TAKUKURU chunguzeni uwekezaji wa Mo klabu yetu ya Simba

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Nawasalimu waungwana na wapenda maendeleo ya mpira wa Tanzania.

Mimi ni moja ya wadau ambao nilipongeza sana uamuzi wa klabu yetu ya Simba kubadili mfumo wake wa uendeshaji ili kujiendesha kisasa zaidi na mafanikio.

Mpira wa miguu unahitaji uwekezaji kuanzia usajili, benchi la ufundi, vituo vya kukuzia vipaji, uwanja wa mazoezi na mechi, maduka ya kuuzia vitu na bidhaa mbalimbali zitokanazo na nembo ya klabu nk
Lakini uwekezaji wowote katika soka letu liwe ngazi ya klabu au Taifa haupaswi kuwa wa ujanja ujanja.

Hivi karibuni nilimsikiliza anayetajwa kuwa mwekezaji wetu klabu ya Simba Ndugu Mohammed Dewji maarufu kama "Moo" alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo alisema wazi kuwa bado hajatoa kiasi cha fedha takribani bilioni 20 za uwekezaji kwa madai bado zoezi la tathmini ya mali na madeni kwa klabu ya Simba linaendelea... Hapa nikajiuliza maswali yafuatayo:-

1. Klabu haikuwa imejijenga kitaasisi hivyo inabidi tuunde mfumo wa kitaasisi utakaoweza kudhibiti fedha zisipotee ndio niweke kiasi kulingana na ripoti ya tathmini. Sasa yeye alipata wapi hamasa ya kusema atawekeza Simba SC kiasi cha bilioni 20 na sasa anasema haya, mwanzo hakujua?

2. Utaratibu unataka taarifa za tathmini ya mali na madeni uwe umefanyika halafu ripoti hii ya wataalam inawasilishwa kwa mtu anayetaka kuwekeza ili aweze kufanya maamuzi. Pia anadai kiasi cha bilioni 20 ni kikubwa sana kuliko thamani ya Simba SC... Sasa ilikuwaje akasema atawekeza kiasi cha bilioni 20 fedha za kitanzania kama hakuwa na ripoti hii ya tathmini ya mali na madeni, alitumia kigezo gani kutoa ofa hii?

2. Kama hana mkataba na Simba tafsiri yake ni kuwa fedha zote anazozitoa kwa ajili ya klabu kwa sasa ni mkopo? Kama ni mkopo yanaibuka maswali magumu hapo

i) Katika mechi zote za kimataifa za klabu ya Simba kuanzia mtoano hadi robo fainali katika uwanja wa Taifa ni bidhaa za Moo tu zilikuwa zikiuzwa uwanjani na nyingine ziliuzika kwa makubaliano na klabu ya Simba. Je, faida iliyopatikana kwa mauzo hayo na yeye hana mkataba na Simba, klabu inapata nini?

ii) Jezi za Simba zina nembo ya bidhaa yake 'Mo Energy' ambapo kwa kiasi kikubwa kinywaji hiki kimeuzika sana miongoni mwa mashabiki wa Simba... Sasa Moo hana mkataba na Simba inakuaje haya yote yanafanyika? Je, klabu inanufaika vipi? Wachezaji wetu wote na logo ya klabu inatumika kutangaza kinywaji chake cha 'Mo Energy' mabango yaliyopo mtaani ni ushahidi tosha... Ajabu klabu haina naye mkataba lakini yeye ananufaika na brand ya klabu... Huu ni uwizi na uhujumu uchumi wa klabu... Moo hawezi kuwekeza kiasi hicho cha fedha ni mjanja mjanja... Hatumtaki

iii) Moo anatajwa kuwa ndiye anayechapisha jezi za Simba na kuzileta nchini kwa ajili ya kuziuza, Je klabu inanufaika vipi?

3. Klabu ya Simba ndio yenye hisa 51% na Moo ana 49% sasa inakuaje Mwenyekiti wa klabu ya Simba asiwe mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi badala yake anakuwa Moo mwenye hisa chache?

4. 'Try Again' akiwa kaimu Rais wa klabu yetu ya Simba na ndiye aliyeongoza mazungumzo baina ya klabu na mwekezaji ambaye ni Moo mpaka mabadiliko yanapitishwa na Moo kukubaliwa kuwa mwekezaji. Ila baada ya muda mfupi Moo alimteua Try Again kuwa moja ya wakurugenzi wake ndani ya bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba.... Je, hiki si kiashiria kuwa Try Again hakuzingatia maslahi ya klabu wakati wa majadiliano?

