Taifa Stars wako uwanjani, tuwaombee

Taifa Stars wako uwanjani, tuwaombee

Zinazile

Senior Member
Joined
Sep 11, 2020
Posts
116
Reaction score
126
Habari zenu watanzania wenzangu, jioni hii kuna mechi ya kusaka ticket ya kushiriki AFCON 2023 kati ya Team yetu ya Taifa( Taifa Stars) na team ya Taifa la Niger, mpaka muda huu kila team imepata goli, wawakilishi wetu walikuwa wa kwanza kupata goli kunako dk ya 2 na Niger wakasawazisha baada ya dk kadhaa. Wafungaji wa mabao kwa team zote sijapata bahati ya kujua ni akina nani kwani nasikiliza kwenye radio na nimekuta mechi imeanza hata line up kwa team zote sijasikiliza, kama kuna mtu anajua ni channel gani inaonyesha live anisaidie ili niweze kuangalia.

Naomba watanzania wenzangu tuendelee kuwatakia kheri wawakilishi wetu ili watuwakilishe vema, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars

Up date: Mpira mpaka sasa ni mapumziko team zote zikiwa sawa kwa 1- 1 goli la Taifa Stars likifungwa na George Mpole wakati goli la kusawazisha kwa wenyeji Niger likifungwa na Adebayor

FT : 1-1

Mungu ni mwema tumeambulia point 1 ugenini, ahsanteni kwa maombi
 
Hii timu nayo bhana! Haijawahi kutabirika hata siku moja! Hatuna wachezaji wenye viwango vya juu!

Hatuna professional wengi nje ya nchi! Na hata hao wachache wenyewe, viwango viko chini! Yaani sijui tufanye nini.
 
Pamoja na mapungufu yote bado vijana wanajitahidi kwa kwakweli
 
Pamoja na mapungufu yote bado vijana wanajitahidi kwa kwakweli
Hakuna timu hapa! Miaka nenda timu inategemea wachezaji kutoka Yanga na Simba!

Hakuna mpango wowote ule wa kueleweka wa kuwa na Professional wengi wa kuja kusaidia timu ya Taifa!

Kwa hali hii wacha tu tuendelee kulipokea kombe la dunia na kupiga nalo picha. Maana hakuna namna.
 
Kwa sasa angalu naona kuna mchanganyiko wa wachezaji kutoka timu nyingine japo si kwa uwiaono sawa, hata hivyo hizo timu kubwa za Simba na Yanga ndizo zenye wachezaji angalau wanaoweza kuleta ushindani uwanjani
 
Mpira unekwisha......Taifa stars wamecheza hovyo kabisa
 
Sijui huwa wanajifunza nini kambini, format ya mpira hata haijulikani ni kubutua tuuu
 
Sijui huwa wanajifunza nini kambini, format ya mpira hata haijulikani ni kubutua tuuu
Kwanza ieleweke kwamba muda wa kambini inawezekana kabisa ukawa hautoshi kuwaunganisha pamoja wachezaji, kwani kila mchezaji ana mfumo aliouzoea na timu yake, hivyo kuzoea mfumo unaotumiwa na timu ya Taifa inaweza ikachukua muda na wakajikuta wanaingia uwanjani pasipokuwa na muunganiko mzuri kiufundi
 
Back
Top Bottom