Taifa teule na mataifa

Mshana Jr

Dunia imeanza kudanganywa tangu karne ya pili baada ya wasomi wa mwanzo kuanza kuitumia katika maslahi yao..........(nimechoka usingizi nashindwa kunyumbua vyema)


Lakini la msingi tambua watu wametanguliza maslahi zaidi na kisha wengine wakajitengenezea madhehebu yao wenyewe na kuuzaa ukiristo.....


Kristo = Mtu mpakwa mafuta au aliyewekwa Mfu kwa kuhani.

Vingi tunadanganywa

Angalia leo hata mpagani anasherehekea sikukuu yake na kuiita siku ya kufufuka kristo
Hivi pasaka ni jina la mtu eeh!!?

Jiulize

Leo wangeachwa watu mashariki ya kati wasambaze uislam duniani mataifa ya magaribi yangelikuwa na nguvu za sasa?!

Tizama nguvu kubwa ya kushabikia 25 Dec duniani na nguvu ya Ramadan duniani

Afu tena kaa jiulize

Je, kuna Mtume yoyote alizaliwa au kuishi Italy?

Je, kuna Mtume yoyote alizaliwa au kuishi Germany?

Je, kuna Mtume yoyote alizaliwa au kuishi England?

Je, kuna Mtume yoyote alizaliwa au kuishi Marekani?

(usingizi nashindwa hata kufafanua vyema kesho kukikuchwa vyema tuangalie uhalali wetu na umiliki wa bustani ya edeni na siri hasa ya bonde la ufa afu tujiulize je bado hatuko tayari kusimamia historia ya kweli na mwanzo wa chimbuko la dini yetu?!")

zitto junior hearly
 
Na kama kuna watu wanamkataa yesu kwa nguvu zote Duniani basi ni waisrael wale Jewish. Sijui kwanini bado wanaqualify kuwa taifa teule then watu wa pale Mbeya waliokoka mkoa mzima wanakuwa watu wa mataifa? Inanivuruga kichwa hii!

Its injustice!
hahahh et mbeya mkoa mzima wameokoka

me nliishi mbeya mwaka na nusu lkn ckuwah bahatika kuona msikiti
 
Nimecheki ni kweli sijaona ila kuna andiko lianataja China ama mashariki ya mbali... Kitu kama hicho.....
Kuwa na hakika na kitu ama uliza Kama umesahau au umetatizika kuhusu jambo

Kumbuka watakuja watu kuuliza hiko kitu na ukawa huna majibu ya msingi utaibua hoja msigano ndani ya uzi wako mzuri na tukajikuta tuna hama kwenye mada husika

Hope umeelewa na umejua ulipoteleza
 
Naamini ndio hili andiko nililochanganya asante kwa ufafanuzi huu
 
Asante sana kuna kona nyingi umegusia hapo... Zitahitaji uchambuzi wetu wenyewe bila kutegemea wala kuegemea mabandiko na vyanzo vya wazungu...
CC : Che mittoga
 
Asante hata kwa ufafanuzi ule pia... Nimekuwa mkweli kwamba kuna mahali nilitatizika
 
Huu uzi unavutia sana comments zake , naomba niwe mpenzi msomaji tu. Jamii forum kisima cha Maarifa
 
Mkuu Mshana Jr kwa maoni yangu kwa reference ya bible/apocrypha na vitabu vya kiyahudi... Ni kwamba baada ya gharika tunaona dunia nzima yaani familia ya Nuhu ilikuwa inamuabudu Mungu mmoja ila baadae alipokuja wasumeria wakaanza ibada za masanamu huko shinar chini ya mfalme Nimrod ambaye aliweza kushawishi koo za Ham na Japhet kumfuata ila ukoo wa shem pekee ndio baadhi walibaku kumuabudu Mungu

Sasa Mungu akajinasibisha kupitia shem baada ya mnara wa babeli maana dunia nzima ilishaanza kuabudu masanamu..... Kupitia shem ndipo Abraham anazaliwa na anaishi kwenye pango kwa shem na kufundishwa habari za MUNGU wa kweli na alipotoka hapo aliweza kusimama katika imani na hilo likapelekea Mungu kuendelea kujitambulisha dunia kupitia ukoo wa SHEM na hilo likaendelea hadi Abraham then Yakobo mpaka Israel iliyofuata