5. Moo mwenye hisa chache (49%) ndiye anatuchagulia mtendaji mkuu wa klabu ambaye ni moja ya wakurugenzi wake aliowateua ambaye ni Ndugu Crescent Magori viongozi wapo tu.

6. Sued Mkwabi Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye yeye ndiye aliyebeba imani na matumaini ya wanachama wote wa Simba kutokana yeye ndio tulimchagua yupo kimya, kawa mnyonge... Ila viongozi njaa wapo kimya na ukisema wanakushambulia sababu wanatetea ulaji wao mmoja wapo ni msemaji mwenyewe wa klabu yetu.

Sisi Simba UKAWA tuna itaka TAKUKURU kuchunguza mkataba huu au sisi tutawaburuza mahakamani kina Try Again na Moo....!!!!!

Hata Aveva na Kaburu ni matokeo ya kuichezea klabu yetu hata hawa kina Moo, Try Again na Sued Mkwabi kuna viashiria vyote vya rushwa.

#SimbaNguvuMoja
 
Mo energy imeifazili simba milion 200 kuwa pale kweny jezi sio bure
 
Mmeanza majungu yenu? Mo hakujipa Simba vikao na mikutano ya wanachama imefanyika mpaka Serikali ikahusika,Hisa za Mo zikapunguzwa nyie mlikuwa wapi?Watanzania kama kilimo sio Siasa basi na Mpira sio Siasa na majungu.
 
Nikusahihishe, ni Mo na siyo Moo. Pili wenzio watakuita ombaomba fc sasahivi kwasabb ufahamu wao unatosha kuitwa mambumbumbu si zaid ya hapo. Simba jipsngane upya Mo alijaribu kwa singida united akafeli akaja kwa Africa Lyon akafeli cha ajabu akaibukia simba kawahadaa mmehadaika wengine wapo tayari kufanya chchte atakachosema Mo.

Mo ni bahiri sana hawezi akaweka hela mahali ambapo anajua hatapata faida.
 
Naweza kuku uliza swali? Wewe ni mfanyabiashara? Au unadhani kuwekeza Bilioni 20 ni kitu kidogo kama kuwekeza kwenye biashara ya karanga?

Umeusoma mkataba wa uwekezaji baina ya simba na mwekezaji? Au unadhani serikali niwajinga pamoja na propaganda zenu chafu juu ya mwekezaji wa simba imenyamaza?

wacheni ujinga na propaganda za kijinga juu ya maendeleo ya mpira. Mpira ni uwekezaji na uwekezaji ni biashara sio ridhaa.

ninyi mawazo yenu yako kwenye soka la ridhaa wakati zama za leo mpira ni biashara. Mo hawezi kuwekeza bilioni 20 bila kutengeneza mfumo utakao dhibiti wadokozi.

yaani watu wana ulizia bilioni 20 ili waanze kuzitafuna, mo ni mtoto wamjini anajua janja janja ya wapigaji ndio maana anataka utengenezwe mfumo utakao dhibiti mazingira ya ulaji wa mtaji wake.

leo unatoa bilioni 20 bila kujua mali na madeni kesho unaambiwa pesa yote imelipiwa madeni ambayo clab ilikua nayo! Uo sio wizi? Muwe mnatafakari kabla ya propaganda zenu.
 
Ndugu nahisi hujui business nahisi, emu jaribu kuuliza wataalamu wakupe mwanga, ulikuwa wapi unakuja kuchafua watu saivi? Elimu ilitumika kwa zaidi ya miezi sita juu ya hiki kitu, serikali imehusika , wasomi wamehusika juu ya mabadiliko haya, wanasheria na wajuvi zaidi yako wewe wamehusika. Wewe ni nani unaeanza kuchafua vitu pasipo na mantiki yeyote? Unahisi 20 bilion ni elfu mbili au? Unajua upigaji ulokuepo simba wewe? Alokwambia mo alitaka wekeza singida ni nani, ? Acheni ukilomoni ndugu!! Unadhani mabadiliko yanakuja kama unaenda chooni , hivi vitu vina process ndugu!! Mpira unahitaji uwekezaji, mpira hautaki siasa, mpira ni pesa, kama huelewi hivi vitu huna haja ya kuwa mshabiki wa simba nenda azam au yanga. Hatutaki watu wanaotaka kuturudisha nyuma.
 
