Mkuu nazani hujanielewa hoja yangu ni ipi kwenye soccer la bongo!!
TFF ni taasisi inayojitegemea,inapata rudhuku na pesa za mashindano toka FIFA,CUF na makampuni makubwa kama TBL,Coca cola na serikalini pia!
Hoja yangu ya msingi ni kwa nini TFF wasibuni mbinu mbadala ili waweze kupata pesa zakuweza kuwalipa walau wachezaji wake wa timu ya taifa 1,000,000 kila mwezi??
Mtu una mke,na watoto unaenda kucheza mashindano zen unarudi na laki 500,000 hv hiyo familia utaiendesha vipi? Mchezaji akiumwa hua anatibiwa na nani?? Tumeona pindi wachezaji wanapostaafu kucheza mpira wengi wao hua wezi (Alex Masawe RIP),makondakita( Paul Masanja) wa kwenye mabasi na wengine hata wakiumwa hadi wapate misaada ndo waweze tibiwa hispotalini (Edibily Lunyamila)
Lakini kama mazingira yalikua rafiki kwao wasingeweza kuishi maisha ya tabu kama hayo! Kama Malinzi anaweza kwapua Tshs 880,000,000/= kwa nini wasipewe motisha wachezaji wetu??