Niwapongeze stars Kwa ushindi wa bahati tu
Team imeshinda ila ndo hivo maajabu ya mchezo wa soka. Team dhaifu inaweza kushinda dhidi ya team Bora kabisa
Sisi tusiopumbazwa na ushindi wa ngekewa tunakosowa yafuatayo.
1 Eneo la goal keeper
Sio GK mzuri, hajui kuji position, Haiti mabeki yupo kimya.
Ni dhaifu kwenye kuanzisha mipira. Naiona nafasi ya Manula badala ya Ali Salim
2 Beki Lusajo ni dhaifu mno
Hana nguvu amekata moto mapema. Upande wake ulikuwa uchochoro Kocha aone uwezekano wa kumpa nafasi Paschal Msindo. Napendekeza Kapombe ajumuishwe kwa ajili ya uzoefu.
3. Feisal kafunga goli zuri sawa, lakini hakuwa bora kabisa
Nashauri coach amuanzishe bench
4. Balua kacheza vizuri, lakini imedhihirika yeye bado haya mashindano ya amzidi kiwango
5. Waziri JR, imeonekana daraja lake bado anatakiwa Mbwana Samatta
6. Zimbwe, Baca na Mwamnyeto kazi nzuri ni mabeki Bora kabisa
Nashauri coach awape vijana confidence, wamecheza ovyo, pasi hazifiki.
Physical hawapokei vizuri, waingie gym wafanye tiz la maana
NB: wanasiasa acheni shobo na kiki Kwa Taifa stars, Tunaweza kufuzu bila hamasa zenu fake
PIA SOMA: FT: Guinea 1-2 Taifa Stars | Kufuzu AFCON 2025 | Septemba 10, 2024| Charles Konan Banny Stadium