Tajiri Uganda ajitangazia msiba ili kupima marafiki wa kweli

Joined
Sep 17, 2023
Posts
14
Reaction score
32
Jamani dunia Ina Mambo na vijimambo.

Tajiri mmoja nchini Uganda amewashangaza wengi.

Tajiri huyo alikuwa na wanawake 4 kama ipasavyo Suna ya kiislam.

Zamu ya mke mdogo ilipofika akaamua kuwa awadanganye watu kuwa amefariki ili awajue marafiki wa kweli.

Alimpa simu mke mdogo awapigie simu ndugu,jamaa,wake wenzie na marafiki awaarifu kuwa mmewe ashakata kamba😭😭

Mme huyo akajiwekea limit kuwa mtu atakayekuja saa tatu kamili mpaka saa Saba Basi huyo ndo rafiki yake wa kweli.

Kila aliyefika alikaribishwa ndani na kuchinjiwa ng'ombe,pombe kwa wingi na kila starehe na kuonya asitoe Siri.

Jambo la ajabu mke aliyeanza kufika amefika saa nne kesho yake asubuhi na wa pili saa tisa mchana kesho na mbaya zaidi mwingine hakuja hata msibani.

Wengi wamefurahi kujipatia karamu lakini wengine wanataka ashitakiwe😂
Sasa najiuliza Maswali atashtakiwaje wakati anataka awajue Marafiki 😂😂😂
Anyway sijui we unamshauri Nini?
 
Mleta mada unajiona mjanjaa kupiga kamba watu wazima?
 
Weka source.

Nyau ww
 
Hizo story za mtaani tu
 
Sio kipimo sahihi, usiishi kwa kukamilishwa na marafiki
 
Acha bangi
 
Awereness joke!!
 
Kama mtoa mada ni mwanaume na hizo emoj nitasikitika sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…