Taifa Tanzania lapinga sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010!

fmes..
ukitulia huwa unaongea vya maana sana.
 
- Only ukinigusa kwenye masilahi ya taifa!

Respect!

FMEs!


halafu nilitaka kukuuliza..
hili la salim a salim kuwa vice president ndo limekufa
now sasa anahusishwa na kina butiku?
wewe unasikia nini huko ndani?
 
Nafikiri kampeni maalumu imeshaanza kulazimisha mafanikio ya JK. Leo kulikuwa na kipindi maalumu kwenye ITV mahsusi kuimba mafanikio ya JK. Lakini kama mafanikio yapo si uache wananchi wayaone, kwa nini uyapigie upatu kiasi hicho?!
 
halafu nilitaka kukuuliza..
hili la salim a salim kuwa vice president ndo limekufa
now sasa anahusishwa na kina butiku?
wewe unasikia nini huko ndani?

- Dataz huko ndani ni kwamba bado wanajaribu kumpa Urais wa Zanzibar!, Wanaamini kwamba itakuwa ndio dawa ya Pemba na CCM, hasa Muungano!

Respect.


FMEs!
 
Nafikiri kampeni maalumu imeshaanza kulazimisha mafanikio ya JK. Leo kulikuwa na kipindi maalumu kwenye ITV mahsusi kuimba mafanikio ya JK. Lakini kama mafanikio yapo si uache wananchi wayaone, kwa nini uyapigie upatu kiasi hicho?!

Kwa nini anyamaze kama anaona ana mafanikio? Hiyo ndio siasa bana...la sivyo kusingekuwa na haja ya kampeni
 
Lenin aliwaita watu wa design hii (mwandishi wa article) 'Useful Idiot'.
 
Nafikiri kampeni maalumu imeshaanza kulazimisha mafanikio ya JK. Leo kulikuwa na kipindi maalumu kwenye ITV mahsusi kuimba mafanikio ya JK. Lakini kama mafanikio yapo si uache wananchi wayaone, kwa nini uyapigie upatu kiasi hicho?!

- Tatizo ni pale wanaposhindwa kujibu hoja bila personal attacks, hapa sio siri kwamba wamekunwa na hoja 51 za Mwanakijiji, mpaka wamekuja mbio kujibu lakini bado wanadai zimetolewa na mtu asiyekwua na uwezo mkubwa wa kuchambua siasa katika jamii, lakini amekuja kujibu anyways!

- Kule kongamano la Mwalimu Foundation, kiongozi wao akadai wana chuki na wivu tena wa binafsi kwa sababu walikosa urais, wakati wote tunajua kuwa Butiku na Quaresi hawajhawahi kugombea urais, licha ya Mwanakijiji, baba wa kujengea hoja Sitta hayupo tena Mtandao, si unaona wanavyopwaya!

- Sasa wataenda kwa Ruhinda tena na Kisumo! Bwa! ha! ha! yamewafika shingoni!

Respect.


FMEs!
 
Alafu huyu mwalimu mwenzio Prof Mushi alianza na hoja nzuri sana kwa kusema anashangaa wapi tumekosea? maana anasema Tanzania mpaka tunapata uhuru miaka 40 iliyopita tulikuwa sawa na nchi kama Korea kimaendeleo lakini leo wala hata hatuwafuati nyuma bali tuko maili maelfu toka walipo.
Ajabu nimeona hakuendeleza hoja hiyo badala yake akaanza naye kumtetea Kikwete kwamba kazi ya urais ni ngumu.
Shit! hivi kama kazi ya urais ni ngumu nani alimwambia agombee na kutupatia ahadi za uongo?
Sikuona ajabu yule mama Shelukindo kumtetea kikwete maana alikuwa pia mwana mtandao. Wala sikuona shaka Sendeka kutetea maslahi ya chama chake.
Katika yote waliyozungumza hakuna hata mmoja aliyetoa point nzuri ya kutuonyesha tutavuka vipi mbali na kushambulia watu wanaomlalamikia Kikwete kwa kutochukua maamuzi mazito.
Chua naye leo kwa hali isiyokuwa ya kawaida hakuweka nafasi ya wasikilizaji kuporomosha maswali badala yake katuwekea one sided mahojiano. Sijui naye sasa amenyweshwa ya kijani? Mungu wangu tusaidie Tanzania. Ondoa hii takataka yote!
 
Na kwa kujua kuwa ni pumba alizoandika na ili asichekwe kaamua kutoandika jina lake.
MMkjj huwa anaweka id yake pale na wao waweke basi.
 
Nafikiri kampeni maalumu imeshaanza kulazimisha mafanikio ya JK. Leo kulikuwa na kipindi maalumu kwenye ITV mahsusi kuimba mafanikio ya JK. Lakini kama mafanikio yapo si uache wananchi wayaone, kwa nini uyapigie upatu kiasi hicho?!

Mwalimu, hapa umeteleza,

Serikali iliyoko madarakani ina haki ya kusema yale iliyotekeleza, na wapinzani wana haki kusema yale ambayo hayakutekelezwa. Then Mwananchi ataamua mwenyewe nani mkweli.


