The Farmer
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,658
- 559
Tunaanza na sababu 3:
Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.
Sijaona hiyo article ya Mwanakijiji kwa hivo nitaongea kutokana na kilicholetwa katika hii reply.
Kikwete mwenyewe amesema kwamba 70% ya Watanzania ni bendera kufuata upepo, huyu ndiye rais anayeshabikiwa?
Labda amesema kweli, maana wangekuwa si bendera kufuata upepo wasingemchagua yeye.Hapa kuna hao bendera kufuata upepo na wale wanaolinda/ kutafuta maslahi binafsi kwa kujikomba kwa wakubwa, style iliyowatoa kina Kikwete na Makamba.
Mwandishi anamsifia Kikwete kwamba amepitia tanuru la moto kwa kushindanishwa na magwiji kama vile Tanzania tuna system ya meritocracy na Kikwete kashinda on the merit (merit gani?).Tunajua Tanzania uongozi wa juu haufuati meritocracy, bali kuna Machiavellianism tupu na Kikwete was simply the best courtesant at stabbing his opposition in the back with a dagger and better at obtaining illegal funding.
Ndiyo maana nikasema rais ajaye atakuwa mbaya kuliko Kikwete kwa sababu system yetu haijakaa kum reward mtu mwenye uwezo na track record (meritocracy) ila the best deceiver kama Kikwete.
Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.
TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:
Sababu 102 kwa nini Jakaya Kikwete agombee 2010 na aendelee kuongoza
MWANDISHI WETU
Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?
Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.
Walipofanikiwa kumg'oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng'oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.
Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.
Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.
Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.
Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa "kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano" wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.
Kwa upande mwingine dhana ya utulivu wa kisiasa (political stability) imepitwa na wakati. Wanataaluma na watunga sera, sasa hivi wanazungumzia utulivu utokanao na mkusanyiko wa sababu mbalimbali za maendeleo katika sekta za uchumi na ustawi wa jamii (structural stability). Kwamba watu hawali maneno matupu na nadharia za siasa.
Utulivu kimfumo una nafasi kubwa kutokana na sekta mbalimbali kutegemeana ili kuleta maendeleo yenye ulinganifu, hivyo ni wazi kwamba sera zote zinazotungwa na miradi inayotekelezwa inakuwa imepangwa kimtambuka kiasi kwamba yanayotokea sekta moja yanaathiri maendeleo yatakavyokuwa katika sekta nyingine.
Kwa namna moja au nyingine watanzania walio wengi katika sekta mbalimbali wanaguswa na kufikiwa na miradi ya maendeleo ya kubadilisha maisha yao . Yawezekana kwamba kasi ya maendeleo inazidiana. Lakini kwa namna moja au nyingine kuna mabadiliko ya msingi kule wanapoishi watu.
Watu wasioelewa hali inavyobadilika wanakuwa wa kwanza kupiga mayowe jinsi serikali ilivyoshindwa kuwaletea watu maendeleo, bila kutambua ukweli wa mambo kwamba watu wenyewe ndiyo watajiletea maendeleo na kazi hiyo ndiyo wameshaianza. Kwa waandishi wapiga ramli, kwa sababu wanataka kuonyesha msimamo wao wa "kupinga kila kisemwacho au kufanywa na hasimu wao", wanakuwa na watu wao ambao wanawaumba na kuwatengenezea mazingira.
Wanapoanzia siyo kuonyesha uwezo wa kiongozi wao wa kufikirika bali ni kubuni na kuzua mambo, na kujaribu kugeuza mkondo wa maji utoke ziwani na kupanda mlima. Kwa hili la Kikwete kugombea 2010 tunasema binadamu ana uwezo mkubwa, lakini hawezi kuzuia jua kuchwa!
Katika jamii inayokua kwa misingi ya kidemokrasi wapiga kura na raia kwa ujumla wana nafasi yao katika mchakato wa siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. Nchi inaweza ikawa katika matatizo makubwa ya kiuchumi lakini hakuna matukio ya uvunjivu wa sheria wa makusudi kutoka kwa watu wengi. Tanzania ilipitia vipindi vigumu ambapo uchumi wa nchi ulikuwa mbaya. Hakuna fujo zilizotokea ambao zilitishia usalama wa watu na mali zao.
Kuna sababu 102 ambazo tunaona kwa nini Rais Kikwete agombee Urais 2010. Tutazitolea maelezo machache baadhi ya sababu kila panapokuwa haja.
Tunaanza na sababu 3:
Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.