HOWEVER baada ya wayahudi kumkana Mungu na kuanza kufanya waliyokatazwa Mungu akawalaani na kuwapa hukumu ikiwemo kuwatawanya duniani.... Kwenda utumwani na kushambuliwa na magonjwa kibao hivyo baada ya Israel kufanya uasi Mungu akaendeleza agano na abraham ila kulingana na maandiko wote wenye imani kwa Mungu wanakuwa uzao wa abraham by default na Yesu alipigilia msumari wa mwisho maana alileta wokovu kwa mataifa yote hivyo wanadamu wote tumekuwa taifa teule sio israel tena maana leo hii Mungu anaabudiwa dunia nzima tofauti na enzi hizo kila nchi ilikuwa na ibada zake na miungu yake

So kwa maoni yangu wanadamu wote tumekuwa taifa teule ila Israel ni mambo ya agano la kale tu na unabii wa siku za mwisho ila wote tupo sawa sasa na waisrael wanaofanya maasi na kutesa watu huko palestina wataonja moto wa jehanum kama kawaida unless na wenyewe wamrudie MUNGU wa kweli

Ni hayo tu

Labda niite wataalam wa historia na maandiko waje wanirekebishe ili tujifunze zaidi

Cc Malcom Lumumba tikakami wa lopelope chabuso blackstarline popbwinyo hearly
 
@zitto junior uko vizuri sana mtaa huu na historia ya dunia kiimani kupitia misahafu unaijua vema! Kudos brother [emoji106] [emoji115]
 
Kwahiyo mkuu ht mweusi akikaa sana hizo nchi anakua mzungu ee au?..nipe elimu kdgo
 
Rangi ya mzungu unaijua mkuu?!..so what about waarabu na hiyo baridi?!
 
Shukrani mkuu hizi ndio mada za kujifunza sana although mie nikijiuliza wanasali/swali wakasema wameona muhammad/yesu kawatokea je wanaweza kutupa ushuhuda kuwa hao waliowaona ni kabila/race/rangi gani?!!..mzungu,mwarabu au mweusi?!
 
Sawa Mkuu,sote tuko sawa kwa Mungu,isipokuwa Bani Israel wao walichaguliwa kama binaadamu wa kusambaza yale aliyoyataka Mungu,yaani kuabudu Mungu mmoja na kufuata sharia zake..

Mapenzi ya Mungu kwa Bani Israel,na ule uteule aliowapa wa kusambaza aliyoyaamuru kayaondoa kwasababu hawa jamaa wameshindwa kuyafanya yale anayoyataka Mungu,Hawa jamaa wamelaaniwa,hakuna hata Mtume mmoja walioletewa wakamkubali…

Baada ya kumkana Musa,Bani Israel(Wayahudi) walikuwa wanasubii Masaya(Kristo kwa lugha ya kigiriki),Mungu akawaletea Masaya(Yesu aka Isa aka Iso aka Yoshua aka Jesus) lakini hata hivyo wakamkejeli na kumsulubu Msalabani..

Kuna watanzania humu JF wanafikiri dini ya kiyahudi(Hebrew) inamkubali Yesu(Isa) lakini hawajui kuwa Wayahudi wa kale na hawa wa sasa hawana habari kabisa na Yesu kwao wao wanamuona Yesu tapeli,mzushi tu..

Kutokana na Kukataa na kuwakejeli Mitume,Mungu kaahidi kwenye Quran kuwa,wale wataowakejeli na kuwakataa Mitume atawaondoa na kuwachagua Wengine,Mungu kamleta Muhamad ambae ni mtume pekee ambae sio Myahudi,Muhamad kafundisha yale yale aliyoyaleta Musa sema akasawazisha mengine na kuzidisha yale yaliokuwa hayajamaliza kuyafundisha Isa(Yesu)...
 
Swadakta kwa asilimia 100% na hili halina shaka...na watu wengi wamekuwa wagumu sana kulielewa hili hasa huku Africa..
 
Shukrani mkuu hizi ndio mada za kujifunza sana although mie nikijiuliza wanasali/swali wakasema wameona muhammad/yesu kawatokea je wanaweza kutupa ushuhuda kuwa hao waliowaona ni kabila/race/rangi gani?!!..mzungu,mwarabu au mweusi?!
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…