1. Rais apunguziwe madaraka ili baadhi anaowateua wathibitidhwe na Bunge!
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe huru, ie cmposition ya wajumbe wa tume ijumuishe pia wapinzani.
3. Tanzania sio tena nchi ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuwa njia kuu za uchumi zote haziko mikononi mwa Serikali. Kwahiyo Katiba ifanyiwe marekebisho kuondoa kipengele hicho!
4. Katiba ifanyiwe marekebisho iendane na Katiba ya Zanzibar, km kuondoa cheo cha uwaziri kiongozi!
5. Viti maalum vya ubunge na udiwani viondolewe, havina kazi yoyote.
6. Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wabunge, kwa kuwa hao wabunge hawawakilishi chochote.
7. Matokeo ya urais yawe challenged mahakamani, kwa hiyo kile kipengele kwamba Tume ikishatangaza matokeo basi hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kuyachunguza kiondolewe!
8. Rais asiwe na uwezo wa kubadili Wizara mara kwa mara, idadi ya wizara ziwekwe kwenye Katiba na kama ataona kuna haja ya kuziongeza Bunge liridhie. Hii itapunguza Rais kubadili Wizara kila mara, kwa kutaka kuwapatia maswahiba wake vyeo! Pia Wizara ziwe chache ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.
9. Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi waondolewe na badala yake wabaki Wakurufenzi watendaji wa Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya!
10. Muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu!
11. Kuwe na equal distribution ya resources badala ya kuconcetrate tu kujenga Dar es Salaam na baadhi ya mikoa. Kwa hiyo iwekwe mechanism kwenye Katiba, eg Swrikali za Majimbo zenye baadhi ya mamlaka juu ya resouces zilizopo maeneo yao.
13. Mgombea binafsi aruhusiwe Kikatiba!
14......