TAIFA Stars Ivunjwe na kuundwa upya kama tunataka matokeo Chanya…

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Nimekuwa nikifuatilia michuano ya kombe la COSAFA inayoendelea mpaka sasa kule nchini AFRIKA KUSINI na hasa hasa mechi ambazo timu yetu ya TAIFA STARS (Kilimanjaro Stars) imekuwa ikicheza. Mungu jalia timu yetu imeweza ‘kufurukuta’ mpaka kufikia hatua ya nusu fainali japo kwa ‘mbinde’ na hii imetokana na wapinzani wetu tunaokutana nao ama kutokuwa wamejiandaa vya kutosha au waliamua kutuma vikosi dhaifu kwenye mashindano haya. Nisiwe mnafiki na mtovu wa nidhamu kwa kukosoa tu bila kutoa shukrani,nianze kwa kuwapongeza wachezaji wetu kwa kufikia hatua ya nusu fainali kwani hakuna mtu alitarajia hilo achilia mbali waandaaji wa mashindano waliotualika kama wageni "wachovu" .Nasema wachovu kwa kuwa pamoja na kualikwa ilibidi tupitie mchakato wa kucheza na timu ‘vibonde’ ili kuweza kufuzu hatua ya robo fainali na kukutana na timu kama Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe ambazo zilikuwa mapumzikoni zikisubiri vibonde wa kwenye makundi tutoane (sawa kuna baadhi ya watu watasema wachezaji wetu walichoka saana kutokana na "Fatigue" ya mechi za mfululizo tofauti na timu kama Afrika kusini na wengine tuliowakuta mbele laikini hii haiondoi mapungufu ya msingi yaliyopo kwenye timu yetu kama nitakavyo yaelezea hapo chini).Tuyaache hayo pamoja na kufanikiwa kufika hatua ya nusu fainali na hatimaye kushika nafasi ya tatu baada ya kuwafunga LESOTHO jana kwa mikwaju ya penalty ( kama ungekuwa unaugonjwa "pressure " usingeangalia dk.90 zote au ungekuja kuambiwa baadae mpira umeisha kwa timu zoote kutoka bila kufungana usingeamini, shukrani zimuendee golikipa wa timu ya TAIFA stars aliedaka jana SIO Manura… Kwa kifupi timu yetu imeonyesha kiwango kibovu kupita kiasi pengine cha chini kuliko hata timu tulizozifunga kama Afrika Kusini...Malawi....
Yafuatayo ni mapungufu niliyoyaona na kama hayatafanyiwa kazi basi tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka atakaporudi Mtume au Yesu.
Wachezaji wetu karibia woote (98%) hawaelewi nini wanatakiwa kufanya wanapokuwa uwanjani..hakuna malengo,wachezaji wanapapara mtu akipewaa pasi anaanza kutetemeka kabla ya kupokea mpira ‘by the time’ mpira unapomfikia ‘either’ utamgonga au atatoa pasi butu.
Kadiri wanavyozidi kusogelea lango la wapinzani (kutokana na papara) ndivyo wanavyozidi kupoteza umakini (wasiwasi mwingi).
Stamina ni tatizo kubwa (stamina sio lazima kuwa na mwili mkubwa nieleweke) tatizo la wachezaji wetu mchezaji akifanikiwa kupiga chenga ya kwanza kinachofuata ni kuanguka na mpira mwenyewe (mfano.Msuva, Kapombe na Kichuya) na wengine wengi.
Sikuona mkakati wa mwalimu wakati wa mechi kufanya mabadaliko kadiri mpira unavyobadirika (badiriko wanalolifanya ni kukariri aanze Msuva badae aingie Ulimwengu) au Msuva awe anabadirishana na Kichuya (rotation) kwa wingi ya kushoto na kulia Jambo ambalo mchezaji haitaji kufundushwa na Mwalimu.
Kati ya mambo yaloniumiza saana pamooja na timu kuwa mbovu ni kuona wachezaji ambao wamekuwa wakisifiwa saana kwenye ligi ya Vodacom kwa matarumbeta (Kichuya na msuva) wakionyesha kiwango cha chini kabisa kuanzia katika umiliki wa mpira,kufanya maamuzi (papara nyingi) kutoa pasi bila malengo. N.k...nikajiuliza hivi ndio hawa tunaowasikiaga wamazifunga Yanga na Simba?..Kwa ufupi hali ni mbaya saana kupita kiasi yaani kama ningekuwa napewa nafasi ya kuchagua timu kwa hawa wa sasa ningewatimua woote labda kutokana na changamoto ya mashindano yanayotukabiri kwa sasa hivi karibuni ningewabakiza Maguri,Mkami (kapteni),Yasini, Erasto ,Nyoni, beki number tatu sijui sudi au said, Mbwana Samatta, Ulimwengu (nkimtazama kwa jicho la ndani) na Kipa wa jana sio Manura.
Wadau haya ni maoni yangu kama mdau wa soka anayefuatilia soka kwa siku nyingi natumai wadau mtaniunga mkono japo sio lazima kwa kila mtu kuwa na maoni kama yangu lakini ukweli ndio huo natamani hii makala isomwe na Baraza la Michezo au Waziri wa Miichezo kwa kuwa najua TFF kwa sasa hakuna mtu mwenye ‘moody’na hivi vitu watu wanawaza chakula yao… Mwisho naomba Wizara ifuatilie malipo ya zawadi waliopata wachezaji jana isije ikaishia kulipia mawakili wa Kesi za TFF…
 
Tatizo sio team ya Taifa..shida iko kwa[BManagement.
 