Hivi sasa ni wazi kwamba nchini Tanzania hakuna mtu anayekuwa juu ya sheria; awe ni raia wa kawaida, kiongozi mkuu serikalini au watendaji wakuu waandamizi. Matukio ya kutaka sheria ichukue mkondo, yako wazi na sasa tunaweza kusema sheria inatawala na watu wanaongoza. Tanzania haitumii utawala kwa sheria.
Rais Kikwete anajali mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu mitatu
Sasa hivi mgawanyo wa madaraka kati ya utawala wa dola, mabaraza ya utungaji sheria na Mahakama uko wazi. Kila mhimili una eneo lake na mipaka yake utawala wa dola unafanya kazi ya utendaji katika mfumo wa dola. Utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama na srikali za mitaa zote ni asasi za mamlaka. Uhuru wa Mahakama ni jambo lisilo la kubishaniwa. Tangu miaka ya 1960 bunge la Tanzania limekuwa linajaribu kuwa muhimili usiothibitiwa. Sasa hivi hilo limewezekana kutokana na Rais Kikwete kujali na kutaka kila mhimili uwe huru kufanya mambo yake na yote kwa maslahi ya taifa.
Rais Kikwete anajali na kutambua ulazima wa utawala bora kwa maendeleo ya taifa Utawala bora ni dhana mpya ambayo imebuniwa katika jitihada za dola kukabiliana na hali mpya inayotokana na matakwa mapya kadri mazingira ndani na nje ya jamii yanavyokuwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Utawala bora una maana ya ushirikishwaji wa wadau na dola kuwa chombo cha kuelekeza matumizi ya raslimali. Na hivyo utawala (bora) ni pamoja na njia zilizo bora za kudhibiti na kuratibu shughuli zinazolenga kuwapa watu uhuru zaidi na uwezo wa kuthibiti mazingira.
Rais Kikwete anathamini mashauriano kati ya wadau juu ya utungaji sera Rais Kikwete anajali usawa wa kijinsia.
Ametunza lengo la kuendeleza sera za kuvutia wawekezaji
Amekubali ushauri wa kufanya mabadiliko katika sera na sheria za madini (kuleta ulinganifu)
Ni kiongozi anayekubali ushauri katika miswada ya serikali inayopelekwa bungeni
Ni kiongozi mwenye kuwa na ubunifu katika utungaji sera za maendeleo mfano mzuri ukiwa ni sera ya Kilimo Kwanza.
Source: TAIFA Tanzania , Desemba 18, 2009
( Mambo yamepamba moto. Nyingine hii nimeinasa kutoka mtandao wa kwanzajamii.com)
Kwenye redhighlights hilo ni swala la kwanza la kutilia maanani.
Secondly,hata kama wadau wengi wanasema JK hafai second term,bado nakubaliana na Mrema kwamba kusema "Hajafanya kitu" ni uonevu,uonevu ambao umetokana na kile wengi wetu wanachokiita "udhaifu" ambao inawezekana udhaifi hu umetokana na jitihada zake za kufanikisha utawala bora ambapo jitihada hizo zinaweza zikawa zimetafsiriwa vibaya....Pengine alitakiwa awe mbabe maana wabongo ndivyo walivyozoea,ukicheka nao wanakuona we ****.
wote mmenena enyi waungwana ila mie nauliza jambo moja tu naomba mnijibu kama kikwete wako wanaomuona hafai kumalizia ngwe yake ya mwisho ya miaka 5 je nani mnaona atatufaa kutuongoza ktk miaka m5 ijayo,naomba mnipe mwangaza ndugu zangu je nani afaa ili tujiandae kumchagua,nijuzeni waungwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?
Sijui hali gani inayoridhisha katika ongezeko la masikini nchini. Sijui ni hali gani inayozungumziwa wakati mfumo wa bei unapaa kila kukicha. Sijui mwandishi anasema nini. Naomba msaada. Tanzania haina mwisho. Kama kuna ramli kama hiyo, mimi siiungi mkono. Ila mwisho au mwanzo wa Tanzania hauna uhusiano na JK kuchaguliwa au kutochaguliwa tena 2010.Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Sioni uhusiano wa waliokosa urais 2005 na kinachosemwa na wananchi kwa wingi wao kuhusu udhaifu wa serikali yao. Waliokosa, wameshakosa. Hata wakifanyaje hawawezi kuwa wameupata urais 2005. Kauli hizi za waliokosa na waliopata ni dhaifu sana, na zina lengo hafifu la kukwepa hoja. Watu wanalalamika jinsi mafisadi wanavyofaidi matunda ya Taifa kinyume na taratibu na kuachiwa huru. Watu wanasema jinsi serikali isiyo na sababu ya kushindwa kutekeleza mambo yake inavyoendelea kushindwa kutekeleza hata yale madogo yanayotekelezeka kwa urahisi. Watu wanavilio visivyosikilizwa na viongozi wao.Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.
