tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kwa mujibu wa nguli wa muziki wa dansi nchini, marehemu Remy Ongalla, muziki ni burudani, furaha, huzuni, nk. Hapa anamaanisha kuwa muziki ni kila kitu.
Hakuna binadamu aliyekamilika asiyependa kusikiliza au kucheza muziki. Pamoja upenzi wa muziki, kila mtu ana aina fulani ya muziki asioupenda hata kidogo.
Binafsi siupendi katu muziki wa bongofleva kwa sababu mbalimbali. Kwanza muziku huu hauna maadili yoyote bali umejaa matusi na ushabiki wa mambo ya ovyo kama vile ngono, bangi, uhalifu, uvunjivu wa amani na kila aina ya ghasia.
Pili, muziki huu hauna mpangilio mzuri wa mahadhi (melody) ukiachilia mbali jinsi waimbaji wake wanavyoimba kwa kubana pua na kuhemea juu juu.
Tatu, muziku huu unatukuza ngono 100%. Nyimbo za bongofleva zinazohamasisha uzalendo, uwajibikaji, maendeleo na utu hazizidi 10 tangu muziki huu ulipoasisiwa hapa nchini zaidi ya miongo miwlili iliyopita.
Wakati nikuwa safarini kwenye basi ya abiria huwa napata taabu na aibu kubwa sana, hasa ninapokuwa nasafiri na watoto wangu au watu wa heshima. Unakuta safari nzima tangu Dar hadi Karagwe zinapigwa vudeo za bongofleva zenye maudhui ya matusi tupu huku mabinti wakiwa uchi wakishikwashikwa makalio na wavulana.
Pia wakati fulani nikihitaji kusikiliza redio napata taabu sana pale ninapotafuta stesheni lakini najikuta stesheni zote zinapiga nyimbo za bongofleva. Inabidi tu nizime redio nisubiri DW na BBC watakapokuwa hewani nisikilize. Ni shida sana kwa kweli.
Aina nyingine ya muziku ambao hauiingii akilini mwangu ni muziki wa taarabu. Kama ilivyo kwa bongofleva, muziku huu umejaa vichambo, masengenyo, masuto na upumbavu mwingine kama huo.
Kusema kweli nikisikia wimbo wa bongofleva au taarabu unapigwa, nahisi kutapika. Yaani najisikia kichefuchefu kabisa kama mwanamke mwenye mimba changa.
Je, ni aina gani ya muziki ambao wewe hauupendi hata kidogo na ambao ukiusikia unapigwa unahisi umeguswa na kitu chenye ncha kali?