Taiwan iko kwenye hatari ya kuingizwa mkenge ikawa kama mikono na damu itakayotumiwa na Marekani kujaribu kuidhoofisha China Kijeshi na kiuchumi!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Marekani iko katika vita ya kiuchumi na kijeshi na China lakini haiko tayari kutumia mikono na damu ya Wamarekani, kama ilivyokuwa kwenye vita ya kiuchumi na kijeshi na Urusi lakini haikuwa tayari kutumia mikono na damu ya Wamarekani.

Kama ambavyo Ukraine iliingizwa mkenge ikajikuta katika mdomo wa Urusi, lengo likiwa ni kuidhoofisha Urusi kijeshi na kiuchumi, hali kadhalika si ajabu Taiwan inaweza kuingizwa mkenge ikajikuta iko kwenye mdomo wa China!!

Ili kufanikisha malengo yake iko tayari kutoa silaha na pesa zote zinazohitajika ili zitumiwe na mikono na damu ya wengine! Ila kibaya ni kuwa hizi silaha na pesa si za bure!! ni mkopo nwa muda mrefu na lazima urudishwe na riba juu. Marekani wako mkwenye biashara!! Ndio maana marekani inaipa Ukraine silaha na pesa kama haina akili nzuri vile lakini hizo pesa zitarudi na faida juu!! Lakini ukraine imepoteza maefu ya askari na raia na sehemu kubwa ya ardhi yake imekaliwa na Urusi jumla!!

Marekani haiwezi kuihurumia Taiwan itakapopigwa na China ili mradi tu malengo ya kuidhoofisha China kiuchumi na kijeshi yatakuwa yanafikiwa!! Ndio maana Marekani inaumia sana kuona Uchumi wa Urusi haujaathirika kivile kama ilivyotarajia. Lakini kilichoiokoa Urusi ni kuwa na mali asili ambazo zinategemewa sana duniani na hazina mbadala kwa urahisi. Tofauti na China, yenyewe China inategemea zaidi kuuza bidhaa ambazo zinaweza kuwa na mbadala kwa urahisi!
 
Neno kiuchumi futa. Ni dhambi kuipambanisha US na nchi yoyote kiuchumi, hasa hapo ulipomtaja US kupambana kijeshi na kiuchumi dhidi ya Russia.
 
Google yao, na hizo valid economy statistics data za USA unazipata kupitia huo mtendao wao, washindwe vipi kupika takwimu feki za usupapawa wa mchongo kiuchumi?
 
Kwanini china asitengeneze hizo sites zake?

Pia unataka kusema kuwa hizo takwimu zinapikwa? China kamuacha mbali kiuchumi US?
 
Google yao, na hizo valid economy statistics data za USA unazipata kupitia huo mtendao wao, washindwe vipi kupika takwimu feki za usupapawa wa mchongo kiuchumi?
Takwimu za dunia huwezi kupika, ndo maana Forex ni soko la west ila Rubble ilipanda juu sana na hawawezi kufanya chochote, nchi za kidemokrasia huwez kupika data, nchi za kidictator ndo data hupika
 
Kobazi mu watu wa hovyo sana.. halafu cha ajabu dream yenu wote ni kuzamia US.
 
Takwimu za dunia huwezi kupika, ndo maana Forex ni soko la west ila Rubble ilipanda juu sana na hawawezi kufanya chochote, nchi za kidemokrasia huwez kupika data, nchi za kidictator ndo data hupika
Kama KAYAFA aisee jamaa alikuwa mwongo shetani anasubiri.
 
Takwimu za dunia huwezi kupika, ndo maana Forex ni soko la west ila Rubble ilipanda juu sana na hawawezi kufanya chochote, nchi za kidemokrasia huwez kupika data, nchi za kidictator ndo data hupika

Cheki kiazi huyu
 
Naona mrusi umeamua kuleta Uzi wa kujifariji ,sema nyie si wanywaji ningekupa k-vant kubwa maana aibu ya leo siyo ya kitoto
 
Neno kiuchumi futa. Ni dhambi kuipambanisha US na nchi yoyote kiuchumi, hasa hapo ulipomtaja US kupambana kijeshi na kiuchumi dhidi ya Russia.
Ukiwa na nguvu kiuchumi si Kwamba hushindani na wale walio dhoofu kihali. Wenye nafuu Kama Russia lazima upambane nao wasifurukute na ndio maana Us hujaribu kuweka vikwazo kwa kill ambaye anagusa maslahi yake.
Ishu ya Iran China na Russia tumeona hapo nyuma

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom