Taka zimejazana sana eneo la Boko Magengeni, magari ya kubeba taka hakuna kwani?

Taka zimejazana sana eneo la Boko Magengeni, magari ya kubeba taka hakuna kwani?

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Uchafu umejazana sana eneo la Boko Mgengeni kwa siku kadhaa sasa na hakuna hatua iliyochukuliwa kutoa taka hizo ambazo zinasambaza halufu mbaya zaidi.

Mbaya zaidi taka hizo zimewekwa mbele ya maduka ya vyakula na dawa ambapo inaweza kupelekea mlipuko wa magonjwa ya mlipuko kama kipindupinu n.k

Je hakuna magari ya kuzoa taka ya kutosha katika manispaa za Dar,maana hili tatizo limeendelea kuwa kubwa kila siku.

Mamlaka zichukue hatua za haraka zaidi ili kuondoa hali hii ya kuzagaa taka ovyo katika maeneo ya Watu.

photo_2024-05-15_09-54-44.jpg
photo_2024-05-15_09-54-04.jpg
 
Back
Top Bottom