SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Nawasalimu waungwana na wapenda maendeleo ya mpira wa Tanzania.
Mimi ni moja ya wadau ambao nilipongeza sana uamuzi wa klabu yetu ya Simba kubadili mfumo wake wa uendeshaji ili kujiendesha kisasa zaidi na mafanikio.
Mpira wa miguu unahitaji uwekezaji kuanzia usajili, benchi la ufundi, vituo vya kukuzia vipaji, uwanja wa mazoezi na mechi, maduka ya kuuzia vitu na bidhaa mbalimbali zitokanazo na nembo ya klabu nk
Lakini uwekezaji wowote katika soka letu liwe ngazi ya klabu au Taifa haupaswi kuwa wa ujanja ujanja.
Hivi karibuni nilimsikiliza anayetajwa kuwa mwekezaji wetu klabu ya Simba Ndugu Mohammed Dewji maarufu kama "Moo" alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo alisema wazi kuwa bado hajatoa kiasi cha fedha takribani bilioni 20 za uwekezaji kwa madai bado zoezi la tathmini ya mali na madeni kwa klabu ya Simba linaendelea... Hapa nikajiuliza maswali yafuatayo:-
1. Klabu haikuwa imejijenga kitaasisi hivyo inabidi tuunde mfumo wa kitaasisi utakaoweza kudhibiti fedha zisipotee ndio niweke kiasi kulingana na ripoti ya tathmini. Sasa yeye alipata wapi hamasa ya kusema atawekeza Simba SC kiasi cha bilioni 20 na sasa anasema haya, mwanzo hakujua?
2. Utaratibu unataka taarifa za tathmini ya mali na madeni uwe umefanyika halafu ripoti hii ya wataalam inawasilishwa kwa mtu anayetaka kuwekeza ili aweze kufanya maamuzi. Pia anadai kiasi cha bilioni 20 ni kikubwa sana kuliko thamani ya Simba SC... Sasa ilikuwaje akasema atawekeza kiasi cha bilioni 20 fedha za kitanzania kama hakuwa na ripoti hii ya tathmini ya mali na madeni, alitumia kigezo gani kutoa ofa hii?
2. Kama hana mkataba na Simba tafsiri yake ni kuwa fedha zote anazozitoa kwa ajili ya klabu kwa sasa ni mkopo? Kama ni mkopo yanaibuka maswali magumu hapo
i) Katika mechi zote za kimataifa za klabu ya Simba kuanzia mtoano hadi robo fainali katika uwanja wa Taifa ni bidhaa za Moo tu zilikuwa zikiuzwa uwanjani na nyingine ziliuzika kwa makubaliano na klabu ya Simba. Je, faida iliyopatikana kwa mauzo hayo na yeye hana mkataba na Simba, klabu inapata nini?
ii) Jezi za Simba zina nembo ya bidhaa yake 'Mo Energy' ambapo kwa kiasi kikubwa kinywaji hiki kimeuzika sana miongoni mwa mashabiki wa Simba... Sasa Moo hana mkataba na Simba inakuaje haya yote yanafanyika? Je, klabu inanufaika vipi? Wachezaji wetu wote na logo ya klabu inatumika kutangaza kinywaji chake cha 'Mo Energy' mabango yaliyopo mtaani ni ushahidi tosha... Ajabu klabu haina naye mkataba lakini yeye ananufaika na brand ya klabu... Huu ni uwizi na uhujumu uchumi wa klabu... Moo hawezi kuwekeza kiasi hicho cha fedha ni mjanja mjanja... Hatumtaki
iii) Moo anatajwa kuwa ndiye anayechapisha jezi za Simba na kuzileta nchini kwa ajili ya kuziuza, Je klabu inanufaika vipi?
3. Klabu ya Simba ndio yenye hisa 51% na Moo ana 49% sasa inakuaje Mwenyekiti wa klabu ya Simba asiwe mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi badala yake anakuwa Moo mwenye hisa chache?
4. 'Try Again' akiwa kaimu Rais wa klabu yetu ya Simba na ndiye aliyeongoza mazungumzo baina ya klabu na mwekezaji ambaye ni Moo mpaka mabadiliko yanapitishwa na Moo kukubaliwa kuwa mwekezaji. Ila baada ya muda mfupi Moo alimteua Try Again kuwa moja ya wakurugenzi wake ndani ya bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba.... Je, hiki si kiashiria kuwa Try Again hakuzingatia maslahi ya klabu wakati wa majadiliano?
5. Moo mwenye hisa chache (49%) ndiye anatuchagulia mtendaji mkuu wa klabu ambaye ni moja ya wakurugenzi wake aliowateua ambaye ni Ndugu Crescent Magori viongozi wapo tu.
6. Sued Mkwabi Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye yeye ndiye aliyebeba imani na matumaini ya wanachama wote wa Simba kutokana yeye ndio tulimchagua yupo kimya, kawa mnyonge... Ila viongozi njaa wapo kimya na ukisema wanakushambulia sababu wanatetea ulaji wao mmoja wapo ni msemaji mwenyewe wa klabu yetu.
Sisi Simba UKAWA tuna itaka TAKUKURU kuchunguza mkataba huu au sisi tutawaburuza mahakamani kina Try Again na Moo....!!!!!
Hata Aveva na Kaburu ni matokeo ya kuichezea klabu yetu hata hawa kina Moo, Try Again na Sued Mkwabi kuna viashiria vyote vya rushwa.
#SimbaNguvuMoja