SoC04 Taifa Moja, Wazo moja na Sauti moja

SoC04 Taifa Moja, Wazo moja na Sauti moja

Tanzania Tuitakayo competition threads

malaika wa zamu

New Member
Joined
Sep 17, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Taifa moja
Tanzania ikiwaza, ikiongea na kusikama kama mtu mmoja nani awezaye kutuzuia?

Tuanze kupiga picha Taifa hilo litaonekanaje, na ungejisikiaje kuwa raia wa Tanzania hiyo, majukumu yako na haki zako zingekuwa zipi?

Wazo moja
Tupo zaidi ya milioni 60 kwa muujibu wa taarifa za sensa ya mwaka 2022, tunawezaje kuwa na wazo moja? Usihofu inawezekana kabisa tukawa na wazo moja ambalo karibia kila mtanzania anakubaliana nalo.

Mfano:Karibia kila mtanzania anakubaliana na wazo kuwa mfumo wa Elimu unahitaji marekebisho, wazo jingine ni Mfumo wa ajira unatakiwa kuboreshwa.

Mawazo kama haya yanatokana na uzoefu wa ujumla katika nchi, kwamba ni mambo ambayo yanamgusa karibia kila mwananchi hivyo kuna mtazamo ambao karibia kila mtu atakuwa nao.

Ni muhimu kuwa na mawazo mazuri kama Taifa, kama vile "Tanzania ni nchi nzuri zaidi Duniani". Wenzetu Wamarekani kwa ujumla wao wanaiona nchi yao kuwa ndio Nchi bora zaidi Duniani.

Kama Taifa kuwa na wazo moja ni jambo litakalotuwezeshaa kufanikiwa katika chochote tutakacho amua.

Sauti moja
Sauti ya kiongozi ikibeba matakwa ya Taifa, Taifa linakuwa na sauti moja, kama viongozi watasema maneno yanayo pingwa na asilimia kubwa ya watu hatutaweza kusimama.

Azimio la Arusha

Hayati Mwalimu J.k. Nyerere alitiongoza kama taifa tukawa na sauti moja.

Maneno yake: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena"

Hii ilikuwa sauti ya karibu kila mtanzania wa wakati huo na wakati huu wa leo.

Na watu wa Taifa moja wakiwa na Tamko moja linalo wapa kusudi la kulitumikia Taifa lao, hakuna nguvu kubwa kama hii.

"Sisi ni matajiri" Hayati Magufuli.

Taifa Moja, Wazo Moja, Sauti Moja.
Azimio la Arusha lilikuwa na muendo wa kisiasa wa ujamaa na kujitegemea.

Je! zama hizi za Leo ambapo Tanzania ina siasa mchangqnyiko za kijamaa na kibepari tunaunganishwa na tamko gani, au wazo gani?

Ujamaa:
Bado mambo mengi yanaendeshwa na serikali, na tuna tamaduni ya kusaidiana kama ndugu.

Ubepari:
Japo tunaukaribisha ubepari kwa kufanya biashara huria na watu wa mataifa mbalimbali bado kama taifa hatuajaukubali ubepari moja kwa moja.

Nini kibadirike sasa?

Kwanza Ujamaa umefanya mazuri katika nchi yetu,Japo kuna changamoto zake amabazo zilipelekea tukakaribisha ubepari nchini mwetu.

Ubepari bado tunauchukulia kama unyonyaji, kama taifa tukiweza kuuchukulia ubepari upande chanya na kuona jinsi ubepari unavyoweza kuleta chachu kwenye uchumi wa nchi yetu.

Serikali iweke mazingira rafiki kwaajiri ya ubepari, hasa kwa kuanza na kutoa Elimu ili tuwaze wazo moja

Mfano swala la bandari ni swala la kibepari (Mwenye mtaji na uwezo wa kuendesha uchumi apewe nafasi) lakini bado mawazo ya kijamaa ( Mali zote za uchumi ziendeshwe na uma) yanasimama katika njia hii.

Kusimama Kama Mtu Mmoja
Utaifa, uzalendo kwa watanzania ni mkubwa sana ukitaka kujua angalia tulivyosimama kama mtu mmoja kumpa mkono SAMATA akiwa Astonvilla.

Tunautaifa mkubwa sana, Hatuna tu nafasi katika mawazo amabayo yanatuhitaji tusimame kama taifa.

Nakuhakikishia Tanzania Tumeshikamana kama fungu la kuni. Na umoja wetu ni nguvu, hii nguvu tunaielekeza kwenye mambo mengine tu, kwa sababu hatujapata Lengo moja.

Nimeuliza mawsali mengi na nimetoa majibu yangu niambie mswahili mwenzangu, Tuna wazo, na sauti moja kama moja?
 
Upvote 1
Tanzania ikiwaza, ikiongea na kusikama kama mtu mmoja nani awezaye kutuzuia?
Hakika hakuna, na taifa linalonia mamoja likiamua jambo jema hata Mungu huweka vema kubwa.
Kwa wanaosali mnakumbuka kisa cha Babeli na ujenzi wa mnara. Amin amin nawaambieni, kilichovurugwa pale sambamba na lugha ni nia zao. Ikitokea tu mmoja anataka wajengee tope na mwingine anataka watumie simenti hapohapo atatokea wa kuiba simenti na tope halafu watajengea mchanga tupu na mnara ubomoke. Kuongea lugha moja ni kunia mamoja ovaa.

Ni muhimu kuwa na mawazo mazuri kama Taifa, kama vile "Tanzania ni nchi nzuri zaidi Duniani". Wenzetu Wamarekani kwa ujumla wao wanaiona nchi yao kuwa ndio Nchi bora zaidi Duniani
Hakika.

Na watu wa Taifa moja wakiwa na Tamko moja linalo wapa kusudi la kulitumikia Taifa lao, hakuna nguvu kubwa kama hii.

"Sisi ni matajiri" Hayati Magufuli.
Aaah we jamaa insha yako, ipo murua sana. Ni kama 'singlehandedly' unawakilisha Tanzania tunayoitaka wote

Nakuhakikishia Tanzania Tumeshikamana kama fungu la kuni. Na umoja wetu ni nguvu, hii nguvu tunaielekeza kwenye mambo mengine tu, kwa sababu hatujapata Lengo moja.

Nimeuliza mawsali mengi na nimetoa majibu yangu niambie mswahili mwenzangu, Tuna wazo, na sauti moja kama moja?
Mi nashauri tu we jamaa wakupe kitengo cha kujenga falsafa na dira ya Taifa, upewe na ulinzi 😁😁😁😁😄.

Kiufupi huo ndio msingi, taifa lolote likitenda kama kiumbe mmoja (as a single organism) hakuna kitakacholizuia kufikia malengo. Na inaanza na kila mmoja kujihisi ni wa taifa na taifa ni lake.
 
Back
Top Bottom