Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Joseph Kasongwa Mwaiswelo, amesema utafiti wa taasisi hiyo uliofanyika mwaka 2020 umebaini kuwa asilimia 23 ya Watanzania, sawa na watu milioni 15, wanapenda rushwa. Aidha, matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa wengi wanachukulia kipindi cha uchaguzi kama "wakati wa mavuno," wakiona fursa ya kupata manufaa kupitia vitendo vya rushwa.