Nani aliemng'oa Edward Lowassa? EL aliamua mwenyewe kwa busara zake kuachia mamlaka ya uongozi wa juu wa nchi. Kuna haja ya kuendelea kukumbusha yaliyopelekea kujiuzuru?Walipofanikiwa kumg'oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng'oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.
Hii ni kauli ya kisiasa zaidi ya ukweli.Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.
Nadhani mwandishi anakusudia kutukana wazee wa Taifa bila sababu. Hata hivyo, ni lini JK alimshinda Mkapa katika uchaguzi wowote? Kauli nyingine ya kisiasa yenye nia ya kuchafua zaidi hata kidogo kilichopo.Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.
Kama sio kwa maslahi ya wapambe ni kwa maslahi ya nani? Maana hakuna maslahi kwa mwingine yeyote zaidi ya wale wanaoendelea kuvuna kidogo kilichopo (wapambe).Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.
Ningefaidika zaidi na mifano ya miradi hiyo, kwa maana kama ipo, ni michache sana ukilinganisha na kasi tulioitegemea kwa nchi tulivu.Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa "kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano" wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.
Wananchi wanataka tangible things/services na wala hawahitaji siasa. Mkapa kweli alikuwa mwizi na muuzaji wa raslimali za nchi kwa wageni na yeye kujiuzia mgodi. Kikwete tangu ameingia ni migogoro tu hakuna lolote alilolisimamia na likaonekana. mfano:
Kuna mambo mengi ambayo kikwete kama raisi ameonyesha kushindwa. Halafu kama ni muungwana kwa nini asitangaze kwamba hata gombea ili amuandae mtu mwingine naye ajaribu?? make hii nchi ni ya kujaribia kuongoza/kutawala.
- TRL ni uozo na hapo kashindwa, kwa nini asiige Hugo Chaves
- TICTS ni uozo kwa nini asi wafurushe wale wahuni pale akina karamai?
- Richmond/Dowans ni uozo
- Loliondo amewauzia waarabu na hakuna tamko lolote mpaka waarabu wanakuwa na mawasiliano yao ndani ya nchi yetu, sijui hata JWTZ kama wanajua kazi za vizuri.
- mauaji ya Mbagala, kwa nini asimfukuze waziri wa ulinzi??
- Mauaji ya albino, masha anafanya nini pal wizara ya mambo ya ndani??
Tanzania is no longer an ideological society it is a realistic society! hiyo data ya jk kushinda kishindo was it real au ni ya wizi kutokana na pesa za EPA? If that it is tru kwa utendaji wake can you please mention hata barabara moja yenye km 10 ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ambayo haikuwepo kwenye mpango kazi katika utawala uliopita/
ninyi vibaraka wa Makamba na Rostam, acheni uongo, semeni kweli!!!!!!
Daktari Slaawote mmenena enyi waungwana ila mie nauliza jambo moja tu naomba mnijibu kama kikwete wako wanaomuona hafai kumalizia ngwe yake ya mwisho ya miaka 5 je nani mnaona atatufaa kutuongoza ktk miaka m5 ijayo,naomba mnipe mwangaza ndugu zangu je nani afaa ili tujiandae kumchagua,nijuzeni waungwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Mkuu mimi naamini kuwa JK alishinda kihalali kabisa mwaka 2005. Ila alishinda kwa matarajio mapya na yaliyopuuzwa kabisa na utawala wake. Watu walitegemea kuwa, kwakuwa alikuwa kiongozi wa juu katika serikali mbili zilizopita, kwakuwa alikuwa anachanganyika na watu na kuongea nao kwa uwazi, kwakuwa alikuwa mwenye nguvu na akili timamu na kwa kuwa alikuwa na ahiba, basi angeweza kuwa Rais bora sana kwa nchi yetu. Leo ndio tunajiuliza kama alistahili imani yote hiyo.
TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:
wote mmenena enyi waungwana ila mie nauliza jambo moja tu naomba mnijibu kama kikwete wako wanaomuona hafai kumalizia ngwe yake ya mwisho ya miaka 5 je nani mnaona atatufaa kutuongoza ktk miaka m5 ijayo,naomba mnipe mwangaza ndugu zangu je nani afaa ili tujiandae kumchagua,nijuzeni waungwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.