Taja Vile Vitu/Mambo Yanayokukeraga Kila Siku za Maisha sema Husemi!!

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Kwenye maisha kuna vitu vingi vinatokea kila siku vingine vinafurahisha na vingine vinakera au vinakuchukiza sema hutakagi kusema tu.

Kwa mfano vitu vinavyonikera Mimi
Ni pale unapoenda kanisani Ila kipindi cha michango na matangazo kinakuwa kirefu kuliko mahubiri[emoji6][emoji6]

Kingine ni pale unapumuona dada flani analazimisha kuvaa nguo ambazo haziendani na maumbile yake...[emoji848][emoji848]

Na kingine ni pale unapoongea na mtu Ila hataki kukusikiliza anataka umsikilize yeye tu tena anatupia na mikono kabisa

Wakati mwingine unakuta umekaa kwenye basi alafu uliyekaa naye anakula kula tu mara mayai,mara viazi huwa inanikera [emoji34][emoji34][emoji34]

Unakuta mtu anakushauri hata mambo ambayo unajua unatakiwa kufanya "mdogo wangu soma sana elimu ni kila kitu"[emoji35][emoji35]
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ile kansani mchungaji anasema mkumbatie jirani yako au anasema mwambie jirani yako nakupenda[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mimi nachukizwa na hali ya kuombwa ombwa pesa hovyo na watu.. Haswaa wanaojitambua kuwa unazo
 
Mahubiri yangekuwa marefu unadhani yangekufanya kuwa mtu tofauti na ulivyo sasa
 
Mahubiri yangekuwa marefu unadhani yangekufanya kuwa mtu tofauti na ulivyo sasa
Ila wanasema human desires wants and needs change after every 10 years so I'm not the same person every day
 
Unajidai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…