Taifa stars imeshinda, lakini haikustahili, imecheza ovyo sana

umeandika sawa kabisa,timu imecheza bila plan,haijulikani walikuwa wanafanya nini uwanjani,balua bado sana kuchezea taifa hafai hata chembe,kipa wetu ndio kituko,makocha wetu ni waganga wa kienyeji
 
umeandika sawa kabisa,timu imecheza bila plan,haijulikani walikuwa wanafanya nini uwanjani,balua bado sana kuchezea taifa hafai hata chembe,kipa wetu ndio kituko,makocha wetu ni waganga wa kienyeji
Unajua mpira mkuu
 
Kwa game ya jana taifa staz amestahili kushinda, alikua timu bora uwanjani tangu mwanzo wa mechi sana sana zile dakika zilizofuata baada ya kufungwa goli., wale Guinea ni kama walikua na papara, staz wangetumia vizuri nafasi wangefunga goli nyingi.

Udhaifu wetu mkubwa ni kutengeneza nafasi za kufunga, kuzitumia nafasi chacche tunazopata kwa ufasaha, pia suala la physique ni tatizo sehemu ya kutumia nguvu mara nyingi wachezaji wetu wanapoteza mpira.

Mabeki na viungo wanajitahidi kukinda na kumiliki mpira, tatizo lonaanzia pale kwa namba 10 na washambuliaji wa mbele yake hawana maarifa ya kupata goli
 
Mleta mada uko sahihi kabisa, mchezo uliochezwa na Stars jana wakikutana na timu iliyojiandaa watapigika sana. Kocha asibweteke na ushindi ajue kuna pa kufanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…