Taifa Stars, kwanini tunataka kuvuna bila kupanda?

Taifa Stars, kwanini tunataka kuvuna bila kupanda?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kila mara inapocheza Taifa stars huwa nashangaa jinsi watu wazima wenye akili wakiwa busy kusubiri kuvuna sehemu ambapo hatujawahi kupanda kabisa.

Binafsi huwa sifatilii kabisa mechi za stars na huwa sishangai tukifungwa, hata kama tukiweza kubahatisha kwenda AFCON tutaenda kufungwa nyingi na kuleta aibu zaidi.

Mpaka hapo tutakapojifunza kupanda kwa kuanza na timu za Taifa under 17 na under 20...tuwekeze huko makocha wazuri na tuwekeze ziweze kushiriki AFCON under 17 na under 20 au world cup under 17 na under 20.

Tukiweza hayo baada ya miaka michache tutakuja kuvuna mafanikio makubwa stars bila kutumia nguvu nyingi, bila ya hivyo matokeo kama ya Leo yatakuwa kawaida kila siku.

Nchi zote zinazofanikiwa zinaanza chini kabisa... Sisi tunataka tuvune huku hatujapanda kabisa.
 
Leo nimeangalia mtanange kwa muda mfupi tu, nikagundua hata mimi naweza kucheza.

Tunawekeza nguvu kwenye hamasa kuliko uwezo wa wachezaji.
 
Bila kuwa na Academy ni Uongo.

Hii NCHI hakuna kitu inachoweza.

UBABAISHAJI Kila kona
 
Bila kuwa na Academy ni Uongo.

Hii NCHI hakuna kitu inachoweza.

UBABAISHAJI Kila kona
Sio lazima academy tumiliki wenyewe.. tunaweza peleka wachezaji kwenye academy za Ulaya
 
Back
Top Bottom