Taifa teule na mataifa

Nimesoma kwa umakini sana post yako mshana jr, ila kuna jambo pia naomba niulize na najua litakuwa nje ya maada kuhusu israel ningependa niulize humu.

Kule instagram kuna page ya state of israel naifollow Israel (@stateofisrael) • Instagram photos and videos

iko verified na ig ila nilichoshangaa sana ni kuwa wanapromote sana ushoga, kiasi kuwa baadhi ya followers wake toka nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakihoji kuhusu kitendo cha taifa teule kama israel kupromote ushoga kiasi hicho tena kwa kuandika SHABBAT SHALOM


Sasa kama taifa teule linafanya hivyo, ni wapi tunaelekea, ni kwanini wanafanya hivyo ili hali nchi mbalimbali za kikristo zinaliheshimu sana taifa hilo kuwa ni taifa teule la Mungu.
 

30 Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;

31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.

32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
 
Ilikuwaje miungu ya Tanzania ishindwe na Mungu wa israel? Si tungetambika kupitia miungu yetu na kupata uwezo wa kuitwala dunia na miungu yetu ikaabudiwa na wanadamu wengine wote duniani. Hilo tu la Bismack ungetakiwa ujiulize nani kalaani miungu yetu na sisi wenyewe. Nimependa huu mchango wako wa vikoba...imependeza.

 
Nashukuru mkuu kwa kunirekebisha hapo kwa mistari iliyoshiba kabisa ila mimi hoja yangu sio kupinga kuwa Israel haina ahadi za Abraham ila nachosema ni kuwa ule UTEULE sio wa kwao tu tena kama hapo zamani ila sasa UTEULE umekuwa kwa wote wanaomcha Mungu ikimaanisha waisrael wamekuwa sawa na mataifa mengine yote as long as yakimfuata Mungu wa kweli


Wagalatia 3
6
Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa
.

..........

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Je hapa Biblia haikumaanisha Uteule wote wa Abraham na baraka zake zimeshakwenda kwa mataifa yote ambayo yatamkubali kristo ikiwemo Tanzania na mataifa mengineyo??? Hivyo kama wote tumerithi hizo baraka uteule wa israel si umekomea hapo au labda niseme uteule wa israel umeongezwa wafuasi hivyo nikimaanisha waliomfuata MUNGU wa kweli wote wamehakuwa sehemu ya taifa teule hivyo hakuna special tena kuhusu ISRAEL

Labda unieleweshe vzuri maana nakiri bado najifunza kuhusiana na maandiko

Cc tikakami wa lopelope
 
Ila pia kuna sehemu Yesu alikuwa anaombwa na mama fulani amponye binti yake na Yesu kwakujua siyo myahudi alikuwa anampotezea mpaka wanafunzi wake wakamwambia mtimizie haja yake huyu mama ila yeye akajibu kuwa HUWEZI KUMPA MBWA CHAKULA CHA WATOTO naye mama hakajibu kuwa hata mbwa wanakula makombo ya bwana zao chini ya meza, naye kwakuona imani ya yule mama akamtimizia haja zake za kumponya binti yake kwakusema sijapata ona mtu mwenye imani kama wewe

hapo unaona kuwa anasema ametuma kwa taifa la wayahudi sio kwawote ingawa pia kuna mifano mingine ile ya harusi na waalikwa kukusanywa katika njia panda inakuwa contradicted na maneno aliyosema hapo juu, hapo ndio unaona biblia ni msitu mnene
 
Yesu alisema "yeye ni njia ya kweli na uzima" yesu alibatizwa vipi issa nae alipatizwa? Yesu alisulubiwa msalabani na kufa siku ya tatu alifufuka. Yesu alizaliwa kwenye hori la ng'ombe Issa alizaliwa chini ya mtende!! Kwakifupi Issa siyo Yesu. "Kweli itakuweka huru".
 

Naomba nieleweshe Yesu alizaliwa vp na mama yake ni nani
 
Biblia ni historia ya waisrael na Mungu wao. kila sehemu wana mungu wao na jinsi ya kumwabudu. issue inakuja jee Mungu ni mmoja wa wakristo,waislam, africa...
 

Hakufa na wala hakusulubiwa...Mwenyezi Mungu alimpaisha na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu...jambo unaloliona wewe ni gumu na haliingii akilini basi kwake ni kitu chepesi mno.
 
Mkuu zitto jr asante ni mara ya pili una ni mention. Hili suala nita hitaji muda kulifuatia ilinije na mistari ya Biblia kusurpport hayo nitakayo ya leta hapa. Mistari mingine tayari imo humu kwenye hii thread. Ila agano la Mungu na Abraham na mjukuu wake Jacob/Israel lita simama milele. Ni kiamini kwa msaada wa Mungu tunaendelea kukomaa katika hii mijadala ya kiimani humu jF.


 
Hakufa na wala hakusulubiwa...Mwenyezi Mungu alimpaisha na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu...jambo unaloliona wewe ni gumu na haliingii akilini basi kwake ni kitu chepesi mno.

Unaona sasa siku zote na jua kuwa Makka au Madina kuna kaburi la Mtume SAW. Naomba basi nielezee siku zake za mwisho hapa duniani zilivyo kuwa na mashuhuda walio zishudia pengine na kwa faida ya wengine humu.

Siku ya hukumu ya mwisho yeye atakuwa wapi? Maana kwa mujibu wa Biblia siku ya hukumu ni shurti kila goti la mwanadamu lipigwe mbele yake kwa ajili ya hukumu ya haki. Sasa sitaki kuamini kuwa Mtume Muhamed SAW si mwanadamu aliye umbwa Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote (Bwana Yesu).
 
Vp zile pua za kizungu na wahindi?
 
Mkuu nakuunga mkono but Issa siyo yesu jaribu kuelewa.
Mkuu hata mimi nakuunga mkono yesu sio Issa bin Maryam kwa kuwa yesu alisulubiwa na Issa A.S hakusulubiwa na pia inawezekana yesu alikuja na kitabu cha biblia lakini Issa alikuja na kitabu cha Injili you are correct
 
Kuna mambo mengi yanachanganya sana kuhusu Israel
Mema na mabaya
Mazuri na ya kutisha
Ya msaada na ya ukatili
Ya akili nyingi na ya ujinga pia
 
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

Bibilia haijasaza kitu
hii kitu hujaweka vizuri mstari wake nimeipenda hii
 
ni
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

Bibilia haijasaza kitu
meiona imetoka wapi
 
hi
hilo jina tanzania tu ni la miungu ya kigeni sina uhakika na tanzania ni muhindi mmoja ndo alishinda hilo shindano la kutafuta jina.
hivyo mwisho wa siku tuendelee kukubali MUNGU wao wanayemtegemea wayahudi ni wakweli nasi tumekubali kumpokea na kufuata kwa kuwa ziko shuhuda mbalimbali kwao na mifano iko mingi daniel 6:16, 2wafalme6:18 na nyingine nyingi.
ila hii haiondoi uhalali wa kutetea yaliyo mazuri yetu ikiwa ni pamoja na historia zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…