Timu iko poa sema uongozi uliopo haujadhamilia kuijenga timu ukiangalia timu inacheza siyo kwa kutumia maelekezo na elimu anayotoa kocha yaani timu haijawa mseto na hii ni kwa sababu wachezaji hawajakaa muda mrefu wakajuana vyema kiufupi mimi nawapongeza sana hata kwa hatua waliyofikia japo ilitakiwa tubebe ndoo.
 
Mkuu jifunze ku-summarize basi. Si kila mtu anauwezo wa kusoma makala ndefu hivo
 
Mkuu jifunze ku-summarize basi. Si kila mtu anauwezo wa kusoma makala ndefu hivo
Nimekusoma mkuu tatizo nimeandika kwa uchungu saana yaani nisamehe muhinu njumbe umefika...Aisee inatia maumivu ukingalia kiwango cha soka tunachokionyesha...
 
Nshomile, Teacher can teach but students refuse to learn!
 
Mna wachezaji wengine tofauti na hawa tunaowafahamu?

Unapeleka wenye ulemavu wa miguu wakashindane na Usain Bolt ukitegemea ushindi!

Maajabu ya karne haya!
 
Mna wachezaji wengine tofauti na hawa tunaowafahamu?

Unapeleka wenye ulemavu wa miguu wakashindane na Usain Bolt ukitegemea ushindi!

Maajabu ya karne haya!
Wachezaji wapo wengi nadhani tatizo watu wanapotezwa na "majina" makubwa...lakini soka zerooo
 
Tunaojua mpira na kuujua vilivyo tunasema kwamba hakuna Kocha ambaye ametuletea Heshima kubwa kwa sasa kama huyu wa sasa Salum Mayanga na naamini pia hata wale ' Wadau ' hasa wa mpira watakubaliana na Mimi. Wamekuja ' Makocha ' kadhaa hapa kati ila nakumbuka kwa mfano katika FIFA rankings tulikuwa tunacheza kati ya 127 na 134 ila Mayanga kashika Timu kwa takriban mechi 7 au 9 tu tumepanda juzi kutoka nafasi ya 139 na sasa ni wa 114 tena huku tukiwa tumezipita nchi nyingi tu ambazo zinasifika kwa Soka.

Kinachohitajika tu kwa Mayanga na Benchi lake zima la Ufundi ni Yeye kupewa full support na TFF pamoja na Serikali lakini pia na sisi Wadau / Watanzania tumuunge mkono bila kujali Usimba na Uyanga wetu kwani hapa tayari naona kale ' Kaugonjwa ' ketu ' Sugu ' bado kanatutesa ambapo Timu aliposhika Boniface Mkwasa ambaye kiasili ni mwana Yanga FC ' Kindakindaki ' Watu wa Simba walikuwa wanaiponda Taifa Stars na sasa hivi tena Timu ipo chini ya Kocha Salum Mayanga ambaye ni mwana Simba SC ' lia lia ' sasa Watu wa Yanga wanampiga majungu na nina uhakika hata Mleta ' uzi ' piga ua lazima utakuwa ni ' Gongowazi / Kandambili / Chura Churani ' tu ( namaanisha mwana Yanga FC )

Wachezaji siyo wabaya kivile na kama ni mabadiliko ya Kikosi basi yawe very minor ila Kikosi hiki hiki kibaki muda mrefu ili wazoeane kama ambavyo sasa wameshaanza kuelewana, Timu ipate trials games za kutosha ndani na nje ya nchi, nidhamu izingatiwe ndani ya Timu lakini pia Vilabu vyetu nchini vijitahidi kuwa na ' Mfumo ' mmoja wa Uchezaji ambao utaweza kuendana pia na ' Mfumo ' wa Kocha wa Taifa Stars ili kusudi anapowaita tu basi asiwe na Kazi kubwa ya kufundisha. Hili linafanyika sana Netherlands, Spain, Germany na Latin America.

Tukiacha tu ' Upuuzi ' wetu wa Usimba na Uyanga na Siasa ya Vyama vya Siasa kuingizwa mpirani nina uhakika Tanzania tunaweza kufanya ' maajabu ' kwani siyo siri kwamba ' Africa ' hii hakuna nchi ambayo imebarikiwa kuwa na ' Talented ' players kama Tanzania na ndiyo maana wengi wenu leo mnamshangilia na kumsifu sana Lionel Messi anavyocheza wakati kuna Mtu hapa hapa Tanzania anaitwa Abdallah King Kibaden Mputa alikuwa anafanya ' vitu ' zaidi ya hivi tunavyoviona leo kwa Messi huku wengine mkimsifia sana Zinedine Zidane kwa ' mavituz ' yake uwanjani mkiwa mmesahau kuwa Tanzania tulikuwa na Mtu aliyeweza kufanya ' maradufu ' ya Zidane sasa ni Marehemu Hamis Tobius Gaga ' Gagarino '.

Naomba niishie hapa kwani nilipomtaja tu Marehemu Gaga ' machozi ' yameanza kunitoka kwani ' Tanzania ' haitokuja tena kupata ' Fundi ' wa mpira kama Hamis Tobius Gaga. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amen.
 
Nimekusoma mkuu tatizo nimeandika kwa uchungu saana yaani nisamehe muhinu njumbe umefika...Aisee inatia maumivu ukingalia kiwango cha soka tunachokionyesha...
Pole mkuu japo ni pole kwa Watanzania wote.

Unajua soka letu kuna watu walishageuza sehem ya kupigia madili.
 
Wachezaji wapo wengi nadhani tatizo watu wanapotezwa na "majina" makubwa...lakini soka zerooo
mtaalamu maximo alitaka wachezaji waliofit tayari, hasa waliochezea timu zilizokuwa kwenye mashindano ya kimataifa, na wenye urefu wa kutosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…