Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Mimi naogopa hata kuwaangalia kwenye picha. Ujasiliamali huo unahitaji ujasiri kwelikweli. Pesa yake nono lakini, mmmh hapana. Niko tayari kukuchangia lakini usinitumie hata picha zao.
 
Ni mradi mzuri sana na ni moja kati ya harakati za kujikomboa kiuchumi. Ila hapo kwenye usafi wa mara kwa mara ndipo patakapoleta matatizo. Hivi kuingia banda la nyoka mara tano au sita kwa siku si ndo kutafuta kifo cha kugongwa na nyoka!
 
Lipo mbeya nashukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri,nawashukuru watu wa Mali asili kwa ushirikiano na ushauri wanaonipatia
Kiongozi kama unautaalam wa kuwakamata, naomba msaada kuna nyoka wawili wapo kwenye bwawa langu la Samaki wamenikosesha raha nashindwa hata kuhudumia Samaki, njoo uchukue au unielekeze navyoweza kuwatoa
 
Haujasema changamoto unazokumbana nazo,na nyoka gani unaofuga.na hyo sumu uchukuliwa vipi?
 
Kati ya pesa na uhai ipi bora ,nyoka huyu huyu khaa
 
Unawahamisha unawaweka kwenye beseni special ,vifaa za kuwabebea nyoka kama fimbo zilizochepuka zenye kibanio kuwakamata nyoka shingoni na unawahamisha kisha unawarudisha

Hukai nao karibu bali unawapa Huduma na kuwapa matunzo vizuri
Faida yao ni hiyo sumu tu na kula panya?

Hawana mbolea?

Hawatoi maziwa? [emoji23]
 
Kwa hali hii jinsi ilivyo sishangai mtu kufuga nyoka kama ameweza kutoa kafara ya mama yake mzazi kwa kuusaka utajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…