Taifa Stars yatua salama yapokelewa kwa shangwe na mashabiki

Taifa Stars yatua salama yapokelewa kwa shangwe na mashabiki

Sasa kuna watu wanaleta siasa kwenye michezo,

Watu wanafuatilia siasa huwa wanajiona kama wao ndo wana mchango mkuuuubwa kwenye maendeleo ya hii nchi [emoji23][emoji23][emoji23] kumbe hamna kitu aiseeeb

Btw, Pongezi nyingi sana kwa Taifa Stars, tuanze mipango ya AFCON sasa
Kama Zitto Kabwe
 
Sasa mzee, ww unaona tumestahili kuwa hapo au ni bahati imetubeba.?
Juhudi na Bahati, lakini unakumbuka jinsi Bara la Afrika lilivyoililia Zambia National Team "KK Eleven" iliyopata ajali huko Gabon? enzi za Omay Bongo
 
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) imetua salama alfajiri ya Septemba 9, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea nchini Algeria kwenye mchezo wa wa kufuzu mashindano ya AFCON 2023 yatakayochezwa mapema mwakani 2024 nchini Ivory Coast.

Katika mchezo huo uliochezwa Septemba 7, 2023, Tanzania na Algeria zilitoka zilitoka sare ya bila kufungana (0-0), matokeo ambayo yanazifanya timu hizo kufuzu michuano hiyo, huku Tanzania ikifuzu kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutua jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo kwa niaba ya Serikali, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono yake kwenye sekta ya michezo, hamasa pamoja na kuunga mkono timu hiyo.

Aidha, amewashukuru Watanzania wote kwa sala, dua na maombi yao na kuiunga mkono timu yao ya Taifa na kusisitiza kutakuwa na utaratibu mzuri kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) hatua itakayowezesha mashabiki waende kwa wingi nchini Ivory Coast mwakani 2024 kwenye michuano hiyo ili kuendelea kupeperusha vyema bendera ya taifa.

"Wizara yetu ambayo inaongozwa na Waziri Mhe. Dkt Damas Ndumbaro itaendelea kuyaishi maono ya Mheshimiwa Rais katika kuiendeleza wa timu ya Taifa na sasa ufadhili na uangalizi utaongezeka zaidi ili Ivory Coast tukafanye vizuri zaidi" amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.View attachment 2743865View attachment 2743866View attachment 2743868View attachment 2743867View attachment 2743869
KESHO LIITISHWE BUNGE LA DHARURA ILI WAENDE BUNGENI
 
Karibuni nyumbani taifa stars. Mumeipa hadhi na heshima nchi yenu Tanzania.
 
Bandari kwanza.

Hatuuzi bandari zetu
Kuhusu bandari tumefikia wapi???

Mbona mnaleta swaga zingine zingine tu! Vipi hapo ikulu wanalisemeaje suala la bandari zetu?
Jazi nyama kidogo mkuu
Huo upmbv [emoji1]

Ova
Ila kuna watu wana muda wa mchezo. Yaani unatoka Kawe hadi Airport kuwashangilia hao kisha unarudi Kawe.
Wakija kupigwa 9 huko kwenye fainali za AFCON mje tena hapa hapa muisifie CCM na huyo mwenyekiti wenu.
Inasikitisha sana, bahati mbaya Mwendazake alikufa Kwa mapenzi yake sio Samia aliyemuua! Pengine angesiliza ushauri wa wadau wa afya tungekuwa naye.

Kingine siasa za wakina Lissu na TEC zimewajengea kidonda cha chuki mnachotembea nacho! Relax maisha ni mafupi acha tusheherekee mafanikio hata kama kidogo. Furahia mafanikio ya wenzako.
 
Kuhusu bandari tumefikia wapi???

Mbona mnaleta swaga zingine zingine tu! Vipi hapo ikulu wanalisemeaje suala la bandari zetu?
Wewe baki na bandari isiyowahusu huku watu wamechapa lapa km zaidi ya 20 kushangilia timu yao.
Waache waenjoy na wewe endelea kuhangaika na bandari isiyokuhusu
 
Inasikitisha sana, bahati mbaya Mwendazake alikufa Kwa mapenzi yake sio Samia aliyemuua! Pengine angesiliza ushauri wa wadau wa afya tungekuwa naye.

Kingine siasa za wakina Lissu na TEC zimewajengea kidonda cha chuki mnachotembea nacho! Relax maisha ni mafupi acha tusheherekee mafanikio hata kama kidogo. Furahia mafanikio ya wenzako.
Huna akili
 
Back
Top Bottom