Taifa Stars ibadili mwonekano wa jezi zake

Taifa Stars ibadili mwonekano wa jezi zake

KAPONGO

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Posts
1,688
Reaction score
679
Inashangaza kuona kuwa wakati timu za Mataifa mengine, hata ya Kiafrika, kuja na mwonekano mpya wa jezi za timu zao za Taifa, Taifa Stars imekuwa ikija na jezi za mwonekano huo huo kwa miaka zaidi ya minne mfufulizo.

Inasemekana kuwa TFF ilimpa tenda Kassim Dewji kuivalisha Taifa Stars, lakini sioni mwonekano wa jezi hizo kubalika kila mwaka kama mataifa mengine yanavyofanya, hasa wakati wa mashindano makubwa kama ya Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Afrika.

Nashindwa kupata jibu kwamba tatizo Dewji hana wabunifu, au ni nini kinachosababisha Taifa Star kuonekana katika fashio ile ile ya jezi kwa miaka mingi mfufulizo?.
 
Kumbe huu ukoo wa wadhamini wa Makolo Football Club ndio wamepewa tenda ya timu yetu ya taifa?Ndio maana basi ya hicho unachokisema kuwa hivyo..ni wakati Muafaka sasa wa GSM kupewa tenda hiyo ili Watanzania tujimwayemwaye na jezi bora nzuri na za kuvutia..hizo jezi ndio zinaleta mkosi hadi Msuva anakosa magoli ya wazi kabisa
 
kwani hao wachezaji wanacheza wakiwa Uchi
Tunataka matokeo chanya sio jezi
hii timu inatukosea heshima

Tunaviongozi wanashindwa kusuka mipango ya muda mrefu kuja na timu inayoweza kutufikisha nchi ya maziwa na asali.
 
Mbona zilibuniwa jezi zenye alama kama msalaba mkubwa mbele, wadau wenye imani kinzanifu waka react wakidhani ile alama inatukuza dini isiyo yao. Zile jezi haijulikani zilipelekwa wapi, hata hivyo zilikuwa na muonekano mzuri tofauti na za sasa.
 
Tudiscuss kwanza perfomance..mambo ya kupendeza yaje baada ya sisi kuwa ranks za juu za FIFA na kufuzu tournaments kubwa kama World Cup.
Hii nchi bwana kuna kipindi rais wa tff jamali malinzi, alipendekeza eti inabidi na jina liwe la kutisha kama indomitable lions, simba wa teranga,nalo linasaidia timu pinzani kukuogopa!!!hahaaaa!!kama mpira hakuna hata ujiite MUNGU, watu wanakuja wanachukua point zao tu!!sasa jezi kitu gani?miaka hiyo watu walicheza kifua wazi na walikuwa wanatisha leo unavaa , adidas bado, eti jezi mbaya!!!
 
Kumbe huu ukoo wa wadhamini wa Makolo Football Club ndio wamepewa tenda ya timu yetu ya taifa?Ndio maana basi ya hicho unachokisema kuwa hivyo..ni wakati Muafaka sasa wa GSM kupewa tenda hiyo ili Watanzania tujimwayemwaye na jezi bora nzuri na za kuvutia..hizo jezi ndio zinaleta mkosi hadi Msuva anakosa magoli ya wazi kabisa
Makolo kila wanapoingia wanaharibu
 
Kumbe huu ukoo wa wadhamini wa Makolo Football Club ndio wamepewa tenda ya timu yetu ya taifa?Ndio maana basi ya hicho unachokisema kuwa hivyo..ni wakati Muafaka sasa wa GSM kupewa tenda hiyo ili Watanzania tujimwayemwaye na jezi bora nzuri na za kuvutia..hizo jezi ndio zinaleta mkosi hadi Msuva anakosa magoli ya wazi kabisa
Gsm jezi zake hazijawahi kuleta mafanikio kimataifa mfano return utopolo imeishia Nigeria
 
Back
Top Bottom