Taifa Stars ina shida kubwa ya kiuchezaji kuliko shida za nje ya uwanja

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
1.Tukianza na eneo la beki upande wa kulia Kibwana ni mfupi,vile vile hawezi kupiga krosi na pasi za akili. Siku hizi beki wa pembeni ni mchezaji muhimu sana katika kuandaa mashambulizi.

2.Beki wa kushoto Tshabalala.Nadhani katumika sana na sasa kachoka. Hachezi kwa kuchangamka km zamani. Anahitaji kupumzika.

3.Job anajituma na mguuni mpira upo ila tatizo lake ni ufupi. Suluhu ni kutafuta beki mrefu. Waganda wanaifahamu hii kasoro ndio maana leo wameitumia vizuri mipira ya juu na kupata goli 2 rahisi kabisa.

4. Mwamnyeto kwangu huyu anamakosa mengi zaidi. Kwanza anacheza kazubaaa sana sio beki mgumu. Pili japo ni mrefu lakini haruki mipira ya juu inapita tuu.Tatu anabutua sana mipira bila kuangalia anampa nani.

5. Eneo la katika tuna viungo wanaocheza square basi nyingi. Fei,Mzamiru,mkude,na Sure boy wote si viungo wanaoforce kwenda mbele.

6.Timu haijui kukaba. Yaani tukipoteza mpira timu in inakuwa very disorganized tofauti na wenzetu Waganda. Timu ikopoteza mpira tu ghafla kila mtu anakaa kwenye eneo husika na wanaanza kukaba kwa space na hata man to man.

7. Timu haijui kushambulia. Mikimbio ya wachezaji wetu inatabirika sana. Yaani akiwa na mpira unajua kabisa wapi atapeleka.Pia kujipanga hawajui ndio maana papatu papatu ni nyingi.


Binafsi haya ndo mapungufu machache nilioyaona. Tuendelee na mjadala wa wachezaji wa kigeni.
 
Umekazania ufupi mbona job mfupi anacheza na mwamnyeto mrefu lakini utumbo?

Ifike wakati ongeeni vitu vya maana Martinez pale Man u unamuona mfupi tu na anacheza beki ya kati
 
We timu lazima benchi la ufundi liwe na mtu wa yanga na simba ili kubalance ushabiki.

Tuwekeze kwenye soka 10 year zinatosha kutupa matokeo stahiki
 
kosa la taifa star ni kuchukua watu ambao wamelizika simba na yanga .
bora tukawapiga bench na kuweka vijana wenye nia ili wakodolewe macho na vilabu vikubwa nje na ndani.

hatujifunzi kwa brazil
 

Winga hatari David Richard Ulomi mchezaji wa Moroka Swallows ya South Africa.

Timu alizochezea Al Hillal Sudan, , Dodoma Jiji, Alliance FC ya Mwanza na Ruvu Shooting stars amekataa kabisa kuja kuchezea klabu za Dar es Salaam.

 
13 September 2022



Joshua Ibrahim mchezaji wa Tusker ya Kenya naye ameitwa timu ya Taifa Stars.

Kabla ya kujiunga na timu hiyo ya Kenya alichezea Namungo FC ya Lindi Tanzania.
 
Safi sana huu uchambuzi ni wa kiwango cha SGR,niliwahi kusema haya matatizo ndio yanayoimaliza Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…