"Muda utaongea" AVEVA anaitambua vizuri kauli hii.
 
Hoja zako hazina mashiko na ni husuda tu inayokusumbua.Mchakato wa mabadilko ndani ya Simba ulichukuwa takribani miaka miwili na uliridhiwa na wanachama kwa uwazi bila usiri na ukapigiwa kura tena chini ya usimamizi wa jaji anayeheshimika Thomas Mihayo na kwa baraka za Serikali tena ya awamu hii ya tano.Serikali ilikataa Mwekazaji kupewa hisa 51% hivyo ikaamuru mwekazaji atamiliki hisa si zaidi ya 49%.Mo kwa mapenzi yake kwa klabu ya Simba akakubali kutoa bilioni 20 na hii ni kianzio cha uwekazaji na inabidi izalishwe na itoe faida na sio pesa itolewe kama hisani.Eleweni hii ni kampuni ndani ya klabu ya Simba Sports club na kampuni ina haki ya kutumia nembo ya klabu kwa mujibu wa katiba. Kasome na uilewe katiba ya Simba Sports Club Company Ltd inavyosema na waliotunga hawakutokea magengeni, vijiweni bali ni wasomi na ilipelekwa kwa msajili na ikaridhia.Sasa unatuaminisha vipi kuwa MO analeta ujanja ujanja kama sio fitina, majungu na figisu figisu.
Sisi wanachama wenye hisa 51% ndio tuna mtihani wa kutafuta mtaji wa kutadhiminisha hizo hisa na sio kukodolea hizo 20 bilioni kuwa zinatolewa kama sadaka.
 
Hujielewi wewe kwa Tanzania ni Simba na Yanga tu ndo unaweza wekeza na ukafanikiwa angalia Azama hawana mafanikio yeyote yakutisha pamoja na uwekezaji wao

Alafu ulitaka Mo aweke pesa ili apate hasara ama acha uzu pumbav wewe
Nilijua lazima ungetoa povu, haya sasa mpeni hati mnyaturu kama mnayo ...vingine sijui mkashike ukuta ilikumshawishi atoe pesa bila hati. Mbumbumbu always is mbumbumbu
 
Mo ni tapeli, simba wakiboronga kombe la africa ndio akili itarudi, sasa hivi akili imezibwa na kutinga robo fainali , muda utaongea
 
Watu mnatolea macho 20b hivi hizo 51% mnazifikiaje mpaka sasa, akili fupi utazijua tu kutwa kushinda vijiweni kula kulala na elimu za machimbo
 
Wametumwa hawa kumchafua "Mo "
 
Huu ni uchafu wa maneno umetumwa wewe sio bure
 
Sidhani kama yanga wote wana akili kama hawa wanao chafua watu kisa ushabiki wa kijinga.

hivi mngekua na akili kidogotu ya kukopa na ninyi mngepambana timu yenu ipate uwekezaji na mabadiliko kama simba na sio kuvutana kwenye sufuria kama kaa. Hizi ni tabia za ukaa.

hatuwezi kuendelea kisoka kama timu hazita badilika na kujiendesha kibiashara.

Ni haibu timu zina miaka 70 hazina hata uwanja wa mazoezi? Na hiyo ni kwasababu ya kungangania mfumo wa kizamani kuendeshea timu.
 
Mmeanza majungu yenu? Mo hakujipa Simba vikao na mikutano ya wanachama imefanyika mpaka Serikali ikahusika,Hisa za Mo zikapunguzwa nyie mlikuwa wapi?Watanzania kama kilimo sio Siasa basi na Mpira sio Siasa na majungu.

Ndo shida ya watanzania wengi akili ndogo wamekalia majungu
 
Kwa Miaka 5 mlikuwa mnalia njaa akili za kukopa hamkuwa nazo?
Au ndio wale mnajiita simba club tajiri kwa kulinganisha na timu kubwa Africa wakati ukiambiwa mchezaji anauzwa 800M ponjoro anakimbia!
 
Wakati anavieleza vikao ikiwemo mkutano mkuu wa klabu kuwa atawekeza kiasi hicho alitumia vigezo gani kama hakuwa na taarifa ya kitaalam ya mali na madeni ya klabu? Huyu mjanja mjanja tu hawezi kuwekeza kiasi hicho
 
kwa kauli ya Moo mwenyewe hana mkataba na klabu yetu ya Simba hayo makubaliano unayoyasema ni yapi?
 
Kingwa kashakuwakilisha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…