Taifa Stars walipaswa kufikia Segerea

Taifa Stars walipaswa kufikia Segerea

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Nadhani kosa lilifanyika hii timu yetu ikashuka kawaida tu pale JKN airport, serikali kupitia wizara husika wangeandaa ka adhabu kadogo just kuwaamsha wajue kua wanapotumia pesa za walalahoi kwenda kuwakilisha nchi kweli wakaze msuli sio tu labda mpaka waahidiwe gari au mamilioni, hawa madogo siku hizi wanabweteka sana kwa wanaomkumbuka mmoja kati ya watoto wa aliyekua rais wa iraq hayati Sadam Hussein.

Yeye alipenda sana mpira na alisapoti kutoka hata kwenye mfuko wake ili timu ya taifa lake ilete sIfa lakini ilifikia walipokua wakifungwa hivi kwa kweli siku ya kurudi wanakuta karandinga la mahabusu na maaskari wanawasubiria nje ilikua hakuna mjadala ni ndani!!

Kumbe basi ingawa wengi walilaumu njia ile lakini imekua na mafanikio makubwa kwa timu ya taifa la Iraq maana ilijenga nidhamu na uwajibikaji kwa kila sekta kuanzia uteuzi wa timu waalimu upangaji na benchi lote la ufundi leo hii kwa mujibu wa rank za Fifa mwaka 2004 Oktoba Iraq walikua namba 39 ki ubora wa soka duniani! Ni kiwango cha kujisifia ila sasa wamedrop kwani rank za fifa 7 may 2015 wanashika namba 86, Tanzania tungechukua somo hili kama changamoto kwa timu yetu.
 
Nadhani kosa lilifanyika hii timu yetu ikashuka lawaida tu pale jkn airport,serikali kupitia wizara husika wangeandaa ka adhabu kadogo just kuwaamsha wajue kua wanapotumia pesa za walalahoi kwenda kuwakilisha nchi kweli wakaze msuli sio tu labda mpaka waahidiwe gari au mamilioni,hawa madogo siku hizi wanabweteka sana kwa wanaomkumbuka mmoja kati ya watoto wa aliyekua rais wa iraq hayati sadam hussein,yeye alipenda sana mpira na alisapoti kutoka hata kwenye mfuko wake ili timuya taifa lake ilete sofa lkn ilifikia walipokua wakifungwa hivi kwakweli siku ya lurudi wanakuta karandinga la mahabusu na maaskari wanawasubiria nje ilikua hakuna mjadala ni ndani!!kumbe basi ingawa wengi walilaumu njia ile lkn imekua na mafanikio makubwa kwa timu ya taifa la iraq maana ilijenga nidhamu na uwajibikaji kwa kila sekta kuanzia uteuzi wa timu waalimu upangaji na benchi lote la ufundi leo hii kwa rmujibu wa rank za Fifa mwaka 2004 oktoba iraq walikua namba 39 ki ubora wa soka duniani!ni kiwango cha kujisifia ila sasa wamedrop kwani ranl za fifa 7 may 2015 wanashika namba 86,Tanzania tungechukua somo hili kama changamoto kwa timu yetu

""Mpaaka tungekuwa na ile timu ya copa-cocacola ya mwaka 2007 iliyoenda brazil ikarudi na kombe iliendaga wap kqan hyo ndo ilikuw timu
 
wengine ni wauza sura.isitoshe wamezoea kufungwa.kwa hiyo wapo adicted naKICHAPO
 
Wazo zuri sana ndugu mtoa mada, tena kichwa cha thread umekipatia vilivyo. Big up mwamba.
 
Mpira ni sayansi,sisi tunaufanya mpira siasa ndio maana unatushinda. Hakuna mikakati ya timu za vijana,ligi sio bora,TFF viongozi wabovu sana kuriko kipindi chochote cha soka la Tanzania. Pale johannesburg kuna messi wa Tanzania ki umri ni mdogo lakini ana mpira mkubwa sana huwa anakodishwa na kulipw ktk mechi zao za ndondo jozi,tunafungwa hadi na swaziland? Malinzi,, malinzi
 
unajua hawa sasa hivi hawa tangazi taifa.wanatuaibisha.kikwete akivunja bunge na timu ivunjwe octoba tusake wengine huku kuna vipaji mitaani vakutosha
 
Edo kasema Eti Taifa starz icheze Na Liverpool ndo wanalingana kiwango!!
 
Edo kasema Eti Taifa starz icheze Na Liverpool ndo wanalingana kiwango!!

Daah watu wengine tunateseka imagine me Mtanzania mshabiki wa Liverpool Kwa nje na ndani Simba. Msimu mzima maumivu
 
Halafu Malinzi alivyo poyoyo huyu jamaa eti amemuongezea muda kocha Mait Haij wa kuifundisha taifa starz,!!! Kwa kocha huyu tusahau kufuzu kucheza mashindano ya CHAN.
 
😀 ingekua hivyo. Baada ya kichapo wangekua wanatimkia hukohuko
 
Bongo mpira umeingilia na siasa tena wapige kambi huko mwezi mzima
 
Kuna mwaka timu ya taifa ya ivory coast kama sijasahau alikuwa mjeshi wa kuitwa Guel aliwapa wachezaji dola kumi alfu kila mmoja baada ya kueleza matatizo yao akawambia nendeni ila msitoke round ya kwanza.
Walipoenda kucheza ACN wakatolewa first round jamaa waliporudi akaenda kuwapokea airport na kuwatupa ndani tena kwenye kambi ya jeshi
.Bosile boli mchezaji wa zamani wa the elephant ndo akaenda kuwaombea msamaha.
 
Huo ni udikteta! Hatupaswi kutafuta suruhu kwa njia hii
 
Back
Top Bottom