‘Take Your Boreholes Back to Canada’: Kauli ya Mbunge Gideon Mulyungi Yazua Hasira Mwingi

‘Take Your Boreholes Back to Canada’: Kauli ya Mbunge Gideon Mulyungi Yazua Hasira Mwingi

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Mbunge wa Mwingi Central Gideon Mulyungi amezua mjadala baada ya kuionya shirika la Lifewater Canada dhidi ya kuchimba visima katika eneo bunge lake bila kuhusisha jamii na ofisi yake.

Akizungumza katika hafla ya hivi karibuni, Mulyungi alisema shirika hilo lazima lishirikishe wananchi pamoja na Mbunge katika miradi yake, akiongeza kuwa lisipofanya hivyo linaweza “take your boreholes back to Canada.”

Kauli hiyo imevuta ukosoaji mtandaoni, baadhi ya Wakenya wakihoji kwa nini mradi unaolenga kuwapatia wananchi maji ungewekewa pingamizi kwa sababu ya namna viongozi walivyoshirikishwa.

Lifewater Canada ni shirika la misaada linalotekeleza miradi ya maji, usafi na sanitation. Nyaraka za mshirika wake nchini, STADA Kenya, zinaonyesha wamekuwa wakifanya kazi katika Kitui–Mwingi, wakichimba, kukarabati na kutengeneza visima. Kufikia ripoti yao ya 2024, STADA ilisema ilikuwa imechimba visima 30 kupitia ushirikiano huo.

Ni kweli kuwa community participation na accountability ni muhimu katika miradi ya maendeleo. Lakini kauli ya “rudisheni boreholes Canada” imeibua swali jingine kuhusu mahali ambapo consultation inaishia na siasa za credit zinaanza.

Ikiwa mradi unafuata sheria na unawapatia wananchi maji safi, je, kutomshirikisha mwanasiasa kunapaswa kuwa sababu ya kuuzuia - au maendeleo ya wananchi yanapaswa kuja kwanza?

HQfS3Vya8AAo4vq.jpg
 
Back
Top Bottom