 
Kwa hiyo Januari Makmba mtoto wa Yusuf Makamba ndiyo amekutuma uandike pumba hizi? Halafu kuna wengine wamemshauri akabadili dini awe mkristu kwa vile mama yake ni Mkrist, ili baada ya Samia Muislamu aje yeye na kofia ya Ukristu.

Nakupa tu kwa ufupi. Januari Makamba hata kama ataruhusiwa kuwa na dini zote mbili yaani Ukristu na Uislamu, hawezi kuwa Rais wa Tanzana mpaka anakufa.

Yeye tayari ni mtu anayesemwa na nayaetaka kama vile Edward Lowassa na Maalim seif Hamad walivyoutaka Urais wa Tanzania na ZNZ kuanzia miaka ya 1990s. Hawa Lowasa na Seif walisemwa na walitaka sana na wamekufa hawajapata uRais wa Tanzania.

Urais wa Tanzania utapewa na Mungu tu kama alivyopata A H Mwinyi (badala ya Salim Ahmed Salim aliyesemwa sana na kupendwa na Nyerere) au B W Mkapa(badala ya Malecela na Kolimba waliosemwa sana). Hata Kikwette alipata mbele ya Fredrick Sumaye na Mwandosya waliokuwa vipenzi vya Mkapa na Magufuli alipata badala Benard Membe na Lowassa ambao waliigawa NEC ya CCM. Mfano wa mwisho ni Rais wa sasa ambaye ameteremshiwa na Mungu tu badala ya JPM aliyetaka kutawala milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…