Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siuelew kabisa kaka labda uniletee zile walizofanya watu timamu kama kina Joseline, Line, Jaydee, Bell 9, Dullayo, nk.Du! Kumbe watu wengi huu muziki wa bongofleva hauwaingii akilini? Nilifikiri ni mimi tu.
Hapa kwako naongeza na Taarab na mdundiko sijui wanaita zile...Singeli, mchiriku
Nimesema siuchukii muziki kwa ujumla wake, nitachukia nyimbo fulani kwa sababu haijaimbwa vizuri.Je, muziki wa bongofleva unauelews mkuu?
Ule wa south Afrika..Hahaha! Amapiano ni muziki wa aina gani mkuu? Unaweza kuweka mfano tuusikie? Inaonekana watu wengi hawapendi aina hii ya muziki.
Yah zote hizo kina Ferooz yan game ya kitambo 💯 💯Na pia miziki ya akina Sugu na Profesa J ina mashairi yanayoeleweka mkuu.
ku-sample na kuiga kumekuwa kwingi mno, unasikiliza wimbo mwanzoni lakini hujui ni wa nani, melody inafanana, beat inafanana au wimbo utolewe vocals basi haujulikani nani kaimbaUnadhani ni nini kilichoharibu muziki wa bongoflrva wa kisasa mkuu?
Hapo umenena mkuu. Kumbe tupo wengi.Binafs nasikiliza...
1.Country
2.Reggae.
3.Hiphop.
Mara chache..
Bakurutu, Softlocks, RNB nk
Ukinikuta nje ya hapo basi kuna uniqueness nimeiona katika uimbaji wa msanii husika, huwa siwez kujinafikia nikuuelewa mziki hata kama ni singeli nasikiliza.
Ila Piano, Bongofleva za kileo, trap na ujinga mwingine NEVAAA.
Yaani kuna siku nilishuhudia watu wakiburudika na muziki wao lakini mm kila nikijaribu kusikiliza kama walau naweza kuambulia hata neno moja tu supatu kitu. Nilichokuwa nasikia tu ni: Selemani weee Selee.....tangu mwanzo hadi mwisho wa track. Nilisikitika sana junsi kizazi cha siku hizi kilivyotuharubua ladha ya muziki.Aina zote za muziki nasikiliza ikitegemea ndani ya muda niko na mood ya aina gani ya muziki isipokuwa taarabu
Ila nakubaliana na NAS alipoimba Hip Hop is dead hiki kizazi kipya cha young rappers wa Marekani sijawahi kuulewa muziki wao
Kweli kabisa mkuu. Umegusa mulemule.ku-sample na kuiga kumekuwa kwingi mno, unasikiliza wimbo mwanzoni lakini hujui ni wa nani, melody inafanana, beat inafanana au wimbo utolewe vocals basi haujulikani nani kaimba
tech imekuwa, electronic beats ndiyo zimepamba moto, PC inamaliza kitu kitu
ladha za instrumental beats huzisikii tena
kizamani, wimbo unasukwa na instrumentalist mpaka watatu, kuna mpiga drums hapo, kuna mpiga keyboard, kuna guitarist, kuna producer, na ni Bongo Fleva hiyo, ladha halisi za keys na strings unazisikia mpaka ndani kwenye mifupa