Taja Uongo mkubwa ambao ushawahi kuambiwa enzi za utotoni!

Utotoni kulikuwa na mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa na wakubwa wetu lakini baada ya kukua, ndio tukaja kugundua ilikuwa ni uongo!
Binafsi mimi nilikutana na haya;
1. Ukifukia soda ardhini ukiiacha wiki mbili itamea halafu inazaa utachuma, nililpofukia tu wakaichimba na kuinywa🤣🤣🤣daah walah..
2. Ngurumo wakati wa mvua ilikuwa ni mapipa yanapigwa mateke na mungu, mvua ni maji yaliyomwagika kutoka kwenye hayo mapipa[emoji23][emoji23]kwa kweli walitushinda...
3.Mwenzio akijamba usipotema mate utaota meno matakoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji38]
4.Ukikalia mafiga unapata majipu kwenye makalio....
5.Ukilia usiku, sauti yako itachukuliwa na mashetani[emoji39][emoji23][emoji23]🤣

Hebu tiririkeni hapa uongo ambao ushaambiwa, tutoe stress kidogo....
Niliambiwa mbwa kapotea kumbe yupo mafunzoni
 
hata hivyo watoto wa zamani tulikuwa wajinga mfano mtu anakutuma anakwambia nenda nitakupa pipi, mtoto wa siku hizi anakwambia nipe pipi kwanza ndo niende maana unanidanganya
 
Utotoni kulikuwa na mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa na wakubwa wetu lakini baada ya kukua, ndio tukaja kugundua ilikuwa ni uongo!
Binafsi mimi nilikutana na haya;
1. Ukifukia soda ardhini ukiiacha wiki mbili itamea halafu inazaa utachuma, nililpofukia tu wakaichimba na kuinywa🤣🤣🤣daah walah..
2. Ngurumo wakati wa mvua ilikuwa ni mapipa yanapigwa mateke na mungu, mvua ni maji yaliyomwagika kutoka kwenye hayo mapipa[emoji23][emoji23]kwa kweli walitushinda...
3.Mwenzio akijamba usipotema mate utaota meno matakoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji38]
4.Ukikalia mafiga unapata majipu kwenye makalio....
5.Ukilia usiku, sauti yako itachukuliwa na mashetani[emoji39][emoji23][emoji23]🤣

Hebu tiririkeni hapa uongo ambao ushaambiwa, tutoe stress kidogo....
Wakubwa hawajambi!
Watoto wananunuliwa!
 
Ukipigwa na mwiko wa ugali hauoi.
Kama kweli vilee.maana mama wa kambo kanichapa Sana na Miko.
Na mpaka sasa sijaoa Wala mpango sina
 
1.ukilala kwa kinu mpaka asubuhi unabadilika jinsia boy anakuwa girl,au girl anakuwa boy.
2.ukiwapiga kuku unageuzwa kama ile hadithi ya jogoo alomgeuza yule kijana kichwa chini miguu.
3.ukiota umeshika ela,kamatilia na uzinduke usingizini utazikuta kwa mkono wako.
 
Mama yangu aliniambiga kuwa watoto huwa wananunuliwa,kwa hiyo kila nilipokuwa napata mdogo wangu nilikuwa nafikiri ameenda kununuliwa sokoni.Nilikuja kugundua kuwa mtoto hanunuliwa wala nini nilipofika la saba!
Duuu!!! Ulichelewa sana[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Mimi la pili tayari najua[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ukilala mtu akakuruka,hutarefuka tena
 
Tukifa tunachomwa moto kama una mazambi..! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama yangu aliniambiga kuwa watoto huwa wananunuliwa,kwa hiyo kila nilipokuwa napata mdogo wangu nilikuwa nafikiri ameenda kununuliwa sokoni.Nilikuja kugundua kuwa mtoto hanunuliwa wala nini nilipofika la saba!
Unasitahili kabisa tuzo ya mtoto mjinga bora wa karne hii hata sayansi ya darasa la sita hukusoma?
 
Back
Top Bottom