Kwa kifupi MO asipobadilika atateseka sana hapo Simba na ataendelea kuwatesa wapenzi, mashabiki na wanachama wa Simba. Na Simba itateseka sana mpaka wanachama akili ziwakae. Kule Yanga Hersi na GSM ndio wametangulia mbele wanaonekana lakini huku nyuma kuna matajiri kibao wanachanga pesa kwa ajili ya usajili na kuendesha timu. Na sio kitu kigeni kwani hata "friends of Simba" ndio walikuwa wanautumia huu mfumo na uliwatesa sana Yanga kipindi kile. Sasa hivi wakati MO anajadiliana na kulialia apunguziwe fedha za usajili kwa mchezaji fulani wenzake upande wa pili nao wakimhitaji huyo huyo mchezaji wanaitana wanapiga "donations" fasta Hersi anapewa mzigo anaenda pindua meza Simba wanabaki wameduwaa.
Shida ya MO yupo peke yake na hataki watu wengine waingie kwa sababu anazojua yeye. Walau basi angefanya juhudi mchakato wa kuruhusu wanachama wapya waingie walau ingempunguzia maumivu ya yeye kutumia pesa nyingi peke yake kwani ada za uanachama zingemsaidia asitoe pesa nyingi peke yake. Mo alimkubali tu Hanspope (RIP) na alikuwa anajitolea sana na fitina za mpira alikuwa anaziweza ndio maana wakati ule Yanga wakitaka kusajili mchezaji ghafla unashtukia yupo Simba.
Kwa kifupi kusipokuwa na mabadiliko ya haraka pale Simba basi wanachama na wapenzi watakuwa wanaendelea kushangaa tu mchezaji fulani mzuri Simba wanaanza kumfuatilia mwisho wa siku anaishia Yanga. Na mabdiliko ni mawili tu aidha Mo akubali matajiri wengine na wanachama maarufu wapewe nafasi pale Simba yeye awe msimamizi wao kama anavyofanya GSM au waanze mchakato wa wanachama wapya ili klabu iingize pesa za ziada. Vinginevyo huu mburuzo hautaisha leo wala kesho na hata Yanga wanaposema watabeba "back to back" miaka kumi mfululizo wanaamanisha maana wameshaona huo udhaifu pale Simba.