Ati serikali isiambiwe wananchi wake imefanya jambo mahali ... aliyeko Mbeya ajue ya Bukoba bila kuhabarishwa ni upotoshaji wa habari mkubwa sana.
 
Unaposema tangu 2005 Kikwete alipoingia madarakani mambo mengi yamefanyika na miradi mingi imetekelezeka bila kuwa more specific ni kujidanganya. Mwanakijiji katika makala yake alieleza very specifically mambo ambayo Kikwete has been a let down mfano, serikali yake kushindwa kutekeleza mapendekezo ya bunge, kutoshughulikia ipasavyo watuhumiwa wa EPA, KAGODA etc. Nilidhani angekuwa more specific ili tuweze kujua mazuri ya Kikwete, he has not done so...!!!for reasons only known to himself...
 
CCM watampendekeza kuwa mgombea wao, then our duty ni kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutomchagua kwa kuweka scientific reasons zenye data badala ya vague statement wanazosema wao, kuna statistics nyingi za kuonyesha kuwa kikwete hatufai, lakini wao watakuja na vague statements na kibaya zaidi kwenye nafasi mbaya zaidi kwani wao wanamiliki vyombo vyahabari.

Pamoja na hayo tunatakiwa kuweka masirahi ya Taifa mbele hasa sisi tunaojadili hapa, mtu unaona kabisa hapa Rais amekosea lakini unamchagua kwa kuwa ww unatekeleza ibara ya 15 ya katiba ya CCM, that is not fair kwa Taifa lako, wazazi wako na ndugu zako wanaoitaji maendeleo ya nchi kuliko ww unayeangalia maendeleo ya mfuko wako

Wana JF charity begins at home, wanachama wa CCM hapa ndio mnatakiwa kuwa wa kwanza kuadvocaye changes kwenye chama chetu kitukufu kwa kuwaadabisha viongozi wetu ambao hawawezi kutekeleza majukumu yao, tuseme ukweli na kuwambia kuwa hawawezi kuwajibika na ikinidi tuwawajibishe kwa njia sahii

Kwenye mambo ya biashara kuna kitu kinaitwa cannibalization, kama huwezi kuwa creative enough na kutumia opportunities zinazojitokeza kwenye environment, then competitor watakucanibalize, then tunachokiiona hapa cha vyama vya upinzani kuja na ufisadi wa CCM kila siku ni kwa sababu CCM imeshindwa kusoma harama za nyakati na inakumbana na environmental punishment

Siku zote jipu linaanza kama kipele, haiwezekani jipu likaanza na ukubwa wake, CCM then jipu limeanza kama mnasubiri liive mjue rangi ya usaa subirini kama mnatafuta njia sahihi ya kuakikisha jipu haliendelei, Kikwete may not be the right person to drive you out of problems
 
kuna msemo mmoja niliupata kwenye filamu fulani usemao...its not about who does what,what matters is how well one does the job..so kwenye swala la JK kupewa nafasi ya kugombea uraisi tena mm binafsi naunga mkono kupinga mana ameonyesha efficiency ni dhahifu,mm sina shida nani apewe ila how well can that person do the job,ahata kama mtampa nchi mwanakijiji well and good muimu ni output
 
Hata zije sababu 10001 za kumsapoti.
Je macho hayaoni ukweli??
 
Hakika uko sahihi kabisa! Tunahitaji mfumo huo unaotoa mwianya ya watu wenye uweza halisia kupewa nafasi za kugombea hadi hatua ya mwisho kabia. Huko CCM kuna vitu ambavyo hufanyika katika uteuzi wa mgombea Urais hakika haviwatendei haki wananchi, maana vyovyote vile mtu akijitokeza kugombea lakini anasifa zinazofaa kabisa kwa mjibu ya uzoefu wake wa utendaji kwa kufuata taratibu, sheria na uwezo binafsi hao hutupiwa vilago kwa kuambiwa ondoa jina lako! Tunakumbuka kwa mfano Mzee Malecela alivyofanyiwa kwa mara kadhaa na huo ni mfano mmoja tu!

Hivyo binafsi nakupongeza kwa uchambuzi wako huo mfupi juu ya kuelezea majibu ya hawa jamaa tusiowafahamu. Kwanza ni wababaishaji tu fulani hawa. Thread ya M. M. Mwkjj iltolewa siyo siku nyingi zilizopita na kwa maana hiyo, leo isingewezekana watu milioni 4 kuwa walishayafanyia kazi mapendezezo yaliyotolewa kwenye kipindi kifupi kama hiki na kuweza kutoa majibu yao. Huyu ni mtu mmoja tu amekaa ama na mwenzake wakaandika kwa kusema watanzania milioni 4.

Tuache ubabaishaji katika masuala ya msingi, masuala yanayotujengea uwezo kama jamii, halafu mtu fulani anaingiza hoja yake ya uongo na kusema ni ya watu milioni 4. Namshauri ajitambulishe kama mtu na siyo kuja kwa mgongo wa kundi. Hata hivyo bado hoja zake ni dhaifu. Maana CCM haijawahi kuwa na tanuru lolote linalopia viongozi wa dhati kama siyo ushabiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…