Taifa staz vs Rwanda: Matokeo

Taifa staz vs Rwanda: Matokeo

Ama kweli shida ndo inayochekwa teh teh teh...!
 
kesho watu watashangilia brazil badala ya starz, kwanini mtu nishangilie hiki kichwa cha mwenda wazimu hadi rwanda wamejifunzia kunyoa....ndo maana mimi nimechoka kuumiza moyo hata huwa sina matumaini yoyote na timu hii. siasa hadi kwenye boli, matokeo zero...
 
Hivi hata sijui walikuwa wanawaza nini kuipanga mechi ya Brazil Jumatatu ilhali wana mechi ngumu tena ya kufuzu for CHAN Jumatatu(hii akili au matope?).....Tamaa ya fedha kitu kibaya sana jamani....Yaani hawa jamaa wa TFF naona mawazo na juhudi zao zote wameelekeza kwenye mechi ya kesho na si hii ya leo..........Kweli wa mwisho ni wa mwisho tu........Inasikitisha sana yaani...Naona hata hao Brazil watatushangaa sana waqksikia tunacheza mechi siku mbili mfululizo....
 
Tumefungwa 1 - 0 ,kwahio tusubiri mechi ya kirafiki na brazil tu.
 
Kama ndo hivyo siendi Taifa kuangalia mpira! Jamani nauza tiketi yangu ya walala hoi ya Tsh 30,000/-, kama hamna mnunuaji, naifanya toilet paper japo ni hard paper. Huu ni upumbavu kabisa, tunawekeza nguvu nyingi kwa mechi ya kirafiki badala ya mechi ya Muhimu. Kama amavubi wametulamba then Brazil watatufanya nini??

Sitaki kwenda kushangilia kufungwa machache, maana tunajua kuwa tutafungwa ila tunaenda kupunguza idadi ya magoli tu! It is so sad, I love my country Tanzania, but I real hate some of my people.
 
mi nimeshangaa hata michuzi kauchuna?
any way hongera serikali ya ccm, maana hata Rwanda wanatujua ingawa kutufunga wametufunga lakini chenga twa wala, na Brazil watatukoma, we subiri kesho.
 
Rwanda inakuwa nchi tishio kubwa sana hapa kwetu; Tanzania tumelala tu.
 
majonzi jamani kutolewa lakini sijui kama walipata mwamko wa kutosha katika mechi hii ya CHAN dhidi ya rwanda
 
So sad..............Tumetolewa!!!!!!!!!!!!!...................Kisa?,mechi ya kirafiki na Brazil..........Tanzania bana

Mkubwa sidhani kama tumetolewa kwa sababu ya Brazil ,kwa kiwango chetu sasa ni sawa kutolewa na Rwanda ambao Kagame aliongoza maelfu ya mashabiki waliongia uwanjani bure kuipa support while huku kwetu tunawekewa kiingilio kikubwa
 
mie nilikuwa wala sijui kama wanacheza na rwanda ghafla tu naona wanaagwa.mechi ya Brazil ilipewa kipa umbele kuliko hii mechi ya kwenda S
udan.
 
hivi brazil wanatakiwa kuja lini? manake nakumbuka walisema tarehe 5 sasa mpaka leo hata media sijaona kuandikia ujio wao na tumewalipa tayari au malipo hayakuwa pamoja na hoteli na chakula ha ha aha ha kuanzia tarehe 5?
 
Starz kuinshinda Rwanda kwao ilikuwa ni ndoto za mchana, hatuko serious katika kila jambo, wale tulikuwa tunawamaliza hapa hapa, sasa kilichotokea tumepigwa 1 oclock.
 
So sad..............Tumetolewa!!!!!!!!!!!!!...................Kisa?,mechi ya kirafiki na Brazil..........Tanzania bana

Kisa siyo mechi ya kirafiki bali ni uwezo wa Maximo kufindisha soka la ushindi ilishagota kikomo na ndo maana akaingia kwenye maigizo na matangazo ya biashara za chapati
 
hivi brazil wanatakiwa kuja lini? manake nakumbuka walisema tarehe 5 sasa mpaka leo hata media sijaona kuandikia ujio wao na tumewalipa tayari au malipo hayakuwa pamoja na hoteli na chakula ha ha aha ha kuanzia tarehe 5?

Brazil wameingia Dar jana usiku
 
kwa nini tusitafute fani zingine jamani?? tuimbeni hata mduara na taarabu kwenye majungu
 
mwaka wa uchaguzi huu kaka !!!!...but ukiacha hilo kama taifa ni vema kujitangaza.....tena nashauri tuweke watu pale wavizie timu zitakazokuwa zinatolewa zifanye stop over Tanzania kujiliwaza kabla ya kurudi makwao...kukabiliana na barua za kufukuzwa kazi kwa makocha wao!!!!

Kama tumefungwa na Rwanda, kisha tukipewa dozi ya kutosha na Brazil, tutakuwa tumetangaza ubora wetu wa kusakata soka au tumetangaza wendawazimu katika soka? Me nadhani tungetumia nguvu kubwa kufuzu mashindano ya CHAN ndio ingekuwa fulsa nzuri na bora ya kujitangaza lakini sio hii. It is total wastage of resources...
 
kwa nini tusitafute fani zingine jamani?? tuimbeni hata mduara na taarabu kwenye majungu
Mkuu naona sasa umeanza kupotea kwani huja wasikia madogo wana piga watu 11,15..umeisikia wapi Historia kama hiyo...wachezaji tulio nao kwa sasa hawakuandaliwa wakiwa madogo.. lkn kwa sera ya sasa iko siku tutafika tu na wala siyo miaka mingi labda tupate akina ndolanga wengine pale TFF..
 
Kama ndo hivyo siendi Taifa kuangalia mpira! Jamani nauza tiketi yangu ya walala hoi ya Tsh 30,000/-, kama hamna mnunuaji, naifanya toilet paper japo ni hard paper. Huu ni upumbavu kabisa, tunawekeza nguvu nyingi kwa mechi ya kirafiki badala ya mechi ya Muhimu. Kama amavubi wametulamba then Brazil watatufanya nini??

Sitaki kwenda kushangilia kufungwa machache, maana tunajua kuwa tutafungwa ila tunaenda kupunguza idadi ya magoli tu! It is so sad, I love my country Tanzania, but I real hate some of my people.
Daaa..... tunaambiwa mlala hoi anaishi chini ya Dola moja leo mlala hoi huyu kamdu kununua ticket ya TZS 30,000, halafu anataka kuifanya toilet paper!? au nikufurahisha jukwaa?
 
Back
Top Bottom